Kisheria, serikali ya kijiji inaweza kugawa chini ya ekari 50, Mpina alitoa rushwa akagawiwa ekari 1000?

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,009
20,684
Kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya Kijiji, (The Village Land Act, Cap 114) na kanuni zake, serikali ya Kijiji hairuhusiwi kugawa ardhi ambayo inazidi ekari 50.

Mpina amegawiwa ekari 1000, kubwa zaidi mara 20 kuliko Ile ambayo Kijiji wanaruhusiwa.
Ni wazi kwamba Mpina alihonga viongozi wa serikali ya Kijiji ili apate ardhi hiyo. Alitoa rushwa.

Wizara ya Ardhi badala ya kuunda taskforce kumfuatilia huyu mtoa rushwa na kufuta umiliki wake, abaki na ekari 49.

Alitetewa na jiwe wakati hii inaibuka, akaizima, akajua imeisha, mali ya umma ukiiba, umma hautakuacha.

Sasa hivi analima mpaka karibu na milango ya nyumba, mpaka watoto hawana sehemu ya kucheza, Kijiji hakina hata eneo la kujenga shule Wala dispensary,lote kachukua Mpina.
 
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,Dada yangu Nsemwa,awe makini anaposhughulikia suala hilo.Asije akatumika vibaya na wakubwa halafu baadaye akashangaa yeye ndiyo anakuwa "toilet paper"
 
Hivi unataka kusema kwamba ni mpina tu ndiyo ana ekari zaidi ya 50 kwenye vijiji? Mpina anawapiga kwenye mishono ndiyo maana wanamuundia zengwe.
 
Hivi unataka kusema kwamba ni mpina tu ndiyo ana hekari zaidi ya 50 kwenye vijiji? Mpina anawapiga kwenye mishono ndiyo maana wanamuundia zengwe.
Mbona mtoto mmoja wa kiongozi wa aliyekuwa mkuu wa nchi ana ardhi sawa na wilaya nzima hasemwi wakati anaiuzia mpaka serikali kila inapotaka kuanzisha miradi maeneo fulani? Serikali iliuziwa na nani eneo la Kwala ambako bandari ya nchi kavu imeanzishwa? Serikali iliuziwa na nani eneo ilipoweka kituo cha kupotezea umeme kutoka bwawa la Nyerere hapo Chalinze?
 
Haya hao viongozi wa kiZanzibari waliojitwalia maeneo makubwa huko Kilosa wamepata kwa ridhaa ya wananchi au unajizima data kichwani?
Nyie maccm mtakuja kusababisha machafuko makubwa sana nchi hii subirini wananchi wafikie kiwango cha mwisho kwenye uvumilivu hapo mtajua kwamba hamjui na tabia yenu wizi kuanzia mkubwa hadi mdogo
 
Hivi unataka kusema kwamba ni mpina tu ndiyo ana hekari zaidi ya 50 kwenye vijiji? Mpina anawapiga kwenye mishono ndiyo maana wanamuundia zengwe.
Wakati wako watu wana miliki ekari hizo na watu wa kawaida tu

Ova
 
Ukiwa msema kweli ccm watakuundia zengwe, kukuua , au kukuloga. Alinukuliwa akisema balozi mtiifu.
 
Mbona mtoto mmoja wa kiongozi wa aliyekuwa mkuu wa nchi ana ardhi sawa na wilaya nzima hasemwi wakati anaiuzia mpaka serikali kila inapotaka kuanzisha miradi maeneo fulani? Serikali iliuziwa na nani eneo la Kwala ambako bandari ya nchi kavu imeanzishwa? Serikali iliuziwa na nani eneo ilipoweka kituo cha kupotezea umeme kutoka bwawa la Nyerere hapo Chalinze?

Ndiyo nimeshangaa kwa mpina kusakamwa kisa ekari 1000 wakati "Prince Moko" anamiliki ardhi kama yote.
 
Ndiyo nimeshangaa kwa mpina kusakamwa kisa ekari 1000 wakati "Prince Moko" anamiliki ardhi kama yote.
Vijiji kama Soga alinununua karibu maeneo yote baada ya kunusa kwamba serikali ilikuwa na mpango wa kujenga SGR kwenye fidia akatia yeye mfukoni. Migogoro iliyozuka juzi huko mabwepande, mbopo, malolo na nyakasangwa, morogoro karibu na msitu wa hifadhi inasemekana yeye ndio 'draft king of the chess'
 
Mpina ni FISADI ila amejifcha kwenye kundi la Legasi ya Mwendazake
 
Wakati wako watu wana miliki ekari hizo na watu wa kawaida tu

Ova

Sure tena wengi sana wanamiliki maeneo hayo ,kuna kipindi maeneo ya kisarawe walikuwa wauza wanakijiji ekari 50 ,watu walikuwa wananunua ekari 300 tena kwa bei rahisi sana....sasa nashangaa wanamzonga mpina kwa ekari 1000 kisa anawapiga kwenye MISHONO.

Mwingira Eftaha ana ekari 500 sehemu tofauti tofauti kama zote na hajawai ambiwa kitu.
 
Mpina atawasumbua sana manake mmekaza mafuvu

Alinunua na utaratibu upo wa mtu ikiwa atahitaji heka nyingi zaid
 
Sure tena wengi sana wanamiliki maeneo hayo ,kuna kipindi maeneo ya kisarawe walikuwa wauza wanakijiji ekari 50 ,watu walikuwa wananunua ekari 300 tena kwa bei rahisi sana....sasa nashangaa wanamzonga mpina kwa ekari 1000 kisa anawapiga kwenye MISHONO.

Mwingira Eftaha ana ekari 500 sehemu tofauti tofauti kama zote na hajawai ambiwa kitu.
Mkuu huyo Efatha kila ukiona kuna kiwanda maeneo ya Pwani tambua na yeye ana eneo pale njia ya kuelekea Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Kisarawe, Morogoro nk amehodhi maeneo mengi sana ya ardhi lakini hakuna mamlaka inayojitokeza kusema chochote lakini mtu akianza kuanika bayana maovu ya serikali wanaanza kumsakama mtu kwa maslahi binafsi sio ya nchi.
 
Back
Top Bottom