Kiswahili kimezidi mno kuelemea kwenye Kiarabu zaidi ya Kibantu. Je, upendeleo wa Uarabu dhidi ya Ubantu?

Ngekewa,
Ahsante Mkuu kwa uchambuzi mahiri. Nashangaa sana na maneno luninga na jokofu na nakumbuka maneno ya kulazimisha kama vile kukarabati, zahanati na mengineyo ambayo yanawapa taabu watoto nyumbani kutamka. Kiswahili jamani na kiwe kiswahili na tukiwache kinyumburuke katika hali asilia na siyo kukilazimisha
 
kwenye kiswahili kuna Kichina,kama neno chai limetokana na neno CHA(茶) la kichina,kuna mchina mmoja alikuja pwani ya Africa ya mashariki akaona majani ya Chai na kuwaambia watu kuwa hii ni Chai,ila sipati picha walikuwa wanazungumza lugha gani,jamani..
 
Mahmoud Qaasim,

Swadakta, umeiweka wazi kabisa kiasi cha kunifanya niulize, Jee wana JF ni nani humu ambae hana shemeji, shangazi, mjomba, mama mdogo, rafiki au japo jirani mwenye asili ya ki-Arabu? Na wangapi wenye hao wenye asili zingine, mfano kizungu, kihindi?

Hata Mtindio ana shemeji wa ki-Arabu...
 
Ameshasema kiswahili kinampiga chenga, atatumia kiingereza pale atakaposhindwa. Sasa wamlazimisha?

"Seriously, I think there is an over-arabization of Kiswahili from its conception to this day."

Hicho cha wazungu hapo juu amesema amejaribu kutumia kiswahili kashindwa!

Nadhani aweza kuwa ni mwenyeji wa sehemu za ndani ndani za Tanzania ambako wanaongea kiingereza!
kuhani yuko sahihi kabisa.........steved umeleta ,ada ya kiswahili na maneno ya kingereza....kama sijakosea kuna sehumu nilishakuambia kuhusu hilo....

.....kuhani kasema kweli......nami nasema wabongo ni malimbukeni.....ukikutana nao yes yes noo nyingi eti kasahau kiswahili......
XP... unisamehe mkuu. The chicken has just arrived at a once dormant roost..
Mleta mada ya kiswahili kaanza upupu wa kikoloni.....
 
kuhani yuko sahihi kabisa.........steved umeleta ,ada ya kiswahili na maneno ya kingereza....kama sijakosea kuna sehumu nilishakuambia kuhusu hilo....

.....kuhani kasema kweli......nami nasema wabongo ni malimbukeni.....ukikutana nao yes yes noo nyingi eti kasahau kiswahili......

Mleta mada ya kiswahili kaanza upupu wa kikoloni.....

Na wewe "ada" ndio nini? Kwani tuko shuleni hapa? Ebo!

Na "sehumu" ni neno la lugha gani? Ki-Yo Yo?

Safari ijayo hakikisha unapomkosoa mwenzako kuhusu lugha, ya kwako iko sahihi.....
 
Asante kwa swali lako. Sidhani ya kwamba Kiswahili kinaweza kuachana na msingi wake jinsi kilivyokua kama mchanganyiko wa lugha za Kibantu na Kiarabu. (Juu ya historia soma wikipedia: Historia ya Kiswahili).

Kwa namna fulani ni lugha chotara - na lugha chotara zinaonekana kuwa na nguvu! Mfano bora ni Kiingereza ambacho ni mchanganyiko wa Kigermanik (Anglo Saxon) na Kifaransa cha kale. Tabia ya kuwa lugha chotara inarahisiha kupokea maneno mapya na kukua kwa lugha.
 
Kwa kweli kiasili Kiswahili ni lugha ya kichotara lakini hii si aibu. Lugha za kichotara zinastawi vizuri kwa sababu ni rahisi zaidi kupokea maneno mapya. Mfano mkuu ni Kiingereza ambacho ni mchanganyiko wa Kigermanik na Kifaransa cha kale; muundo wake unafanana na Kiswahili kwa sababu kuna msingi upande moja (Kiing.: Kigermanik; Kiswahili: Kibantu) na msingu huu ni sarufi pamoja na kiasi kikubwa cha msamiati halafu lugha ya pili iliyoingiza maneno mengi.

