Dhehebu la UMCA lilichapisha vitabu kufuatia mtindo uliotumiwa
katika kuchapisha vitabu vya Steere. Misheni wa Kizungu walifanana na
waanzilishi wa uchunguzi wa Kiswahili kwa kuwa ilikuwa rahisi kwao
kutumia hati za Kirumi badala ya zile za Kiarabu. Mkutano wa Dar es
Salaam wa 1925 uliamua kutozitumia hati za Kiarabu pamoja na
konsonanti za Kiarabu kama vile kh. 18* Uamuzi huu wa l925 uliwakasirisha
wengi wakiwa ni pamoja na gazeti la Mombasa, Al-Islah, kama ilivyo-
jadiliwa kwa kireru katika sehemu ifuatayo.
Profesa Carl Meinhof alipohudhuria mkutano wa Mombasa wa 1928,
waliohudhuria walikuwa na nafasi ya kushauriana naye kuhusu othografia
ya Kiswahili. Meinhof alikubaliana na nyingi kati ya tahajia iliyopendeke-
zwa kwa kuwa ilikuwa rahisi bila kutatanisha, isipokuwa katika herufi ch
na ng'. Meinhof alipendekeza c itumiwe badala ya ch. Badala ya kutumia
alama tatu za maandishi (ng') kusimamia sauti moja, alipendekeza
kutumiwa kwa n yenye mkia itumiwe kama ilivyo katika maandishi ya
kifonetiki.
Lakini mashauri haya ya Meinhof hayakukubaliwa. Wasomi wa
Kiswahili wakati huo walijiona kuwa sahihi, na kwamba mapendekezo ya
Meinhof yalifaa tu katika maandishi ya kifonetiki katika isimu lakini
hayakufaa othografia ya kawaida ya Kiswahili.
Achana Naye Boya huyo!Baada ya ufafanuzi uliopewa hapo juu ndio umepata hitimisho kuwa kiswahili ni CHOTARA?.
Mkuu kiswahili ni KIBANTU full stop.
Kwanini kibantu? lugha zote duniani zina asili yake na asili ya kiswahili ni kibantu kwa maana ya kuwa iliasili utamkwaji aka rithm au kwa maana nyingine pronaunciation yake ni ya kibantu licha ya kukopa maneno lukuki kutoka katika kiarabu.
Moja ya sifa ya lugha ni namna unavyotamka maneno pronaunciation, ndio maana mengi ya hayo maneno ya kiarabu hayatamkwi exactly kama waarabu wenyewe wanavyo yatamka na kuyaandika.
Kibantu si kabila ila inamaana ujumla wa makabila yaliyozaliwa katika asili moja yanayo share baadhi ya maneno na utamkwaji na hii inafanya kiswahili kuwa kibantu.
Najua kwanini katika wote waliotoa michango umemkubali zaidi ZOMBA ni kwasababu unaelekea kuipeleka hoja hii ktk udini, ionekane atutaki kusema ni kiarabu kwakuwa kiarabu kina uislam ndani yake(which is not true) naamini ndugu yangu umepitia madrassa unaweza kulinganisha maneno mliyojifunza huko kimatamshi yapo sawa na yaliyotoholewa kuwa kiswahili? mfano sahil na mswahili, ni wazi utamkwaji upo tofauti yaliyotoholewa yanatamkwa ktk tone ya kibantu.
Mwisho mkuu zomba inferiority complex ndio inayo kusumbua wewe na wenzio mnaodhani watu wapo kupinga uislam tu, hapana watu wapo bize kujenga mahospitali, mashule, mavyuo mabenki nk ili watu kama ninyi mpate huduma huko serikali iliposhindwa na si kukomalia kiswahili ni kiarabu, haiwasaidii
Kiswahili sio kibantu wala kiarabu, Kiswahili ni Kiswahili tudah! Mpka sasa bado cjaelewa kiswahl ni nini mana naona mnanizungusha kama 2livyokuwa 2nazungushana mana cjaelewa kiswahl ni nini labda kama ikiwezekana itakuwa vzur ukinipa hstoria ya kiswahili