Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Hapana hizi ni tamaduni tu kulingana na jiografia ya kidunia hasa kwenye mila na desturi... Hivi ni vitu vyepesi mno kwenye ulimwengu wa roho kwahiyo hatuwezi kuvitumia kama mfano
Na ndiomaana nasisitiza kua kwenye ulimwengu wenu wa roho wewe na wenzako inawezekana kabisa mkawa na maneno kama hayo kulingana na muktadha wenu.

Sasa mimi ambaye siujui huo ulimwengu wa kiroho ukaniletea maneno hayo kutoka kwenu lazima nione machenga chenga
 
Wakuu,
hili suala la uthibitisho wa uwepo wa mungu ni suala dogo sana, halihitaji kuchukua hata dakika 3 kulithibitisha. Tatizo sio kukosekana kwa uthibitisho wa mungu, ila tatizo ni njia tunazo tumia kutafuta huo uthibitisho. Kuna njia nyingi sana za kupata uthibitisho, na chaguo la hizo njia linategemea na Subject matter to be proven. Miongon mwa hizo njia ni Logical proof, mathematical proof,empirical proof, histoeical-logical proof, axiomatical proof na zinginezo.

Sasa subject yetu hapa ni kuhusu Mungu, na tatzo linakuja pale ambapo tunachagua logic ama empirical proof kutafuta uthibitisho bila ya kujua kwamba kwa kufanya hivyo tumekiuka taratibu za kiudadisi kwa sababu tumechagua njia zisizoendana na subject yetu na hivyo si ajabu tukakosa kupata uthibitisho ulio sahihi.

Kuna watu ( hasa Kiranga ) wanaamin kuwa logical, empirical & mathematical proof ndio njia sahihi na bora Zaidi kuliko zingine, na kutokana na iman hiyo potofu wanaamini kuwa uthibitisho wowote usiotokana na logical, etc basi ushahidi huo unakuwa batili.

Huu mjadala hauwezi kuisha na uthibitisho hautaweza kupatikana kwasababu ya njia mlizo chagua, mmeiacha axiomaticcal proof ambayo ndio njia bora kabisa kwa hii dhana tunayojadili.

Na hata hivyo napenda kuwaambia kuwa "kukosekana kwa uthibitisho wa dhana haimanishi kuwa eti hiyo dhana haipo"

"silence isn't a proof of absence "

Kunavitu vingi binadamu hatuvifahamu, lakini Hatuwez kusema kwamba hivyo vitu havipo.

Kama umeshindwa kupata uthibitisho wa dhana flan, basi usihitimishe kwamba hicho kitu hakipo, inachotakiwa ni wewe kuangalia mapungufu yako katika njia ulizotumia kudadisi dhana husika.

Kama Kiranga na wenzako hamjapata uthibitisho wa Mungu, msihitimishe kuwa Mungu hayupo.
Unaweza kuandika kwa kutumia alphabet bila kutumia logic?

Unaelewa ukishasema tusitumie logic kuthibitisha uwepo wa Mungu, mpaka hapo ushatumia logic kusema tusitumie logic?

Sina uthibitisho kwamba wewe ni Mungu, hilo linathibitisha wewe ni Mungu?

Utajuaje Mungu yupo, hatuna uthibitisho tu, na si kwamba hatuna uthibitisho Mungu yupo kwa sababu hayupo?
 
Nimetangulia kukuwekea link mbili kwanza.. Lakini hizo nafsi 3 ni
Nafsi mwili
Nafsi roho
Nafsi jina (utambulisho)
Mwili unapoungana na roho ndio hupatikana wewe
roho inakaa wapi kwenye mwili
 
Ukiwa unakurupuka hata unachokiandika unakuwa huelewi,nazungumzia jambo ambalo hulijui. Umbile la kawaida la binadamu linakulikana mzee na damu rangi yake inajulikana.
kama aliyekurupuka anakua hakielewi hata anachokiandika halafu kukatokea mtu mwingine akawa anajibizana na maandishi ya huyo aliyekurupuka basi mtu huyo anakua amekurupuka maradufu zaidi ya yule wa mwanzo.

Umbile la kwaida la mtu ni lipi, umelijuaje wewe?? Watu wezaliwa hawana miguu na pia wapo watu wamezaliwa wanamiguu, sasa yupi wa kawaida na yupi asiye wakawaida??? Kwanini kuwe na wakawaida na kuwe na waio wakawaida???

Huyo Asiyewakawaida sio binadamu??

Haya yote yanajulikana,naongelea jambo na dhati yake,sasa unaposema kuhusu baba angu kwa dhati ya binadamu umbile linajuliakana.
linajulikanaje?

