Asili ya Kiswahili na Waswaheli

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,928
Tulifundishwa shuleni kuwa Kiswahili kilikuja kwa kuchanganya Kiarabu na lugha mbalimbali za Kibantu. Hata hivyo, hiyo haikuwa kweli. Waarabu na Wazungu walipofika pwani ya Afrika Mashariki waliwakuta Waswahili/Wangozi wakizungumza Kingozi/Kiswahili. Kiswahili/Kingozi ilikuwa lugha ya zamani yenye lahaja nyingi. Kiswahili ni lugha ya wenyeji ambayo asili yake ni Lamu, Kenya. Sarufi ni kibantu 100% inayoifanya kuwa lugha ya Kiafrika. Chanzo cha Kiswahili kilikuwa ni lugha ya Kingozi ambayo ilizungumzwa na Wangozi. Wangozi siku hizi wanajulikana kama Waswahili na wamepangwa katika mfumo wa koo wanazoziita 'Mbari'. Koo 10 za Waswahili na koo ndogo 41. Koo na koo ndogo ni kama ifuatavyo:

1. MBARI ZA WAKILINDINI

Mbari ya Mwinyi Nguti wa Mwinyi Mwinzagu
" Mwinyi Humzi
" Mwinyi Kombo wa Dani
" Mwinyi Kae wa Pembe
" Mwinyi Hudumzi

2. MBARI ZA WATANGANA

Mbari ya Mwinyi Muli
" Mwinyi Mjaka
" Mwinyi Umbwi
" Mwinyi Ngwisa

3. MBARI ZA WACHANGAMWE

Mbari ya Mwinyi Kitue
" Mwinyi Mgosi
" Mwinyi Mfaki
" Mwinyi Koba
" Mwinyi Ngovo

4. MBARI ZA WAMVITA

Mbari ya Mwinyi Kutani
" Mwinyi Kae
" Mwinyi Hunziali

5. MBARI ZA WAMALINDI

Mbari ya Banu Shasha
" Banu Mbwana

6. MBARI ZA WAJOMVU (au WAJUNDA)

Mbari ya Mwinyi Faki
" Mwinyi Chande wa Shamaniya
" Mwinyi Usi Muhija
" Mwinyi Uledi wa Ndau
" Mwinyi Jaa wa Mwinyi Nguti

7. MBARI ZA WAMTWAPA

Mbari ya Mwinyi Nyali (au Mbari ya Ng'ombeni)
" Mwinyi Jimve
" Mwinyi Goziadi
" Mwinyi Rakwe
" Banu Muyaka
" Banu Shemapwe

8. MBARI ZA WAKILIFI

Mbari ya Mwinyi Shoka
" Mwinyi Kiwanda
" Mwinyi Mkomati
" Mwinyi Gome

9. MBARI ZA WAPATE

Mbari ya Wa-Pate
" Wa-Amu
" Wa-Kitau
" Wa-Twaka
" Wa-Tikuu
" Wa-Kipungani
" Wa-Barawa
" Wa-Shela

10. MBARI ZA WAGUNYA (au WABAJUNI)

Mbari ya Washaka
" Wa-Uziwa
" Wa-Ungama
" Wa-Ozi
" Wa-Sada

These clans speak different Kiswahili dialects depending on where they are found, especially in Kenya, Comoros, Mozambique, Somalia & Tanzania. The dialects are:

1. Shikomor spoken Comoros

2. Kiamu, Kipate & Kingozi are spoken in Lamu,

3. Chijomvu, Kimvita, Kingare, Kimrima, Kiunguja, Mambrui, Chichifundi, Chwaka & Kivumba are spoken in Mombasa,

4. Kipemba, Kitumbatu, Kimakunduchi, Mafia, Mbwera, Kilwa (extinct) & Kimgao are spoken in Pemba.

Oldest Kiswahili/Kingozi dialects include:

1. Kimwani which is spoken in the Kerimba Islands and northern coastal Mozambique

2. Chimwiini which is spoken by the ethnic minorities in and around the town of Barawa on the southern coast of Somalia.

3. Kibajuni which is spoken by the Bajuni minority ethnic group on the coast and islands on both sides of the Somali–Kenyan border and in the Bajuni Islands (the northern part of the Lamu archipelago) and is also called Kitikuu and Kigunya

4. Socotra Swahili (extinct) and

5. Sidi in Gujarat, India (possibly extinct)

As speakers of Kiswahili language we are owed this information. We should not be speaking a language whose origin we don't clearly know.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulifundishwa shuleni kuwa Kiswahili kilikuja kwa kuchanganya Kiarabu na lugha mbalimbali za Kibantu. Hata hivyo, hiyo haikuwa kweli. Waarabu na Wazungu walipofika pwani ya Afrika ...

Hapa Kuna shida ya udhibiti wa Historia. Sababu hatuna Historia yenye mashiko, inabaki ya kuwa Kiswahili ni chotara.

Kuna Waswahili, Kuna kiongozi na Kuna Kiswahili.
 
Nilisoma hii makala sehemu fulani.
Whatever the case, hizo sehemu ulizotaja mpaka leo zimeathiriwa na Waarabu na Uislam.
Kwa ufupi huwezi kukitenganisha Kiswahili na Uislamu hasa katika utamaduni na msamiati, yaani Kuna msamiati wa Kiarabu na ule kidini.

