Hebu elezea vizuri hii,am curious to know mkuu
Kungekuwa na Watanzania wawili kati ya kumi wana utashi kama wako, tungefika mbali.
Nilitarajia swali hili zamani sana.
Sijaliona.
Mpaka sasa najitayarisha kulala nakata tamaa kuna mtu atauliza ndo nakuina unaokoa jahazi.
Ni hivi.
Wewe hapo ulipo. Mwili wako.
Ukuta wa nyumba, ulivyojenhwa.
Nyoye mko 99.99999% empty space.
Tafuta kwenye vitabu vyote vya sayansi vinavyoelewa latest atomic theory na quantum physics.
Sasa kamanwewe ni 99.99999% empty space. Na ukuta nao ni 99.99999% empty space, mtu akijua jinsi ya ku align hiyo 99.99999% yake ya empy space iende sawa na 99.99999% empty space ya ukuta, ili ile 0.000001 yake yenye matter isikutane na ile 0.000001% yenye matter ya ukuta, akapita kwenye ukuta bila mkwaruzo, kwa mujibu wa quantum physics, tutasema huo ni uchawi au quantum physics tu ambayo hatujaijua?
Sisemi kwamba hicho ndicho kilichotokea. La hasha. Sina ushahidi huo.
Naukiza tu.
Kwa nini tuko tayari sana kurukia kukubali uchawi, wakati mambo ambayo tunasema ni ya uchwai hata kwenye sayansi yanaweza kutokea bila mgogoro wowote tu?
Ni sawa na mtu aue kwa sumu 8nayoeleweka vizuri kwa Chemistry, kwamba ukimpulizia mtu hewa hii anakufa, kwa sababu ya chemical rwactions zitakazotokea katika mwili, halafu mtu akitumia sumu ile kuua hivyo hi yo kwa kumpulizia mtu tumuite mchawi.
Huyo atakuwa mchawi kweli au tunampa cheo cha uchawi tu wakati kiukweli pale katumia Chemistry tu?
Sijajibiwa swali hili.