Kiranga sio atheist ni non-believer

Huwa nakariri mara kwa mara ya kuwa wewe hutumii akili na mifano yako huwa unakurupuka,mpaka unawaza kuhusu samaki na silika yake kisha unaleta kama mfano ni udhaifu mkubwa kwa kutokujua kuweka kitu mahala pake. Samaki yale ni maisha yake na huwezi kuukosoa mfumo wake. Lakini wewe ni dhaifu sana katika kujenga hoja na kutumia akili,ndio nakufundosha sasa.

Hapa nazungumza na wewe. Mfano wa samaki hapa si mahala pale.

Nakufundisha wewe ambae umekiri ya kuwa jumjuo Mungu lakini bado una mzungumzia na ujinga wako hauja anza kudhihiri leo bali tangu siku ya kwanza najadiliana na wewe.

Kwani mimi haya sio maisha yangu??

Utanifundisha nini, mimi wewe?

Kunifundisha kwamba jiwe ni kiumbe hai???
 
hivi ikiwa Kama uwepo wa magorofa, uwepo wake ni kwa njia ya binadamu. Na binadamu na ulimwengu uwepo wake umechangiwa kwa nguvu hiyo, je uwepo wa nguvu hiyo umechangiwa na njia ya kitu gani????
Hivi ulivyouliza swali, unafikiri maghorofa uliyotaja na yenyewe yanauliza na kuoji hivyo juu ya aliyeyajenga kama wewe unavyofikiri na kuoji?
 
Nimekuonesha namna ambavyo naweza kujua uongo wa kitu bila hata kujua
Kijana hili hujalionyesha bado,zaidi ya kukukosoa juu ya mifano yako ya kijinga na isiyo na uhalisia uliyo itoa.

Hujaonyesha bado namna gani unaweza kujua uongo wa jambo ambalo hulijui na mifano uliyo itoa yote tunaijua.
 
Kwani mimi haya sio maisha yangu??

Utanifundisha nini, mimi wewe?

Kunifundisha kwamba jiwe ni kiumbe hai???
Nina uwezo wa kukufundisha vingi na hapa nina kufundisha na nitaendelea kukufundisha sababu katika hili tunalo lijadili huna unacho kijua mzee,sikudhulumu bali huu ndio ukweli wenyewe.

Kwahiyo katika somo ninalo kupa ni hiari yako kuchukua na kulifanyia kazi au ukaniachia.
 
Hapana! Kwanini? Kwa sababu kati ya binadamu, yeye akijitokeza bora zaidi, na viumbe vingine na ulimwengu, utaona na utakubali vimeumbwa. Hivyo hivi vitu ni viumbe na hivyo kuna muumba wake, ndio chanzo chao na ndio kikomo chao.
Huyu muumba wa hivi vitu, yeye ndie chanzo cha vitu hivi; kama yeye ndiye chanzo anawezaje kuwa na chanzo cha chanzo chake?
Kwanini chanzo cha chanzo chake kisiwepo??

Yaani kuwepo na mauaji ambayo chanzo chake ni vita halafu kusiwepo chanzo cha vita???
 
Kwanini chanzo cha chanzo chake kisiwepo??

Yaani kuwepo na mauaji ambayo chanzo chake ni vita halafu kusiwepo chanzo cha vita???
Fikiri vizuri utaelewa. Fanya utafiti ili uelewe vizuri vitu.
Swali lako juu ya chanzo cha binadamu, ulimwengu na vitu vingine na mfano uliyoutoa kama kutafuta: kuchunguza au kutafiti ukweli wa mambo hauna maana yoyote. Yaani unamrejelea mwanadamu tu.
"Mauaji chanzo chake ni vita na vita chanzo chake ni binadamu", bado hujaona usivyoweza kuelewa!
 
Ukitazama wewe binadamu uwezo wako wa akili: ufahamu, uelewa, kufanyakazi, mfumo wako, unyoofu wako na ukamilifu wako, utaona na kuelewa unatokana na chanzo chenye akili ya juu sana.

Na pia ukitazama vichaa, uwezo wao wa akili, uelewa, kufanyakazi na mfumo wao usio mnyoofu na upungufu wao, utaona na kuelewa tumetokana na chanzo chenye akili ya chini sana kiasi kwamba kimeshindwa ku fix matatizo hayo ambayo hata watu wanapigana usiku kucha kupambana nayo

Hapo hapo tazama ulimwengu na viumbe vingine, hivi vyote havionekani kuwepo kwa bahati nasibu au mbaya, ni kwa mpangilio, unyoofu na kwa mfumo thabiti na kamilifu.
na vyote vilivyo kinyume na hayo uliyoyataja ni uthibitisho kwamba hakuna mpangilio wenye mfumo thabiti wala nyoofu

Hii ni ajabu ya aina gani? Ni akili gani hii: ni nguvu gani hii iliyofanya hivi vitu kwa usahihi na ukamilifu huu, jinsi hii, akili hii ya juu kabisa, nguvu hii ya ajabu kabisa, ndio tunaiita Mungu.
Kwanini ustaajabishwe na ukamilifu wa vitu vichache kua ni lazima viwe vimefanywa kwa akili kubwa wakati vitu vingi vina kasoro kubwa??? Huoni kasoro hizo zinapinga hiyo dhana ya kusema akili thabiti yenye mpangilio nyooofu????