Kiingereza kiliweza kupokea kirahisi maneno mengi kutoka kote na kuimarika hivyo. Maneno ya Kisayansi ambayo tunajifunza kama "Kiingereza" si Kiingerza kiasili bado Kilatini au Kigiriki hasa ila tu Waingereza hawapigani nayo wanayapokea tu. Hapo ndipo pia nguvu moja ya Kiswahili ninavyoona na asili yake ya kichotara inasaidia sana. Kwa zaidi angalia hapa.
 
Na wewe "ada" ndio nini? Kwani tuko shuleni hapa? Ebo!

Na "sehumu" ni neno la lugha gani? Ki-Yo Yo?

Safari ijayo hakikisha unapomkosoa mwenzako kuhusu lugha, ya kwako iko sahihi.....

ndipo hapo penye utata na penye chanzo cha kulumbana kwa mambo ya kurekebishaka kwa kuwa "ignored"
 
Mtowa maoni haelewi hasa chimbuo la kiswahili pia hakuwahi kubahatika na kuelezwa kuwa hicho kiswahili anachokiongelea hakikuwa kinaongelea na kila sehemu hapa Tanzania mara ya julias kuwa Rais ndio alilazimisha hata wale waliokuwa hawaongei kiswahili wafanye hivyo.

Pili ni kweli kiswahili kimetokana na maneno mengi ya kiarab ukiongelea kibatu sijuwi wangapi nchi hii wanaongelea hicho kibantu jengine kumekuwa na mbinu za makusudi kukiharibu kiswahili kisingizio eti kina lingana na kiarabu ndio leo utakuta kunapandikizwa maneno ya makabila ili kuondowa yale yanoyofanana na kiarabu
 
Shule = Geman w skuli = English w ZANZIBAR wanatumia neno skuli wanarifaa kwa neno la kiengereza school wakati mainland wantumia neno shule wanarifaa neno la kijarumani lenye maana skuli mjarumani alifanya makosa kutowafundisha koloni lake lugha yake
 
Bwana Steven, asante kwa hoja lako kilio chako kinaeleweka lakini kwangu haieleweki ni kwa nini unalia. Kwa bahati mbaya huelezi mifano yako ni maneno gani ya Kihaya yanayofaa kutaja kitu kisicho na jina la Kiswahili tayari na watu wanapendelea kutumia neno la Kiarabu.

Kwa jumla mabadiliko siku hizi ni zaidi kuingiza maneno ya Kiingereza katika Kiswahili na hivyo ndivyo inavyoonekana katika mchango wako. Maneno ya Kiarabu yalikuwemo katika Kiswahili tangu mwanzo na hii ni sababu ya kwamba Kiswahili kimekuwa lugha ya pekee tofauti na Kigiriama au Kizaramo.

Ila tu ukiangalia historia ya lugha huwezi kuona upanuzi wa Kiarabu hata kidogo. Utaona ya kwamba asilimia ya msamiati wa Kiarabu imepungua badala yake siasa ya lugha baada ya uhuru imeunda maneno mapya yenye asili ya Kibantu halafu Kiingereza kimeingia kwa mbio; ukitazama Kiswahili cha Kongo ni Kifaransa pia.

Sijui labda biashara ya muziki yaani nyimbi zinazorekodiwa Dar es Salaam hasa imesababisha lahaja za pwani kusikika zaidi kuliko zamani? Au ni vyombo yva habari, runinga n.k. vya kisasa (tena kutoka Dar hasa) vimeleta matamshi ya pwani kwa watu ambao hawakuzoea bado?
 
Wajerumani walimkuta Chief Rumanyika anaongea Kiswahili fasaha mika ileee ya 1800....na huyu alikuwa ni Mhaya.

Kiswahili kilikuwa kimeshaenea kuanzia Zanzibar hadi Congo na alichofanya Mwalimu ni kukiendeleza kwa manufaa ya Taifa.

