Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Mkuu Ndio Maana nilisema ww una Grandisity clinical feature ya mania Hilo ni tatizo hatari
Kwakuwa nimetoa mifano ya akina Tyson? Au kwakuwa nimemuasa Samaritan cha kufanya? Sijamtusi mtu wala kumdhihaki yeyote.. Wala hakuna lugha ya kuudhi niliyotumia hapa.. Angalia mwisho wa siku tatizo lisije ikawa ni wewe na sio maandishi yangu
 
Tatizo mkuu ww unayo elimu nzuri hutaki kuwapa faida wenzako umekaa nayo mwenyewe hiyo inakuwa huitendei haki nilitaka kujifunza mengi kupitia ww lakn unanikatisha hutaki challenge kama sijakosea ktk post yako ya nyuma ukanitoa mkuku ukisema hutaki mjadala sasa hv naona km unadonoa unaondoka unatakiwa utupe elimu ili tukubali nashndwa kukuelewa, Mkuu Samaritan mbn tunaenda vzr?
 
Sizungumzii watu kujiua au kujua kuna nini baada ya kufa bali nazungumzia mtu kujua siku yake ya kufa,hili si jambo dogo hivi unafikiri watu wangekuwa wanajua ni lini wanakufa hali ingekuwaje?

Mara zote hapa mnasema kuwa imani ya Mungu ilianzishwa kipindi cha ujinga watu walikuwa hawajui mambo mengi na ndiyo wakawa wanatoa jibu la Mungu kwa yale mambo wasioyajua.

Hivyo leo hii hakuna sababu ya kendelea kuamini Mungu kwa sababu mambo mengi yanajulikana.
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Nashukuru mkuu. Tunaweza kutofautiana misimamo, itikadi, elimu, imani n.k lakini sitadharau utu wako.

Kumcha Mungu ni chanzo cha hekima.
Kumcha Mungu kunaweza kuwa chanzo cha hekima.

Tatizo wewe umeishia kwenye chanzo cha hekima tu, hujatafuta hekima zaidi.

Hilo neno la "kumcha Mungu ni chanzo cha hekima" nalikubali sana.

Kwa jamii ambazo zilikuwa hazina organization yoyote, hazina elimu yoyote, hazina ujuzi wowote, dhana ya kumcha Mungu iliweza kuwaunganisha watu, wakakaa pamoja, wakapata moral compass, wakaweza kuungana, wakapata serikali za kuwaongoza.

Dhana hiiil ikuwa chanzo cha hekima.

Wakafanya mpaka specializalion, division of labor, industrial revolution.

Wakasoma sana wakaona huyu Mungu ana makosa kibao.

Wameshapita "chanzo cha hekima",wameenda kwenye hekima kubwa zaidi.

Wewe bado unabaki kwenye "kumcha mungu ni chanzo cha hekima" tu!
 
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Siwezi kuthibitisha na wala sipo hapa kuthibitisha. Lakini pia hata kama ningeweza haina maana huo uthibitisho wangu ndiyo ungekuwa umemfanya Mungu awepo na pia kutoweza kwangu kuthibitisha hakuondoe uwepo wa Mungu ikiwa kweli yupo atabaki kuwepo.

Kwa hali hiyo mie nitaendelea kuamini uwepo wa Mungu kutokana na dalili na sababu za msingi,na kwahiyo ninachokiamini kwangu ndiyo ukweli na si kwa sababu ya kutokujua.
 
Huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Huwezi kuondoa contradictions katika dhana ya kuwepo kwake.

Kwasababu hayupo.

Kuamini unaruhusiwa kuamini chochote unachotaka mradi usivunje sheria.

Sizungumzii imani, nazungumzia unachojua, facts, not faith.
 
Inaelekea una taaluma au uwezo ambao mimi sina. Utakua umenipa faida kubwa sana ya kufuatilia huu mjadala endapo utafanikiwa kunipa huo uthibitisho mkuu, karibu.

Mkuu naomba ukitaka kujua hapo kuwa mungu na jeshua kuwa walikuwa wanaongelea kwa macho kuwa jua limesimama Ngoja tucheki andiko hilo kwa lugha ya kiebrania

Jeshua 10:12

Az (ndipo) Ya-ab-ber (akanena) Ya-ho-wo-su-a (Joshua ) Yah-weh (Na Bwana) Ba-yo-wm (katika siku hiyo ambapo) te (aliwatoa) Yah-weh (Bwana) ha-emo-ri (waamori) lip-ne (mbele ya) ba-ne (wana) Yis-ra-el (waisrael) way-yo-mer (akasema) la-e-ne (mbele ya macho yao) Yis-ra-el (israe ) Sha-mesh (wewe jua) ba-i-own (gibeoni) do-wm (simama kimya)
Wa-ya (mwezi) ba-e-meq (ktk bonde) ay-ya-lo-wn (aiyaloni)

Ktk lugha ya kiebrania neno jua ni shamesh kwa kiarabu shams lakn neno kusimama lilitumika hapo juu ni do-wm likiwa limetokana Na neno la kiebrania daw-man likiwa Na Maana stop Au still stand pia kuna neno lingine la kiebrania lenye Maana kusimama heb-amad

Kwa hiyo hapo unaona wazi ni jua lilisimama physical

Andiko hili ndio lilioleta gumzo dunia nzima watu wa zamani walikuwa wanaamini kuwa jua linatembea Ndio maana ktk vita ya jeshua mungu alilisimamisha jua mpaka wa Israel wakashinda vita

Kabla ya karne ya 15 watu walikuwa wanafahamu jua linatembea vile wanavyoliona kwa macho akaja Gallileo akapinga akisema jua halitembei
Kanisa la kipindi hiko RC wakampa hukumu Kwakuwa alikuwa anaonekana anaenda kinyume Na maandiko ya mungu wakamuua kwa ukweli wake mwaka 1992 RC kupitia papa wakatengua hukumu hiyo

Swali je jua lilisimama ktk vita ya jeshua Au mwandishi wa kitabu cha jeshua alivyoona kwa macho jua linatembea nae akadhani linatembea?

