Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 87,744
- 152,619
Mara zote huwa unaniambia sijui tofauti ya hayo maneno na mie huwa sichoki kukuambie unipe maana ya hayo maneno,ila matokeo yake unaingia mitini.
Na leo nakwambie tena eleza tofauti ya hayo maneno ujuzi,kujua na kuamini.
Kila mara natoa huu mfano.
Nikiwa nakuja kwako,sina hakikakama upo kwako,lakini nafikiriutakuweponyumbani, maana kuna mpira leo na wewe hupenda kutulia nyumbani kuangalia mpira, wakati nakuja,sina hakika ya kusema upo kwako, hapo naamini upokwako.
Nakuja kwako, kwakuaminikwamba upo, sina hakika, sijuikama upo kwako au umebanwa kazini.
Hapo naamini.
Nikifika kwako, nikakuona, uko kwako, hapo nimeshajua kwamba upo kwako, siamini tena kwamba upo kwako, najua.
Sasa weweunachanganya mawili hayo. Unataka kutuambia kwamba kuna kitu unakiamini n akukijua kwa wakati mmoja.
Wakati kukua maana yake si kuamini na kuamini si kujua.