Hakuna upendeleo wa Kiswahili kuelekea kwenye Kiarabu kama mtoa mada anavyodhani bali maneno ya lugha yoyote huwa yanaingia bila hata kujua.Maingiano hayo ndiko kukua kwa lugha husika. Mtoa mada anadhani Wasukuma hawajui Kiswahili...hilo ni kosa kwani Wasukuma wa kileo ni wazungumzaji wa Kiswahili fasaha ingawa hawalainishi matamshi yao.

Ukitaka kujua ufahamu wa lugha ya Kiswahili wewe msikilize Ngeleja au hata Dr. Msekela utaona raha ya lugha.Hata Danhi Makanga ingawa anatamka kwa nguvu lakini ufasaha wa lugha haumpigi chenga.
 
Mtowa maoni haelewe hasa chimbuo la kiswahili pia hakuwahi kubahatika na kuelezwa kuwa hicho kiswahili anachokiongelea hakikuwa kinaongelea na kila sehemu hapa TANZANIA mara ya julias kuwa Rais ndio alilazimisha hata wale waliokuwa hawaongei kiswahili wafanye hivyo pili ni kweli kiswahili kimetokana na maneno mengi ya kiarab ukiongelea kibatu sijuwi wangapi nchi hii wanaongelea hicho kibantu jengine kumekuwa na mbinu za makusudi kukiharibu kiswahili kisingizio eti kina lingana na kiarabu ndio leo utakuta kunapandikizwa maneno ya makabila ili kuondowa yale yanoyofanana na kiarabu


Mimi nawaunga mkono wanaojitahidi kurekebisha makosa ya uandishi. Uzembe au kutojali si busara hata kidogo. Nadhani wapo wengineo wanaokumbwa na vikwazo, pengine vilivyo nje ya uwezo wao hata wafanye makosa mengi kwenye aya moja.
Nimejiuliza, hivi mtu anayechapa kwenye keyboard kwa kudonoa-donoa akitumia vidole viwili tu, atakuwa na hamu ya kurekebisha spellings baada tu ya kumaliza kuandika?

Niwakumbushe kuwa hili ni jukwaa la lugha.
Ninyi mnaokosea kila mara kwenye uandishi wenu humu jamvini, hebu jiteteeni kama mnazo sababu!



.
 
Mtowa maoni haelewe hasa chimbuo la kiswahili pia hakuwahi kubahatika na kuelezwa kuwa hicho kiswahili anachokiongelea hakikuwa kinaongelea na kila sehemu hapa TANZANIA mara ya julias kuwa Rais ndio alilazimisha hata wale waliokuwa hawaongei kiswahili wafanye hivyo pili ni kweli kiswahili kimetokana na maneno mengi ya kiarab ukiongelea kibatu sijuwi wangapi nchi hii wanaongelea hicho kibantu jengine kumekuwa na mbinu za makusudi kukiharibu kiswahili kisingizio eti kina lingana na kiarabu ndio leo utakuta kunapandikizwa maneno ya makabila ili kuondowa yale yanoyofanana na kiarabu

LazyDog,

Tutofautishe kukosea Kiswahili na kutumia maneno ya lahaja tofauti, katika maneno yote yaliyokuwa underlined hapo makosa ni mawili tu, ambayo nayo yaonekana kuwa kama "makosa ya kichapo" zaidi kuliko makosa ya Kiswahili sawia.Ingawa inawezekana muandishi si muangalifu.

Kama umezoea kuongea Kiswahili cha Mrima/ Dar-es-salaam, ukazoea kusema "kaloa maji" lahaja nyingine za Kiswahili zinaweza kusema "kalowa maji"

Wengine watasema "hapo" wengine "papo" n.k

Kwa hiyo mtowa ni sawa kama vile mtoa ilivyo sawa, lahaja tofauti tu.
 
