Iko hivi
Kwanza wale wasio waamini katika Mungu mmoja wamekwepa sana sana kujibu hili swali kwakuwa wanajitambua wazi kuwa wanazo akili lakini kimbembe ni kuthibitisha! Na kamwe hawawezi kukwambia hawana akili... Hivyo hivyo ni sawa na uwepo wa Mungu! Yupo lakini huwezi kumthibitisha kimwili kama usivyoweza kuthibitisha akili ulizonazo japo zipo
Dunia ina pande mbili giza na nuru, juu na chini, kushoto na kulia VINAVYOONEKANA na VISIVYOONEKA...
Tunahisi, njaa kiu ama hamu ya kitu lakini hatuwezi kuvionyesha vikaonekana... Ila vinatulizwa na vitu VINAVYOONEKANA yaani chakula, maji nk
Kama tunakubali kuwa kila kitu duniani kina pande mbili basi tutakuwa wajinga tukibisha kama kuna upande wa pili wa dunia usioonekana na huu ndio ulimwengu wa roho, ulimwengu wa Kimungu usio na ithibati za kisayansi lakini upo