Nyie ndio mnaosema asante mungu kwa kunusuru watu wawili katika ajali, halafu ajali hiyo unakuta imeua watu 1000. Hao 1000 waliokufa mbona humsemi mungu kua kafanya uhuni??
 
Fikiri vizuri utaelewa. Fanya utafiti ili uelewe vizuri vitu.
Swali lako juu ya chanzo cha binadamu, ulimwengu na vitu vingine na mfano uliyoutoa kama kutafuta: kuchunguza au kutafiti ukweli wa mambo hauna maana yoyote. Yaani unamrejelea mwanadamu tu.
"Mauaji chanzo chake ni vita na vita chanzo chake ni binadamu", bado hujaona usivyoweza kuelewa!

Na ndio maana nimekuuliza kivipi chanzo kisiwe na chanzo

Kama chanzo cha vita ni mauaji, basi chanzo cha mauaji ni watu. Sasa ukisema chanzo cha chanzo hakina chanzo utajikuta umesema mauaji hayana chanzo, kwasababu ni chanzo cha chanzo kingine (watu)

Mtu pia ni chanzo cha vyanzo vingi, sasa unaposema chanzo cha chanzo hakina chanzo unajikuta umesema mtu hana chanzo kwasababu yeye ni chanzo cha vyanzo vingine
 
Kwanini ustaajabishwe na ukamilifu wa vitu vichache kua ni lazima viwe vimefanywa kwa akili kubwa wakati vitu vingi vina kasoro kubwa??? Huoni kasoro hizo zinapinga hiyo dhana ya kusema akili thabiti yenye mpangilio nyooofu????

Nyie ndio mnaosema asante mungu kwa kunusuru watu wawili katika ajali, halafu ajali hiyo unakuta imeua watu 1000. Hao 1000 waliokufa mbona humsemi mungu kua kafanya uhuni??
Unachoshindwa kuelewa na kwasababu hiyo unachanganya makosa au uharibifu wa mwanadamu kwake yeye mwenyewe, kwa wengine na kwa dunia na kuyafanya au kuufanya kuwa wa Mungu.
Fanya utafiti na utaelewa kila kitu.
 
Nina uwezo wa kukufundisha vingi na hapa nina kufundisha na nitaendelea kukufundisha sababu katika hili tunalo lijadili huna unacho kijua mzee,sikudhulumu bali huu ndio ukweli wenyewe.

Kwahiyo katika somo ninalo kupa ni hiari yako kuchukua na kulifanyia kazi au ukaniachia.

Unauwezo wa kupayuka, hilo ni koo lako na domo lako siwezi kukupangia, ila siwezi kukizingatia unachokipayuka

Unauwezo wa kunifundisha ujinga ndio nakubali lakini huna uwezo wa kunifanya nikubaliane na huo ujinga

Kunifundisha ujinga na kukubali kufundishika huo ujinga ni vitu viwili tofauti

Naweza nikakuangalia wewe ukajua nakusikiliza wakati mimi naona lips zina cheza tu ila kinachoongelewa hakisikiki
 
chanzo kisiwe na chanzo

Kama chanzo cha vita ni mauaji, basi chanzo cha mauaji ni watu. Sasa ukisema chanzo cha chanzo hakina chanzo utajikuta umesema mauaji hayana chanzo, kwasababu ni chanzo cha chanzo kingine (watu)

Mtu pia ni chanzo cha vyanzo vingi, sasa unaposema chanzo cha chanzo hakina chanzo unajikuta umesema mtu hana chanzo kwasababu yeye ni chanzo cha vyanzo vingine
Ni kweli binadamu ni chanzo cha vitu vingi. Mfano, kama tulivyotoa hapo awali; magorofa.
Sasa, fikiri gorofa ambalo limejengwa na mwanadamu na lenyewe lina hoji hivi juu ya aliyelijenga?
Naomba mawazo yako hapo.
 
Unauwezo wa kupayuka, hilo ni koo lako na domo lako siwezi kukupangia, ila siwezi kukizingatia unachokipayuka

Unauwezo wa kunifundisha ujinga ndio nakubali lakini huna uwezo wa kunifanya nikubaliane na huo ujinga

Kunifundisha ujinga na kukubali kufundishika huo ujinga ni vitu viwili tofauti

Naweza nikakuangalia wewe ukajua nakusikiliza wakati mimi naona lips zina cheza tu ila kinachoongelewa hakisikiki
Poa.

Hili pia limeisha au kuna la ziada ?
 
Unachoshindwa kuelewa na kwasababu hiyo unachanganya makosa au uharibifu wa mwanadamu kwake yeye mwenyewe, kwa wengine na kwa dunia na kuyafanya au kuufanya kuwa wa Mungu.
Fanya utafiti na utaelewa kila kitu.
MaTsunami yanatokana na makosa ya binadamu???
 
Ni kweli binadamu ni chanzo cha vitu vingi. Mfano, kama tulivyotoa hapo awali; magorofa.
Sasa, fikiri gorofa ambalo limejengwa na mwanadamu na lenyewe lina hoji hivi juu ya aliyelijenga?
Naomba mawazo yako hapo.

Kisicho hai hakiwezi kuhoji

Lakini hata kwa kuto kuhoji huko hakumaanishi kwamba hakina chanzo na aliyeumba hilo ghorofa hana chanzo
 
Back
Top Bottom