Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

"...Biblia kuna maneno ambayo si Mungu...",
Hii kauli haina maana mpaka uifafanue,je ".... ambayo si Mungu" au ".....ambayo si ya Mungu" ? Kama si ya Mungu au Mungu kwanini yapo kwenye Biblia ? Huo utukufu unatoka wapi.
Nikakujibu hivi: hicho kinachoonekana kwenye biblia kama kuna maneno ambayo si ya Mungu, ni maarifa ya binadamu katika kuelewa maneno ya Mungu kwenye biblia.
Japo kuwa wewe ni kigeu geu,ili kuokoa muda nimeamua kujibu kuhoji sasa kulingana na kauli ya sasa.

Unakubali kwenye Biblia kuna matini inayo jipinga na matini nyingine ?

Je nani alisema Yesu ni Mungu ? Ni Yesu mwenyewe au wanao dai ni wafuasi wake?
 
Mkuu, axiomaticcal proof inatupatia jibu la uwepo wa Mungu. Na Kama utakubaliana na hiyo proof basi utamjua Mungu kiundan Zaidi,

nakushaur uachane na fikra za kuamin kwamba eti logic inajibu kila kitu, ukiamin hivo utakuwa unadhalilisha taaluma ya udadisi, hauwezi kulazimisha usafiri wa barabara ukutoe dunian kukupeleka mwezini.


Leta hapa tuuone
Unaenda benki kukopa halafu unasema wewe unanyumba ya kuweka dhamana hivyo wakupe mkopo bila kuonesha hati miliki halafu unashangaa kwanini unakataliwa?
 
Hakuna kinyume chake hapo. Jambo lolote ambalo hulijui huwezi kujua kama ni uongo,mpaka uwe unalijua au unalifahamu au una ishara,zaidi ya hapo ni kuidanganya nafsi yako.
Ishara kama zipi? Na utajuaje kua ishara hizo zimelenga kitu hicho??

Hapa nakuuliza swali,unajuaje jambo fulani ni la uongo ukiwa hulijui jambo hilo ?
Kwa kujipinga

naweza kujua uongo kua umedanganya kama utasema baba yako ambunyike ni raisi wa tanzania hata kama simjui baba yako ambunyike. Umeelewa?


Swali zuri,njia za kuhakiki kuhusu ukweli wa jambo fulani hutakiwa kufata baada ya jambo hilo,na njia zenyewe huwa ni kuhoji na si kukanusha.
Si lazima kuhoji ndipo utajua uongo wa kitu

Ukiniambia wewe umeishi miaka 3000, nitajua tu ni uongo sina haja ya kuhoji kivipi uliishi miaka hiyo

Unapokiri ya kuwa hujui,basi huna haki ya kuliznugnumzia jambo hilo zaidi ya wewe kuonyesha kutaka kujua au kukaa kimya. Huu ndio utaratibu wa kielimu.
Kukiri kua sijui haimaanishi nikipewa jibu la uongo sitalijua, kwaiyo wewe utakubali kila uongo uliovikwa sura ya ukweli kwasababu hujui kitu kitu hicho???
 
Mkuu, axiomaticcal proof inatupatia jibu la uwepo wa Mungu. Na Kama utakubaliana na hiyo proof basi utamjua Mungu kiundan Zaidi,

nakushaur uachane na fikra za kuamin kwamba eti logic inajibu kila kitu, ukiamin hivo utakuwa unadhalilisha taaluma ya udadisi, hauwezi kulazimisha usafiri wa barabara ukutoe dunian kukupeleka mwezini.
Hapo uthibitisho uko wapi???
 
