Nilicho kigundua kwenye uzi huu mnaogopa kujibu hoja za kiranga sasa kwa style hii ndugu kiranga atazidi kila siku kuwashinda kwenye midahalo ya hapa jf
Mimi na kiranga hatutofautiani sana kwenye suala la kuwepo au kutokuwepo kwa mungu.
Niliachana na habari za mungu miaka kumi iliyopita, nikiwa na miaka 16 tu.
Kuna maswali mpk leo nimeshindwa kujibiwa, nikaona ni habari za kipuuzi.
Mshana tunatofautiana sana humu kwa habari zake za mungu na uchawi, lkn kwenye mjadala huu nimejikita kwenye swali lake la msingi kwa Kiranga. Naona yupo sawa kabisa.
Lkn nimekuta mjadala, nimeona swali sawia kabisa akiulizwa kiranga Je Ana Akili?
Yeye nae hakujibu bali kauliza apewe maana ya akili kwanza kwani anajua tafsiri nyingi.
Sasa anapaswa atupe hizo tafsiri, sisi tuweze kujua kweli swali lilikuwa halieleweki kwake.
Sasa km hawezi kutupa hata tafsiri mbili tujionee kweli anatafsiri zaifi ya moja huko ni kutuchanganya zaidi.
Angesema hajui maana ya akili au ni msamiati mpya kwake, au aelezwe maana yake kwanza ili ajibu hapa tingesema kweli tumsaidie ili aweze kutujibu swali leti kwa ufasaha.
Sasa kusema ana tafsiri nyingi alafu hazisemi ni kutuhadaa.