Kumbuka mtu yoyote aliyekufa Kabla ya Gallileo kusema nadharia yake kuwa jua lipo limesimama alikufa akijua jua linatembea Na Ndio mwandishi wa kitabu cha jeshoua kafa akijua hilo
 
Siamini kwa sababu naruhusiwa,mbona naruhusiwa kunywa pombe lakini sinywi. Hivyo naamini kwa sababu na dalili za msingi na sio kwa sababu kwamba kuna mtu ameniruhusu kuamini.

Ninachokiamini ndiyo ninachokijua,kama nilivyosema kuwa uthibitisho haufanyi jambo liwepo au lifanyike na pia kutokuwepo uthibitisho hakufanyi jambo lisiwepo au kutofanyika.
Huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Huwezi kuondoa contradictions katika dhana ya kuwepo kwake.

Kwasababu hayupo.

Kuamini unaruhusiwa kuamini chochote unachotaka mradi usivunje sheria.

Sizungumzii imani, nazungumzia unachojua, facts, not faith.
 
Siamini kwa sababu naruhusiwa,mbona naruhusiwa kunywa pombe lakini sinywi. Hivyo naamini kwa sababu na dalili za msingi na sio kwa sababu kwamba kuna mtu ameniruhusu kuamini.

Ninachokiamini ndiyo ninachokijua,kama nilivyosema kuwa uthibitisho haufanyi jambo liwepo au lifanyike na pia kutokuwepo uthibitisho hakufanyi jambo lisiwepo au kutofanyika.
Huwezi kuamini unachojua.

Ukijua kitu kinakuwa si imani tena, ni ujuzi.
 
This is a slap on the face.
Kumcha Mungu kunaweza kuwa chanzo cha hekima.

Tatizo wewe umeishia kwenye chanzo cha hekima tu, hujatafuta hekima zaidi.

Hilo neno la "kumcha Mungu ni chanzo cha hekima" nalikubali sana.

Kwa jamii ambazo zilikuwa hazina organization yoyote, hazina elimu yoyote, hazina ujuzi wowote, dhana ya kumcha Mungu iliwezakuwaunganisha watu, wakakaa pamoja, wakapata moral compass, wakaweza kuungana, wakapata serikali za kuwaongoza.

Dhana hiiilikuwa chanzo cha hekima.

Wakafanya mpaka specializalion, division of labor, industrial revolution.

Wakasoma sana wakaona huyu Mungu ana makosa kibao.

Wameshapita "chanzo cha hekima",wameenda kwenye hekimakubwa zaidi.

Wewe bado unabaki kwenye "kumcha mUngu ni chanzo cha hekima" tu!
 
Huwezi kuamini unachojua.

Ukijua kitu kinakuwa si imani tena, ni ujuzi.
Nimesema navyoamini ndivyo nijuavyo,mfano ninacho kiamini kuhusu chanzo cha Ulimwengu basi hivyo ndivyo nijuavyo kuhusu chanzo cha Ulimwengu.

Sioni haja ya kucheza na maneno ya kujua wala ujuzi.
 
Nimesema navyoamini ndivyo nijuavyo,mfano ninacho kiamini kuhusu chanzo cha Ulimwengu basi hivyo ndivyo nijuavyo kuhusu chanzo cha Ulimwengu.

Sioni haja ya kucheza na maneno ya kujua wala ujuzi.
Nasema hivi, unachoamini, hujakijua bado, ndiyo maana unakiamini.

Ukikijua, hakipo kwenye imani, kipo kwenye ujuzi.

Tatizo hujui tofauti ya kuamini na kujua.
 
Nasema hivi, unachoamini, hujakijua bado, ndiyo maana unakiamini.

Ukikijua, hakipo kwenye imani, kipo kwenye ujuzi.

Tatizo hujui tofauti ya kuamini na kujua.

Hahahaaaa I’ve been telling you these people don’t know diddly about what they are talking about!
 
Hahahaaaa I’ve been telling you these people don’t know diddly about what they are talking about!
I do recall.

It feels like teaching an ant the math in the first half of Sir Roger Penrose's "The Road To Reality: A Complete Guide To The Laws of The Universe".
 
Nasema hivi, unachoamini, hujakijua bado, ndiyo maana unakiamini.

Ukikijua, hakipo kwenye imani, kipo kwenye ujuzi.

Tatizo hujui tofauti ya kuamini na kujua.

Mara zote huwa unaniambia sijui tofauti ya hayo maneno na mie huwa sichoki kukuambie unipe maana ya hayo maneno,ila matokeo yake unaingia mitini.

Na leo nakwambie tena eleza tofauti ya hayo maneno ujuzi,kujua na kuamini.
 
Back
Top Bottom