Rudi kwa Mola ambae humjui kwa lolote wala huna marejeo yake,ngoja nikusaidie hapa naona umevamia hoja ndio maana unashindwa kuitetea mifano unayoitoa dhati yake inajulikana.

Wewe mbona hujarudi kwa invisible unicorn ambaye humjui???

Tukiza kichwa,usiwe unakurupuka hapa utahangaika bure.
Unayeandika "tukiza" badala ya "tuliza" ndiye unayepaswa kutuliza kichwa
 
kama aliyekurupuka anakua hakielewi hata anachokiandika halafu kukatokea mtu mwingine akawa anajibizana na maandishi ya huyo aliyekurupuka basi mtu huyo anakua amekurupuka maradufu zaidi ya yule wa mwanzo.
Mimi sibishani na wewe,,bali nakufundhisha namna ya kujenga hoja na kutumia akili vizuri.

Kwahiyo kama unahisi nabishana na wewe,unaidanganya nafsi yako.

Tuendelee ....
Umbile la kwaida la mtu ni lipi, umelijuaje wewe?? Watu wezaliwa hawana miguu na pia wapo watu wamezaliwa wanamiguu, sasa yupi wa kawaida na yupi asiye wakawaida??? Kwanini kuwe na wakawaida na kuwe na waio wakawaida???

Huyo Asiyewakawaida sio binadamu??
Ndio maana nikasema hivi,mimi sibishani na wewe na unauliza maswali ya kitoto ambayo hata mtoto mwenyewe ni mara chache sana kuuliza maswali haya.

Umbile la kawaida la mwanadamu ni kuwa na mikono miwili,macho mawili,kichwa kimoja,vidole vitano na vingine ndio maana akitokea mwenye viungo kinyume na umbile hili la kawaida huwa ni habari na pia huitwa kilema,sababu si kawaida.

Ukawaida ndio marejeo ili kujua lipi sawa na lipi si sawa.

Anabaki kuwa binadamu ila anakuwa si wa kawaida. Mola aliumba maumbile ili yawe ni marejeo kwetu sisi. Ndio maana leo hii kuna usiku na mchana ili uwe ni marejeo ya muda kwetu sisi na kukia idadi ya miaka na kuzijua nyakati. Haya yote ni maumbile.
 
linajulikanaje?
Kawaida mwanadamu ana kichwa kimoja,miguu miwili,macho mawili,mikono miwili. Kwahiyo kinyume chake si kawaida ndio maana hata wewe kwa kulijua hil hukutaka kutaka ushahidi sababu si kawaida mwanadamu akawa na vichwa saba.

Huelewi wapi bwamdogo ?
 
Wewe mbona hujarudi kwa invisible unicorn ambaye humjui???

Hili tamko kwangu ni jipya "Invisible Unicorn" ndio nani kwanza ? Kabla sijakujibu.

Wewe ni lazima urudi huku sababu ndio tunae mzungumzia na ulikiri huko nyuma kwamba humjui na huko ndipo kumetufikisha hapa.

Tuendelee.....
 
Kawaida mwanadamu ana kichwa kimoja,miguu miwili,macho mawili,mikono miwili. Kwahiyo kinyume chake si kawaida ndio maana hata wewe kwa kulijua hil hukutaka kutaka ushahidi sababu si kawaida mwanadamu akawa na vichwa saba.

Huelewi wapi bwamdogo ?
Mtu anaweza kuzaliwa kinyume na hapo au haiwezekani??

Kwaiyo kama si kawaida ikitokea mtu kazaliwa kinyume na hapo anakua sio mtu???
 
Unayeandika "tukiza" badala ya "tuliza" ndiye unayepaswa kutuliza kichwa
Nacheka sana,hili ni kosa tu la kiuandishi ambalo hata wewe unaweza kulifanya bali zaidi ya hili,kwahiyo lisikushughulishe.

Hapo nilikusudia "Tuliza" ila weww makosa yako ni makubwa wala si ya kimaandishi bali ya ujinga wa kutokujua huku ukijiaona unajua,mwisho unaonekana kituko.

Nipo .....
 
Mtu anaweza kuzaliwa kinyume na hapo au haiwezekani??

Kwaiyo kama si kawaida ikitokea mtu kazaliwa kinyume na hapo anakua sio mtu???
Hili nimeshalijibu ya kuwa anakuwa ni binadamu ila sio wa kawaida unarudia maswali ambayo nimeyajibi tayari.

Binadamu hazai kopo wala hazai nyani mzee,ungekuwa na akili timamu usinge uliza swali hili la kijinga na kitoto.
 