Ishu kubwa hapa ni chanzo cha kitu na sio maarifa ya hicho kitu

Binadamu kuumba nyumba, magari nk hiyo inamaanisha kua kila kilichopo kina chanzo, hatuwezi kusema majumba, magari nk vilivyoumbwa na mtu vina chanzo lakini huyu aliyeviumba (mtu) hana chanzo. Alikadhalika huwezi kusema binadamu na vilivyomo vina chanzo halafu msababishi wa hivyo hana chanzo
Unatambua vema kwamba, licha ya mwanadamu kufanya au kuumba magari, majumba na kadhalika, lakini hivi vyote vina chanzo chake ikiwemo na mwanadamu mwenyewe. Hapa kwa hakika unaelewa vitu hivi vyote: ulimwengu na binadamu chanzo chake ni kimoja.
Mashaka yako ni, vipi vitu hivi viwe na chanzo, lakini chanzo kisiwe na chanzo?
Chanzo ndio uwepo wenyewe. Ni nguvu ambayo imevifanya vitu hivi vyote: vinavyoonekana na visivyoonekana, pasipo kutumia kitu chochote (utupu) vikapata kuwepo.
Hivi vitu kwa sababu vinatokana na nguvu fulani vina uwamo wa nguvu hiyo ndani yake.
Ulimwengu na binadamu, uwepo wake ni, kwa njia ya nguvu hiyo.
Hivyo ukimtazama, ukimchunguza: kumtafiti mwanadamu, unagundua anampangilio, mnyoofu na amefumika kiasi ambacho kuaribika kwa mfumo mmoja ndani yake huwa na madhara kwa mfumo mwingine.
Jinsi hii ya binadamu inakuwa ya kipekee ukilinganisha na viumbe wengine.
Vilevile utaona viumbe vingine vikiwa kamilifu, nyoofu na kwa mfumo uliyo wa ajabu. Hivi ndivyo pia ilivyo kwa dunia: mpangilio wake, unyoofu wake, uzuri wake na mfumo wake, ni wa ajabu na wa kustajabisha!
Hii yote "ya ulimwengu, binadamu, na viumbe vingine" jinsi yake, namna yake na ndani yake kila kimoja kinavyofanya kazi inatupa kufahamu kwamba, "NGUVU HII" Iliyovifanya Hivi Vitu ni, HAI, KAMILIFU na UPENDO, ni Mungu.
 
Hakika hawa watu siyo tu kwamba wametengana na akili zao, lakini pia miili yao hawaijui.
Ukiwachunguza hawa watu wa jamii hii utagundua wamejeruhiwa.
Halafu hasira zao wanazimalizia kwenye nguvu inayowashikilia, kuwaongoza na kuwapa ukomo
 
Kwa kujipinga

naweza kujua uongo kua umedanganya kama utasema baba yako ambunyike ni raisi wa tanzania hata kama simjui baba yako ambunyike. Umeelewa?
Kaka uwe unafikiria basi aisee,kwani wewe humjui raisi wa Tanzania ni nani ?

Sasa unachi pinga kitu gani ? Uwe unafikiria hata kwa bahati mbaya.

Ungekuwa unatafakari kiundani usingetoa mfano wa kitoto wa sampuli hii,jambo liko wazi ya kuwa raisi wa Tanzania ni Magufuli kwahiyo yeyote atakae kuja na kudai yeye ni raisi wa Tanzania lazima atakuwa ni Muongo sababu tunamjua raisi wa Tanzania.

Sasa chukulia jambo hulijui kabisa,vipi unaweza kujua kama ni la uongo ?

Pili,kuhusu kujipinga kwa jambo huwa kuna sababu kadha wa kadha.
 
Ishu kubwa hapa ni chanzo cha kitu na sio maarifa ya hicho kitu

Binadamu kuumba nyumba, magari nk hiyo inamaanisha kua kila kilichopo kina chanzo, hatuwezi kusema majumba, magari nk vilivyoumbwa na mtu vina chanzo lakini huyu aliyeviumba (mtu) hana chanzo. Alikadhalika huwezi kusema binadamu na vilivyomo vina chanzo halafu msababishi wa hivyo hana chanzo

Sijui kama umeelewa
Ni kuunda sio kuumba
 
Kaka uwe unafikiria basi aisee,kwani wewe humjui raisi wa Tanzania ni nani ?

Sasa unachi pinga kitu gani ? Uwe unafikiria hata kwa bahati mbaya.

Ungekuwa unatafakari kiundani usingetoa mfano wa kitoto wa sampuli hii,jambo liko wazi ya kuwa raisi wa Tanzania ni Magufuli kwahiyo yeyote atakae kuja na kudai yeye ni raisi wa Tanzania lazima atakuwa ni Muongo sababu tunamjua raisi wa Tanzania.

Sasa chukulia jambo hulijui kabisa,vipi unaweza kujua kama ni la uongo ?

Pili,kuhusu kujipinga kwa jambo huwa kuna sababu kadha wa kadha.

