Kiswahili ni Kibantu au Kiarabu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiswahili ni Kibantu au Kiarabu?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by MUREFU, Jan 10, 2011.

 1. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  WanaJF ninaomba 2saidiane mana 2libisha sana kiasi kwamba 2meshndwa kuelewa nan yupo sawa
   
 2. s

  saif ali New Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kiswahili ni mchanganyiko wa lugha kama sita hivi ndio umezaa Kiswahili. Ingawaje aghalabu ya maneno ni Kiarabu lakini tusiseme kiswahili ni Kiarabu si sahihi.
  Kwani humo kimo Kiiingereza,Kireno,Kihindi,Kifarisi,Kiarabu na Kibantu chenyewe.
   
 3. Tekelinalokujia

  Tekelinalokujia JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Chotara
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Umesahau kijerumani!
   
 5. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  lugha zote hizo za kibantu na kiarabu zimo kwenye kiswahili pamoja na nyinginezo kama kijerumani, kireno, kiingereza, kifaransa n.k.
   
 6. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kiswahili ni kibantu kilichochanganyika na lugha nyingine nyingi.
   
 7. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  dah! Mpka sasa bado cjaelewa kiswahl ni nini mana naona mnanizungusha kama 2livyokuwa 2nazungushana mana cjaelewa kiswahl ni nini labda kama ikiwezekana itakuwa vzur ukinipa hstoria ya kiswahili
   
 8. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  duh! Sasa huyu atakuwa njiwa kama co mpemba
   
 9. N

  Nonda JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
 10. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kiswahili ni Kiswahili period.

  Lugha nyingi i.e Kijerumani, Kiingereza, Kireno, Kibantu etc, ni mchangiko wa lugha mbali mbali pia. Kama lugha hizi zinavyotajwa kwa majina bila kuangalia origin, basi na Kiswahili kitabakia Kiswahili tu.
   
 11. N

  Nonda JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Kiswahili ni kibantu, si kiarabu.
  Kiswahili kina maneno yenye asili ya kiarabu, kwa 44% tu. Na lugha zote duniani huazima, hukopa maneno kutoka katika lugha nyengine na kuyatohowa. Yakishapita hatua hiyo huwa ni maneno ya lugha husika siyo tena ya kule yalikoopolewa.

  Ukubwa wa Tanzania ulivyo, na lugha zaidi ya 120, tumshukuru Nyerere aliyefanya juhudi kuieneza lugha hii ili kutuunganisha kama taifa.
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Asilimia kuubwa ya maneno ya kiswahili yanatokana na Kiarabu, hakuna lugha duniani inaitwa kibantu, kibantu ni mchanganyiko wa lugha nyingi za watu wenye asili ya kibantu. Watu wenye asili ya kibantu hupatikana kusini mwa sahara. Wale wa Afrika wengine wasio wabantu, ambao na hapa kwetu wapo wengi tu, kama vile wamasai, waIraqw, waRangi, wa Zanaki, waJaluo na kadhalika, utakuta wana asili za kiarabu kwenye lugha zao. Ikumbwe pia uArabu ni lugha na si utaifa. Kuna mataifa mengi katika Afrika yanayoongea kiarabu na wao hujiita wa Arabu, si kwa uTaifa bali kwa lugha.

  Ukichukuwa Kiarabu na lugha ambazo si za kibantu lakini za kiafrika zilizongiza maneno yake kwenye kiswahili utakuta kuwa maneno ya lugha za kibantu si mengi sana katika kiswahili, hayawezi fika asilimia 40%, asilimia chache zingine zinatokana na lugha za nchi ambazo zilikuwa na muingiliano mkubwa wa kibiashara na utawala katika pwani ya afrika mashariki, kama vile Kireno, Kijerumani, Kiingereza, Kihindi, Kichina.

  Duniani, kila mawasiliano yanavyozidi ndio lugha huchukuwa maneno kila muingiliano wa mataifa unapozidi, ni lugha chache sana zinazojitolesheza na maneno yake yeneyewe, na hizi ni lugha za zamani na huitwa kugha tajiri, utajiri wa kuwa na maneno mengi.

  Kiswahili kimebahatika kuwa na maneno mengi ya Kiarabu (Kiarabu ni Lugha tajiri) na nadhani ni hivi ppunde tu na chenyewe kitakuwa moja ya lugha tajiri.

  Kwa sasa, kuna hujuma za wazi za kukitowa kishahili kutoka uasili wa kiarabu kwa sababu tu uarabu unahusishwa na uIslaam. Kilanjia zinafanyika kubuni maneno mapaya ambayo hayana hata msamiati wala lafdhi za kiswahili, ili mradi tu, kitoke kwenye asili yake ya asili.

  Baraza la kiswahili limeingiliwa na watu wasio na asili ya lugha ya kiswahili. Wenye asili ya lugha ya kiswahili ni watu wa pwani ya Afrika Mashariki na wanaoongea kiswahili kama lugha mama.

  Hta neno ki- swahili lenyewe linatokana na kiarabu "sahil", pwani, "sawahil" watu wa pwani.
   
