Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,239
- 113,613
Dunia nzima sasa ni kama imesima kwa sababu ya hofu ya kirusi cha Corona.
Watu hawaendi makazini. Shule zimefungwa. Michezo imesitishwa. Matamasha hakuna. Mikusanyiko marufuku. Madukani kuna uhaba wa baadhi ya bidhaa hadi watu wanatwangana ngumi wakigombea makaratasi ya chooni.
Eti yote hayo ni kwa sababu watu wanakiogopa hicho kirusi cha Corona.
Mimi kirusi cha Corona sikiogopi. Kama malaria haikuwahi kuniua, kama kipindupindu nilikistahimili, nini Corona bana?
Kwa nilichokiona, kirusi pekee kinachotisha sasa hivi ni kirusi cha uoga/ hofu.
Uoga/ hofu hii ndo inayofanya maisha yasimame. Ndo inayofanya watu wanunue na kuhodhi makaratasi ya chooni kupelekea hadi kurushiana ngumi.
Hofu hii imewatoa kabisa akili watu. Watu hawafikiri kabisa kwa kutumia akili. Wanatenda kwa kufuata hofu.
Hofu isiyo na akili [irrational fear] ndiye kirusi wa kuogopwa kushinda hata ukoma.
Mshinde huyo kirusi wa uoga/hofu.