KISUTU: Mahakama upande wa Watoto yatupilia mbali shtaka la Hamisa Mobetto dhidi ya Diamond kuhusu malezi ya mtoto wao

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
268,282
1,096,070
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Leo Novemba 10, 2017 inatarajia kutoa uamuzi dhidi ya kesi ya matunzo ya mtoto iliyofunguliwa na mwanamitindo Hamisa Mobeto dhidi ya msanii maarufu nchini, Nassib Abdul au Diamond Platinum.

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka upande wa Watoto. Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote husika kutokana na.msanii Diamond kuwasilisha pingamizi kupinga kesi hiyo kwa madai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi.

Mwezi uliopita, Mwanamitindo Hamisa alifungua kesi hiyo mahakamani hapo akiiomba mambo mbalimbali likiwemo la matunzo ya mtoto waliozaa na msanii huyo. Katika kesi hiyo, Hamisa alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys ambapo anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi.

Kupitia hati hiyo ya madai, mwanamitindo huyo anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake. Hata hivyo, Diamond aliwasilisha hati ya majibu kinzani akipinga maombi hayo ya Diamond akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi sh. milioni tano kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu

============================
UPDATES

Mwanamitindo Hamisa Mobeto amekwaa kisiki mbele ya Diamond Platnumz baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto kutupilia mbali kesi aliyofunguliwa mwanamuziki huyo juu ya matunzo ya mtoto Prince Abdul.

Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Novemba 10 ,2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika.
Diamond aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto akidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi. Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.

Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine anaiomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond.

Mobeto anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi na alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys. Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.

Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ya Sh 5 milioni kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.


Chanzo; Mwananchi
 
Back
Top Bottom