Unatambua vema kwamba, licha ya mwanadamu kufanya au kuumba magari, majumba na kadhalika, lakini hivi vyote vina chanzo chake ikiwemo na mwanadamu mwenyewe.
Kama binadamu kuumba magari, majumba na kadhalika lakini hivi vyote vina chanzo chake ikiwemo binadamu mwenyewe
Kwa principle hiyo hiyo
Basi licha ya mungu kuumba binadamu na ulimwengu kiujumla vitu hivi vyote ni lazima viwe na chanzo ikiwemo na mungu mwenyewe. Utakubali??
Hapa kwa hakika unaelewa vitu hivi vyote: ulimwengu na binadamu chanzo chake ni kimoja.
sawa lakini chanzo hicho kivipi kiwe ni mungu???
Mashaka yako ni, vipi vitu hivi viwe na chanzo, lakini chanzo kisiwe na chanzo?
mashaka zaidi ni kivipi kila kilichopo kisiwe na chanzo??
Chanzo ndio uwepo wenyewe
uwepo wa nini??
Ni nguvu ambayo imevifanya vitu hivi vyote: vinavyoonekana na visivyoonekana, pasipo kutumia kitu chochote (utupu) vikapata kuwepo.
umejuaje kwamba nguvu hiyo ipo?? Hiyo nguvu ilitoka wapi??? Na kivipi nguvu hiyo iwe mungu na sio kingine tofauti??? Wapi makazi yake kabla ya kusababisha viwepo vingine??? Kabla ya nguvu hiyo kufanya vingine viwepo hali ilikuweje kabla nguvu hiyo haijafanya kazi???
Hivi vitu kwa sababu vinatokana na nguvu fulani vina uwamo wa nguvu hiyo ndani yake.
naweza nikakubaliana nawewe kua ni nguvu
fulani ambayo haijulikani vizuri lakini haimaanishi nayo haina chanzo au nguvu hiyo ni lazima iwe mungu
Ulimwengu na binadamu, uwepo wake ni, kwa njia ya nguvu hiyo.
Ni hivi ikiwa Kama uwepo wa magorofa, uwepo wake ni kwa njia ya binadamu. Na binadamu na ulimwengu uwepo wake umechangiwa kwa nguvu hiyo, je uwepo wa nguvu hiyo umechangiwa na njia ya kitu gani????
Hivyo ukimtazama, ukimchunguza: kumtafiti mwanadamu, unagundua anampangilio, mnyoofu na amefumika kiasi ambacho kuaribika kwa mfumo mmoja ndani yake huwa na madhara kwa mfumo mwingine.
hapana
Usitumie experience unayoiona kua ni bora kwasababu hujaona kinyume chake
Umejuaje kwamba mtu ana mpangilio mnyoofu?? Ikiwa kama tungezaliwa na race ya bluu ungepata wapi wazo la kusema kua binadamu angezaliwa kwa mpangilio tofauti na huu angekuwa bora zaidi???
Mpangilio mnyoofu uko wapi wakati watoto wanazaliwa na upungufu wa viungo??
Jinsi hii ya binadamu inakuwa ya kipekee ukilinganisha na viumbe wengine.
Vilevile utaona viumbe vingine vikiwa kamilifu, nyoofu na kwa mfumo uliyo wa ajabu.
Na vilevile utaona voumbe vikiwa havina ukamilifu wala unyoofu kwa mfumo unaopinga dhana ya unyoofu, kuonesha kua havija dzainiwa na kitu kisichokosea
Hivi ndivyo pia ilivyo kwa dunia: mpangilio wake, unyoofu wake, uzuri wake na mfumo wake, ni wa ajabu na wa kustajabisha!
Unajuaje hiki kimenyooka bila kujua kilichopinda???
Masunami pia nao yanakamilisha unyoofu wa dunia mbona hujayataja??
Unyoofu wa dunia uko wapi wakati watu wana suffer kwa matetemeko ya ardi ya sunani???
Hii yote "ya ulimwengu, binadamu, na viumbe vingine" jinsi yake, namna yake na ndani yake kila kimoja kinavyofanya kazi inatupa kufahamu kwamba, "NGUVU HII" Iliyovifanya Hivi Vitu ni, HAI, KAMILIFU na UPENDO, ni Mungu.
Kwanini nguvu hiyo iwe mungu???
Huwezi ukakuta ghorofa mahali bila hata kujua nani amelijenga unaanza kwa kusema kua haiwrzekani likawa limejijenga, basi kwasababu hiyo litakua limejengwa na mohhammed builders lmtd
Kivipi ghorofa hilo liwe limejengwa na mohamed builder na sio kampuni lingine???