Raisi wa tz namfahamu lakini babako simfahamu hivyo nimekuoneshea kua naweza nikapinga uongo huo hata kama simfahamu

Sio tu hivyo

Naweza hata nisimjue baba yako lakini ukiniambia anavichwa saba na miguu nane na anadamu yakijani nitakataa. Sitahitaji kuhoji kujua ushahidi wa vipimo vya kisayansi wala picha

Naweza nisimjue babako lakini haimaanishi kwamba ukiniambia alisha wahi kufa na akafufuka nikubali. Niatakataa bila hata kumjua kiundani baba yako

Ukiniambia wewe umezaliwa mwaka 1970 halafu baba yako mzazi kazaliwa 1992 nitajua huu ni uongo ilihali sijui umri sahihi kati yako na baba yako

Umeelewa???
 
Umeelewa maana ya '...Imeandikwa ndani ya moyo wako...'?
Hakuna mtu alie amua kuiita hivyo. Nguvu hii: Mungu, iko ndani mwako.
Wewe kama huijui au huisikii, hilo sio kosa la Mungu, bali ni lako.
haya maelezo umeyatoa wapi
 
Ni kuunda sio kuumba
Kivyovyote vile haimaanishi kilicho undwa/umbwa kiwe na chanzo halafu kilicho unda/umba kisiwe na chanzo

Yaani gorofa lililo undwa/umbwa liwe na mjenzi, halafu huyo mjenzi asiwe na chanzo????
 
Wakuu,
hili suala la uthibitisho wa uwepo wa mungu ni suala dogo sana, halihitaji kuchukua hata dakika 3 kulithibitisha. Tatizo sio kukosekana kwa uthibitisho wa mungu, ila tatizo ni njia tunazo tumia kutafuta huo uthibitisho. Kuna njia nyingi sana za kupata uthibitisho, na chaguo la hizo njia linategemea na Subject matter to be proven. Miongon mwa hizo njia ni Logical proof, mathematical proof,empirical proof, histoeical-logical proof, axiomatical proof na zinginezo.

Sasa subject yetu hapa ni kuhusu Mungu, na tatzo linakuja pale ambapo tunachagua logic ama empirical proof kutafuta uthibitisho bila ya kujua kwamba kwa kufanya hivyo tumekiuka taratibu za kiudadisi kwa sababu tumechagua njia zisizoendana na subject yetu na hivyo si ajabu tukakosa kupata uthibitisho ulio sahihi.

Kuna watu ( hasa Kiranga ) wanaamin kuwa logical, empirical & mathematical proof ndio njia sahihi na bora Zaidi kuliko zingine, na kutokana na iman hiyo potofu wanaamini kuwa uthibitisho wowote usiotokana na logical, etc basi ushahidi huo unakuwa batili.

Huu mjadala hauwezi kuisha na uthibitisho hautaweza kupatikana kwasababu ya njia mlizo chagua, mmeiacha axiomaticcal proof ambayo ndio njia bora kabisa kwa hii dhana tunayojadili.


Na hata hivyo napenda kuwaambia kuwa "kukosekana kwa uthibitisho wa dhana haimanishi kuwa eti hiyo dhana haipo"

"silence isn't a proof of absence "

Kunavitu vingi binadamu hatuvifahamu, lakini Hatuwez kusema kwamba hivyo vitu havipo.

Kama umeshindwa kupata uthibitisho wa dhana flan, basi usihitimishe kwamba hicho kitu hakipo, inachotakiwa ni wewe kuangalia mapungufu yako katika njia ulizotumia kudadisi dhana husika.

Kama Kiranga na wenzako hamjapata uthibitisho wa Mungu, msihitimishe kuwa Mungu hayupo.
Sahihi kabisa lakini pía ni ngumu kutafuta ithibati ya kimwili kwa kitu cha kiroho... Ni makosa makubwa kufanya hivyo kwakuwa ni vitu viwili tofauti kabisa lakini vyenye kuunganishwa pamoja kutengeneza kimoja
Ni kati ya hivyo viwili kimoja kinaonekana na kingine hakionekani... Kimoja kina ukomo na kingine hakina ukomo...
 
Unawezaje kutunga kitu ambacho kipo ndani yako? Mungu yuko ndani yako, vipi iwezekana kutungwa!
Fikiri jambo dogo kama hili 'Akili', je, ni jambo la kutungwa?
ndani yangu kwenye utumbu,ubongo au ?? akili ipo kwenye ubongo
 
Back
Top Bottom