Kisa cha marafiki wawili, madikkteta wakubwa wa Afrika

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,721
10,220
Tarehe 8 Januari 1989 serikali ya Uganda ilitoa wito kwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kumpeleka Idd Amin nchini Uganda ili kujibu mashtaka yanayomkabili ikiwemo uvunjifu wa haki za binadamu. Lakini serikali ya nchi ya DRC wakati ule ikiitwa Zaire ilikataa kutii wito huo.
1704302321098.jpg

Pichani anaonekana Mobutu Seseseko rais wa Zaire akiwa na Dada Idd Amin, aliyekuwa rais wa Uganda kabla ya kupinduliwa mwaka 1979 na kukimbilia uhamishoni nchini Saudi Arabia. Aliishi huko Saudi Arabia hadi mwaka 1989 ambapo kwa kutumia passport bandia alirudi Afrika na kufikia nchini Zaire siku ya tarehe 3 Januari. Ile kufika tu, maaskari wakamkamata na kufungwa kifungo cha ndani 'house arrest'.

Watu wakaanza kumshangaa Rais Mobutu Seseseko kwa kumhifadhi Iddi Amin nchini mwake, naye akaona isiwe tabu, akaamua kumfuzia nchini Senegali.

Maafisa wa serikali ya Zaire walisema kwamba uwepo wa Idd Amin pale Zaire ungeweza kuharibu mahusiano na nchi zingine hususani Uganda, hivyo walimuondosha hapo ili arudi zake huko Saudi Arabia alipokuwa akiishi.

Lakini alipokuwa Senegal, Iddi Amin alizuiwa kusafiri na ndege ya Saudi Arabia kutokana na kutokidhi vibali. Hivyo ilibidi arudishwe tena Kinshasa.

Wakati yupo Kinshasa, Serikali ya Uganda ilitoa wito kwa Zaire, kukata Iddi Amin arudishwe nchini Uganda kukabiliana na mashtaka yanayomkabili. Waziri wa mambo ya nje wakati huo Tarcis Kabwegyere aliongea kwamba kuna wajumbe wametumwa kwenda Zaire kuzungumzia mustakabali wa Iddi Amini kutaka arejeshwe Uganda.

Mobutu aligoma 'kumtoa sadaka' Idd Amin akishinikiza kwamba nchi hizo hazikuwa na makubaliano au mkataba wa kubadilishana wahalifu 'extradition treaty'.

Baadae kidogo, tuliona maafisa wa Saudi Arabia wakisema kwamba Idd Amin alikiuka taratibu za kuishi pale SaudiArabia kama mkimbizi wa kisiasa". Kumbe baada ya mkwaruzano na serikali ya Saudi Arabia, ndipo akaamua kuja Kongo Zaire. Hivyo Saudi Arabia hawakutaka Idd Amin arudi tena nchini humo ingawa baadae alirejea Saudi Arabia baada ya mfalme wa Moroko, Hassan II kufanya mazungumzo na serikali ya Saudi Arabia.

Alirejea huko Jiddah Saudi Arabia siku ya tarehe 19 Jan 1989 na kuishi huko hadi alipofariko mwaka 2003.
_________

Ahsante.

©KichwaKikuu.
 
Back
Top Bottom