 14. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  kaka Zomba umeongea vizuri sana hapo mwanzo wa maelezo yako na nilikuwa nakufata vizuri tu, lakini huku mwisho umemliza kwa kuboa, Hivi kwa nini kila kitu mpaka uingize mambo ya uislamu,
  Hivi wewe ni mdini kiasi hicho ama? tatizo ni nini hasa?
   
 15. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kwa baadhi ya watu ni UJIKO kuona kuwa socially wana uhusiano wa karibu na waarabu. Watu wa namna hiyo watakwambia, kiswahili kina MANENO YA KIARABU zaidi ya asilimi 60 au hata 70.
  Hata hivyo ukipata watu ambao wapo objective, utaona wanaonyesha kuwa MANENO YENYE ASILI ya kiarabu si zaidi ya asilimia 40.
  Na kiswahili kama lugha inaelezwa wazi kuwa ni one of the bantu languages kama inavyoonesha hapa kwenye Encyclopaedia britannica
  Swahili language (African language) -- Britannica Online Encyclopedia
   
 16. Nyasirori

  Nyasirori Senior Member

  #16
  Jan 11, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 186
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Zomba,
  Una uhakika makabila yote uliyotaja hapo juu si ya kibantu? Mimi nimesoma shule na wazanaki. Siku moja mwalimu akiwa anafundisha somo la kiswahili, akatolea mfano ulioonyesha ni kabila la kijaluo tu katika waliotakiwa kutaja neno maji, kwa makabila yao. Wakati wengine wote walitaja maneno yaliyoelekea kufanana kwenye tamshi maji, ni mjaluo tu aliyetaja tofauti. Sijui kwa makabila mengine, ila nahisi wazanaki uliowataja hapo wako kwenye group la wabantu.
   
 17. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  thanks sana bwana ZOMBA mana nimekuelewa na nimeelewa na utata sasa unaisha mana mbish na mpinzan wangu kakubal yan nilikuwa cjui mengne ila nimeelewa kwel wanaJF mmenielimisha yan kiswahl ni CHOTARA
   
 18. P

  Paul S.S Verified User

  #18
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Baada ya ufafanuzi uliopewa hapo juu ndio umepata hitimisho kuwa kiswahili ni CHOTARA?.
  Mkuu kiswahili ni KIBANTU full stop.
  Kwanini kibantu? lugha zote duniani zina asili yake na asili ya kiswahili ni kibantu kwa maana ya kuwa iliasili utamkwaji aka rithm au kwa maana nyingine pronaunciation yake ni ya kibantu licha ya kukopa maneno lukuki kutoka katika kiarabu.
  Moja ya sifa ya lugha ni namna unavyotamka maneno pronaunciation, ndio maana mengi ya hayo maneno ya kiarabu hayatamkwi exactly kama waarabu wenyewe wanavyo yatamka na kuyaandika.
  Kibantu si kabila ila inamaana ujumla wa makabila yaliyozaliwa katika asili moja yanayo share baadhi ya maneno na utamkwaji na hii inafanya kiswahili kuwa kibantu.
  Najua kwanini katika wote waliotoa michango umemkubali zaidi ZOMBA ni kwasababu unaelekea kuipeleka hoja hii ktk udini, ionekane atutaki kusema ni kiarabu kwakuwa kiarabu kina uislam ndani yake(which is not true) naamini ndugu yangu umepitia madrassa unaweza kulinganisha maneno mliyojifunza huko kimatamshi yapo sawa na yaliyotoholewa kuwa kiswahili? mfano sahil na mswahili, ni wazi utamkwaji upo tofauti yaliyotoholewa yanatamkwa ktk tone ya kibantu.
  Mwisho mkuu zomba inferiority complex ndio inayo kusumbua wewe na wenzio mnaodhani watu wapo kupinga uislam tu, hapana watu wapo bize kujenga mahospitali, mashule, mavyuo mabenki nk ili watu kama ninyi mpate huduma huko serikali iliposhindwa na si kukomalia kiswahili ni kiarabu, haiwasaidii
   
 19. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  thank PAULSS kwa maelezo yako ninaweza kusema hamkumuelewa vzur ZOMBA kwa maana alijieleza vzur kuhusu chimbuko la kiswahl na akachambua ni namna gan kiswahl kinavyopotea pia so hakuwa na maana mbaya sana ila co mbaya kama alikosea kudokeza udin ila mm nilimuelewa vzur na wewe PAULSS unavyosema kibantu co kabisa sawa ninajua ni muunganiko wa makabila ila nachelea kukuelewa bale unaposema kuwa vitamkwa ndo vinavyosababisha kuhamisha lugha so mfano kichna akitamka tofaut na vle inavyotakiwa na cc 2kachukuwa 2tasema hvyo 2navyoelewa au ndo?
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mimi ni muIslam na kama uIslam wangu unakufanya unione mdini basi hayo ni maono yako.

  Nani asiejuwa kuwa uIslam unahusishwa na uArabu ingawa wa Arabu ni asilimia chache sana kati ya Waislaam wa duniani.

  Kiswahili kina maneno mengi mazuri lakini utakuta hayatumiki na yanabuniwa mengine mapya ambayo hayana asili ya uswahili. Lugha si kubuni maneno tu, hayo maneno yanayobuniwa yafanane na lafdhi za kiswahili ili kukipa raha yake ya asili kiswahili chetu kitamu.
   
Loading...