Nimetumia akili yangu nimefahamu Mungu hayupo, ni hadithi tu.
Kwa sababu ana contradictions nyingi sana.
Unaambiwa eti Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.Ana haki ya juu kabisa.
Halafu unaambiwa eti kahukumu wanyama katika gharika, wamekufa sana kwa mafuriko, kwa makosa waliyoyafanya watu.
Sasa Mungu gani wa haki anahukumu wanyama kwa makosa ya watu?
Tunaambiwa Mungu ni wa haki, lakini anahukumu vitukuu na vitukuu vya vitukuu kwa makosa ambayo hata havijafanya, yamefanywa na wazee wao zamani sana huko.
Sasa huyu Mungu wa haki kwa nini anahukumu vitukuu hivi kwa makosa ambayo havijafanya? Mungu anashindwa kwa haki na hakimu ambaye sheria inamkataza kumhukumu mtoto kwa kosa la baba?
Tunaambiwa eti Mungu anapata hasira. Hasira ni udhaifu ambao unaonesha kukosa control, kukosa kujua mambo vizuri, kupata matokeo ambayo hukutegemea, ni udhaifu. Sasa huyu Mungu aliyekamilika kila kitu hasira anaanzaje kuipata?
Tunaambiwa Mungu anapanga mpango, halafu unaenda tofauti na alivyotaka, anataka kughairi.
Sasa huyu Mungu anayejua kila kitu inakuwaje hakujua mpango huu utaenda hivi, mpaka anataka kughairi?
Tunaambiwa Mungu ana taifa lake teule, sasa Mungu mwenye upendo wote inakuwaje atoe upendeleo kwa taifa lake teule?
Tunaambiwa kuna watu Mungu atawaziba mioyo, masikio na macho, hata wajitahidi vipi kumjua hawatamjua, hao msihangaike nao. Sasa inakuwaje Mungu awazibe masikio, macho na mioyo watu wasimjue? Na hawa nao atawahukumu kwa kutomjua?Au atawasamehe tu kwa sababu ni yeye mwenyewe aliwaziba mioyo, masikio na macho na hivyo anajua wasingeweza kumjua?
Tunaambiwa Mungu yeye ndiye anatoa neema ya kumjua, sasa wale ambao hajawapa neema ya kumjua atawahukumu kwa kutomjua au atawachia tu kwa sababu ni yeye mwenyewe hakuamua kuwapa neema ya kumjua?
Tunaambiwa mti ambao hauzai matunda utakatwa na kuchomwa moto kama adhabu ya kutotoa matunda, sasa Mungu mbona anauhukumu mti kwa sababu haujazaa matunda, wakati yeye ndiye anatoa rehema ya kuzaa matunda?
Contradictions allover the place.
Ukichunguza unaona huyu Mungu katungwa na watu tu, ndiyo maana kapewa tabia za watu.