Lakini watu huuliza, kipindi Waarabu wanakuja katika pwani hii, wenyeji walikuwa wanaongea lugha gani na ilikuwa lini ?

Lakini ukimsoma Ibn Batuta amewaongelea watu miaka mingi kabla ya kufika Mreno, akataja na tamaduni zao. Rejea kitabu chake kiitwacho "Rihla".
 
Lugha hubadilika badilika as times passes, kwa kukaribisha misamiati mipya, lafudhi n.k
Watu walikuwepo na walikua wanawasiliana. Kuja kwa Kiarabu kukaathiri lugha zetu za asili. Zamani hata Kiswahili chenyewe kiliandikwa kwa herufi za Kiarabu hasa babu zetu ambao hawakusoma Kizungu.
Hili nimelishuhudia kwa macho, si jambo la kuhadithiwa.
 
Sio "Misamiati" sahihi ni "Msamiati".

Lugha inabadilika kwenye nini ? Msamiati au Sarufi ?

Unayo Historia ya Kiswahili ? Imeandikwa lini kwa mara ya kwanza ?

Naam, hoja yako ni nini katika nilichokiandika ?
 
Wazee wetu sijui walifeli wapi, yaani hawakuandika historia popote na kiarabu walikijua enzi hizo.

Wazee wa waliozaliwa miaka ya 1940's mpaka karibu na 70's hasa walioenda shule wengi wana vidaftari au vinotebook wanaandika matukio muhimu kila siku.
Hii ilitusaidia sana babu alipofariki kujua wanaomdai na anaowadai, maeneo yake yote na vitu vingine vingi alivyokua akiandika.

Miaka ya hivi karibu vijana na kina baba hatufanyi hivyo, pamoja na tech kukua bado hatuweki kumbukumbu.

Labda ni asili yetu, sisi sio watu wa historia.
 
Sio "Misamiati" sahihi ni "Msamiati".

Lugha inabadilika kwenye nini ? Msamiati au Sarufi ?

Unayo Historia ya Kiswahili ? Imeandikwa lini kwa mara ya kwanza ?

Naam, hoja yako ni nini katika nilichokiandika ?
Asante. Sina hoja.
Kaa kwa kutulia.
 
Watu wote wanao ongea kiswahili wanayo lugha yao ya asili. Sasa hawa wangozi lugha yao ni ipi? Ikiwa wadai kiswahili pekee ndio lugha yao basi itakua lugha yao ya asili imepotezwa kwa kwa kutumia kiswahili.
Hili litatokea kwa lugha nyingi hapa Afrika Mashariki zitapotea sababu ya matumizi ya kiswahili.
 
Yaani maandishi yooote hayo ajili tu kupinga kiarabu kuwemo kwenye kiswahili?
Basi tufanye kiswahili kimo kwenye kiarabu

Unajua fanyeni mfanyavyo lakini hamuwezi kukitofautisha kiswahili kuiba kutoka kiarabu kabisaaa, hili halina mjadala
 
Kwani kuna umaalumu gani kwenye kiarabu? Nayo si lugha tu kama kiswahili?

Kenapa ada kepakaran dalam bahasa Arab? Bukankah ia hanya bahasa seperti Kiswahili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ufupi huwezi kukitenganisha Kiswahili na Uislamu hasa katika utamaduni na msamiati, yaani Kuna msamiati wa Kiarabu na ule kidini.

Lakini watu huuliza, kipindi Waarabu wanakuja katika pwani hii, wenyeji walikuwa wanaongea lugha gani na ilikuwa lini ?

Lakini ukimsoma Ibn Batuta amewaongelea watu miaka mingi kabla ya kufika Mreno, akataja na tamaduni zao. Rejea kitabu chake kiitwacho "Rihla".
Hili swali nimejiuliza sana kabla ya kuja waarabu walikuwa wanaongea lugha gani?

Ninavyojua mimi ni kwamba waarabu na wageni walileta ty baadhi ya misamiati na maneno...Sema kuchaguliwa kwa lahaja ndio kunafanya waswahili wawe na lugha nzuri hata ingechaguliwa kanda fulani basi wao ndio wangekuwa vinara...

Pia ni kwa vile waswahili walipitiwa na wageni wote kwa sababu wageni walianza kufikia pwani..kuna maneno ya kijeruman, Kingereza , kiarabu kweny lugha ya kiswahili.
 
Kwa ufupi huwezi kukitenganisha Kiswahili na Uislamu hasa katika utamaduni na msamiati, yaani Kuna msamiati wa Kiarabu na ule kidini.

Lakini watu huuliza, kipindi Waarabu wanakuja katika pwani hii, wenyeji walikuwa wanaongea lugha gani na ilikuwa lini ?

Lakini ukimsoma Ibn Batuta amewaongelea watu miaka mingi kabla ya kufika Mreno, akataja na tamaduni zao. Rejea kitabu chake kiitwacho "Rihla".
Rihla ni neno la kiarabu na linatumika kwenye kiarabu.
 
Back
Top Bottom