Na ndiomaana nasisitiza kua kwenye ulimwengu wenu wa roho wewe na wenzako inawezekana kabisa mkawa na maneno kama hayo kulingana na muktadha wenu.

Sasa mimi ambaye siujui huo ulimwengu wa kiroho ukaniletea maneno hayo kutoka kwenu lazima nione machenga chenga
Unayo roho ama huna ama hujui?
 
Unayo roho ama huna ama hujui?
Roho sijui ni kitu gani, pengine umetumia neno ambalo kwa muktadha wenu linaeleweka vyema.

Umaweza kuhusisha na kitu gani kama mfano ili nikuelewe vizuri??
 
Hili nimeshalijibu ya kuwa anakuwa ni binadamu ila sio wa kawaida unarudia maswali ambayo nimeyajibi tayari.

Binadamu hazai kopo wala hazai nyani mzee,ungekuwa na akili timamu usinge uliza swali hili la kijinga na kitoto.

Kama inawezekana, huoni kwamba kupitia mgongo huo unaweza kutengeneza uongo kua kitu kipo wakati hakipo na mimi nikakupinga kua hakipo bila hata kujua ukweli kua kipo???
 
Nacheka sana,hili ni kosa tu la kiuandishi ambalo hata wewe unaweza kulifanya bali zaidi ya hili,kwahiyo lisikushughulishe.

Hapo nilikusudia "Tuliza" ila weww makosa yako ni makubwa wala si ya kimaandishi bali ya ujinga wa kutokujua huku ukijiaona unajua,mwisho unaonekana kituko.

Nipo .....

Cheka tu

Ungetuliza hicho kichwa usingefanya hilo kosa
 
Hili tamko kwangu ni jipya "Invisible Unicorn" ndio nani kwanza ? Kabla sijakujibu.

Wewe ni lazima urudi huku sababu ndio tunae mzungumzia na ulikiri huko nyuma kwamba humjui na huko ndipo kumetufikisha hapa.

Tuendelee.....
Farasi asiyeonekana mwenye pembe moja ni mungu pia
 
Roho sijui ni kitu gani, pengine umetumia neno ambalo kwa muktadha wenu linaeleweka vyema.

Umaweza kuhusisha na kitu gani kama mfano ili nikuelewe vizuri??
Kwahiyo hii ni mara yako ya kwanza kulisikia hili neno na ni geni kabisa masikioni mwako? You must be kidding dude.. If not joking.... [emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]
 
Mimi sibishani na wewe,,bali nakufundhisha namna ya kujenga hoja na kutumia akili vizuri.
Umezaliwa maisha yako yote umemkuta samaki anaogelea, unaanzaje kuanza kumfundisha namna ya kuogelea???

Kwahiyo kama unahisi nabishana na wewe,unaidanganya nafsi yako.

Tuendelee ....

hatuwezi kuendelea kama hujafafanua nafsi ninini

Ndio maana nikasema hivi,mimi sibishani na wewe na unauliza maswali ya kitoto ambayo hata mtoto mwenyewe ni mara chache sana kuuliza maswali haya.
Umavyosema maswali ya kitoto bila kuyajibu unadhihirisha kua we ni mtoto usiyejua chochote na ndio maana umeyakwepa

Umbile la kawaida la mwanadamu ni kuwa na mikono miwili,macho mawili,kichwa kimoja,vidole vitano na vingine ndio maana akitokea mwenye viungo kinyume na umbile hili la kawaida huwa ni habari na pia huitwa kilema,sababu si kawaida.
Sasa ikitokea mimi nimekuambia kua si wakawaida nina vichwa saba na miguu nane vidole viwili na pua tatu utakubali???
Ukawaida ndio marejeo ili kujua lipi sawa na lipi si sawa.
kwani kila kisichokawaida nilazima iwe umewahi kukiona?? Naweza kutumia uvungu huo kuweka uongo wangu kwakujua kua haiwezekani ukajua watu wote wenye kasoro waliopo duniani, itakubali uongo huo kua ni kweli kwasababu haujui kinyume chake???

Anabaki kuwa binadamu ila anakuwa si wa kawaida. Mola aliumba maumbile ili yawe ni marejeo kwetu sisi. Ndio maana leo hii kuna usiku na mchana ili uwe ni marejeo ya muda kwetu sisi na kukia idadi ya miaka na kuzijua nyakati. Haya yote ni maumbile.

Kama anabaki kua binadamu, basi pointi ya kusema baba yako anasifa za ubinadamu usio wakawaida kua anavichwa vinne na miguu tisa inatakiwa ikubalike kwasababu binadamu wasio wa kawaida wapo sindio???
 
Back
Top Bottom