Kiswahili ni lugha ngangari ya Kibantu. Ndio maana pamoja na kuwa na maneno kedekede ya Kiarabu, Kiingereza na Kireno bado Kiswahili si Kreoli wala si Pijini. Hata 100% ya maneno yake yakiwa ni ya kigeni bado mnyumbuliko wa sentensi zake utabaki kuwa wa Kibantu tu. Hebu angalia tofauti hii mathalani tukiamua kuazima/kuchukua neno 'dead' kutoka kwenye Kiingereza:

He died - Amededi
He is dying - Anadedi
He will die - Atadedi

Hii ndio lugha iliyokataa kata kata kutawaliwa. Imekataa Ukoloni. Imebaki kuwa lugha ya Kibantu japo Wakoloni hawakuwa Wabantu. Ndio lugha ya mapambano hii. Na ukombozi. Kidumu Kiswahili.
 
  • haelewe
  • kuondowa
  • sijuwi



Huyo huyo aliyeandika ukimwambia asome kwa sauti atajing'ata ulimi. Unaposema "ni sawa" una maana ya kusema "ni sahihi" au sio? Sahihi kivipi? Kwamba ni kiswahili fasaha?

Sio mbaya, nasubiri visingizio toka kwa wengine!
 
Ni kweli kabisa Kiswahili kimeazima maneno mengi zaidi kutoka katika lugha ya Kiarabu kuliko lugha nyingine yoyote. Hayo ni matokeo ya kihistoria.

Waarabu ndio waliokuwa wageni wetu wa kwanza kabisa kutoka nje ya Bara la Afrika. Wao ndio tuliofanya nao biashara tangu wakati huo hadi hii leo. Wao ndio waliokuza miji yetu mikubwa ya mwanzo kabisa. Pangani, Sadani, Bagamoyo, Kilwa na Mikindani.

Katika wageni Waarabu walikuwa wepesi kuoa, kuolewa, kuzaa nasi na kuselelea nchini mwetu, kuliko wageni wengine wetu. Katika kuwasiliana kibiashara na kiukazi ndipo Kiswahili kiliweza kukua na kujitosheleza kawa kuazima maneno mengi katika lugha hiyo ya wageni wetu hao.

Wareno hawakukaa sana Tanzania, hali kadhalika na Wajerumani. Wahindi nao walikuja baadae kidogo hasa wakati wa ujenzi wa reli ya kati. Hata hivyo Kiswahili kimeweza kuazima baadhi ya maneno yao machache. Wangereza ndio Wakoloni wetu wa mwisho. Tazama jinsi tunavyosema na kuandika Ki-Swanglish.

Lugha zote duniani zinazokua na kustawi huazima maneno kutoka lugha zingine. Hilo haliepukiki. Kiingereza kimeinamia sana maneno kutoka lugha ya Kilatini kama Kiswahili kutoka lugha ya kiarabu.
 
tutaendeleaje kujadili mada wakati tabia inayopingwa ni ya kilimbukeni na anaepinga anajua, anakubali, kwamba yeye ni mfano wa kitabuni wa saratani ya ulimbukeni?

Tutakuwa wanafiki kenyekenye.

Anza upya!



mtumzima huzima hauwashi ukawaka!
ushuhuda nasikia lugha imeegemea, tangu zama za vilembwe ukweli utasikia hautapita usemi usitaje arabia ushuhuda nasikia lugha imeegemea.
 
Kiswahili ni mchanganyiko ea lugha za Kibantu na Kiarabu kwa zaidi kwa sababu asili yake ilikuwa ni lugha ya biashara kati ya watu wa pwani na bara.

Lugha zingine nazo zimechangia kwa kiasi chake, kama kireno ni meza, mvinyo, kijerumani ni shule, kengele, hela n.k. Hata hivyo maneno ya kiarabu ni mengi kama yale ya kibantu. Je unajua kuwa maneno haya pia ni kiarabu: asali, jirani, harusi? Tujivunie lugha yetu na historia yake vilevile.
 
Chimbuko ni watu walio katika balaza la kiswahili. Wengi wao ni wazee wa pwani wenye background za kiarabu na hawana elimu ya fasihi wala utaalamu wa lugha yoyoye ya kimataifa.

Kuanzia miaka ya 70/80 ( said nyoka, khalid bali diwani, mohamed mbarouk nk.)

baraza linatakiwa kuwa na mchanganyiko wa watu waliobobea katika lugha za kimataifa na historia ya tanzania.

La sivyo robo tatu ya maneno ya kiswahili yatatoholewa uarabuni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom