kipindi cha star tv kuhusu tiba ya babu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kipindi cha star tv kuhusu tiba ya babu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by yeto, Apr 6, 2011.

 1. y

  yeto Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 15
  kuna kipindi kinaendelea sasa hivi star tv kuhusu tiba ya babu, wamekipangilia vizuri wamehoji askofu laizer na wengineo,
  kuna Dr Ambokile shilogile wamemhoji ambaye ni wa klinik ya magonjwa sugu Arusha. amesema wagonjwa wote walioathirika waliokuwa wanafika kwenye clinic hiyo arusha na pia wamepata kikombe na amewafuatilia zaidi ya siku 21 bado wako positive. hivyo anashauri waliopata kikombe wasiache dawa mpaka dr awaambie wmepon kwani bil daktari kuwaambia wanaumwa wasingeenda
   
 2. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Mkuu mbona huo mwanzo tu, daily mie nasema tutasikia mengi tu, at the end viongozi wa makanisa waliomshabikia babu watatafuta jinsi ya kulisafisha kanisa kwa kosa lao la kuchoteka kiurahisi mno na nguvu za giza. Hakika hiyo ni kipimo watu wamepewa kupima imani zao, na kuwapima akili zao jinsi gani wanaweza tofautisha tiba sahihi na tiba za kishirikina. Wasukari tumeambiwa wako wanapukutika na hao wa ngoma hakuna hata mmoja ambaye ni neg, sasa dawa ya babu inatibu ugonjwa gani?
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Acha uongo wewe. Umeona wote waliokuwa na ngoma kuwa hawajapona?

  Mbona mie nimepona kabisa ugonjwa wangu? Na nilikwenda German kupima ili niwe na uhakika.

  Hospital kubwa kabisa pale Mannheim akanihakikisha kabisa baada ya kupimwa mara tatu kuwa niko fresh na sasa hivi mie ni SUKARI ni damudamu.

  Nimerudi zangu sasa hivi Sikonge na nimeamua kuwa Mcha Mungu na napiga zoezi ili kuwa fit.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mimi nadhani tangu hii kadhia ya babu wa loliondo ianze baadhi yetu tulisema si vizuri watu wakaingia kichwa kichwa bila kutafakari kati herb na miracle lakini kwa vile ccm were in a hurry to sway the public from life difficulties to Loliondo, basi ukakuta almost the all republic walikwa wagonjwa watu wakasahau dowans na bei ya mafuta na kutaka kujisalimisha Loliondobila hata kuwa na uhakika wa tiba yenyewe madhali ilikuwa original kutoka kwny mitishamba ( mugariga) tofauti ni zile cheap na feki za India zilizo jaa kwenye pharmacy zetu! Taratibushetani mwnyewe ataanza kuwaumbua kabla Mungu hajaamua kuwapa na fasi ya kutubu!
   
 5. D

  Dopas JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Asante kwa hili Mak, tangu waanze huo ushirikina wao nilikuwa nasema hayo kwenye red italics. Kila siku watu wanakufa, uone ni jinsi gani ushirikina ulivyokita ktk mawazo ya wengi, hata watanzania wakitolewa kafara namna hiyo kila siku baadhi ya viongozi wa dini na serikali wanashangilia.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Halafu huyu anakimbilia kusema ni nguvu za giza. Nguvu za giza ni za akina Sheikh Yahya na wanajimu. Kasisi si mnajimu. Anatumia jina la Mungu kutibu na amewashauri wote wanaokunywa kikombe watoe shukrani kwa Mwenyezi Mungu na wala si shetani wa gizani.
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kuna haya niliyasema kwenye uzi mwingine wenye kufanana na huu:

  ...
  Hao wanao mtetea huyu babu, kila kukicha wana kuja sera na mpya...!

  Watu sasa wanaonekana wakifa wengi tunasikia jinsi wanavyo mtetea...! Oooh babu hazuii kifo, ndio tunajuwa kuwa hakuna mtu mwenye uwezo wa kuzuiya vifo... ndio hata hao mitume tunao waamini kwenye dini zetu, ziwe za jadi au hizi ambazo tuna ziita za kimapokeo, hawakuwa na uwezo wa kuzuiya watu wasife... Lakini kama vifo vinatokana na uzembe na ujinga wa makusudi kwa kuacha kula dawa zenye kukuongezea uhai, mnataka tuwaeleweje?

  Sasa tunasikia tena kuwa watu wasiache kula dawa zao, japokuwa wamepata kunywa dawa za Kinjeketile Ngwale wa karne hii ya ishirini na mbili... Kulikoni tena?

  Hao waliokwisha kunywa dawa mpaka leo hatusikii wakisema kuwa wamekwenda kupima... Wanaogopa kitu gani...!? Utawasikia wakijisifia kuwa wamepona kwa kujiangalia kwenye kioo...! Na hali maradhi yanawatafuna ndani kwa ndani...!

  Mwisho hao watetezi watakuja na utetezi mpya kuwa wale wote ambao hawakupona hawana imani ndio maana dawa ya babu Kinjeketile haikufanyakazi...!

  Hivi hao waathirika waliozidiwa baada ya kuto endelea na dawa zao za mahospitalini, watajisikiaje watakapo simangwa kwa kushutumiwa kuwa hawakupona kwa kuwa hawana imani...! Je hamuoni ni kuwadhidishia maradhi zaidi?

  Hivi anayetakiwa kuwa na imani hapa ni nani mgonjwa au babu kinje...! Yeye si ndiye aliye dai kuwa kaoteshwa na mungu na dawa yake inaponyesha maradhi yote...!? Hivi Mwenyezi Mungu anapoleta Neema huwa anachaguwa wa kumpa? Au huwa anawapa hata wale wasio muamini?

  Hivi ni kweli uwezi kupona mpaka huwe na imani ...!? Inaingia akilini kweli?

  Mbona tunasoma kwenye maandiko ya biblia kuwa kuna watu waliponywa na wala hawakuwa na hiyo imani...! Na wengine walifufuliwa...! Je wale walioponywa na kufufuliwa na Nabii Elisha...! Walikuwa na imani? tena wengine walifufuka kwa kugusa mifupa ya manabii tu.

  Jamani tuwache kushabikia vitu ambavyo haviwezekani kwenye karne hii... karne ambayo mwenyezi Mungu ametujaalia utaalam wa kutengeneza madawa ya kutibu maradhi mbali mbali...! Kinacho wafanya watu wasitumie hiyo miujiza ya kunywa dawa mahospitalini ni kitu gani kama si ulimbukeni na kutafuta njia za mkato ni nini...!? Kwani hizo dawa za mahospitalini hazina baraka za Mwenyezi Mungu!?

  Hivi tunamwambia nini Mwenyezi Mungu siku ya hukumu... Na hali ametupa akili na tunashindwa kuitumia... Hivi ni neema gani zaidi ya kutumia akili zako na kutambua kuwa hapo Lolly hakuna uponyaji zaidi ya kuwapumbaza watu kwa kivuli cha imani!?

  Mara nyingi ni vigumu sana kushindana na wajinga, watakushinda tu...!

  Watakusumbua na hoja zao za kijinga na kukushusha mpaka ufikie level yao...!

  Kisha watajiona kuwa wao ni mahodari na kuanza kujisifia na hali wanaona kuwa ujinga wao umepelekea maangamizi ya ndugu, marafiki na jamaa zao wenyewe...! Ukiwauliza haya mambo yamekuwaje... Hawakosi hoja hata siku moja...! Utawasikia wakisema "Aaah wale, wale wamekosa imani ndio maana hawakupona, unatakiwa umkili bwana kwanza..." Jamani hivi hakuna viongozi wa dini ambao wamefariki kwa maradhi ya kutibika, lakini wakafariki? Je hawakuwa na imani!?

  Msije sema kuwa hatukuwaonya na kuwatahadharisha na hatari iliyoko mbele yenu...! Sisi tunawapenda zaidi ya hao ambao wanao wapeleka kwenye mdomo wa mauti, uko mnakoenda hakuna uponyaji, bali kuna mauwaji...!
   
 8. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,931
  Trophy Points: 280
  Mie najaribu kutafakari serikali yetu hii ambayo ndio imejitwalia jukumu la uwakala wa mitishamba ya babu itajificha wapi. Mawaziri wamekaa, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, viongozi wa kidini wote wametekwa na trick ndogo sana ya babu. Je, si zaidi basi kwa Kibwetere ambaye yeye aliwaahidi kwenda mbinguni wafuasi wake? Au si zaidi sana kwa Mary Sinaida Akatsa ambaye alimleta "Yesu" huko Nairobi na waumini wake wakamwona mchana kweupe? Nakuhakikishia kama Akatsa angelikuwa hapa nchini kwetu, basi serikali yetu ingezunguka duniani kote kutamba ni jinsi gani taifa letu lilivyokubalika na Mungu.
   
 9. Nkamu

  Nkamu JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 206
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ole wao wanyweao kikombe cha shetani hali wakijiita wacha Mungu, kwani hukumu yao iko tayari. Nawaomba ndugu zangu wote mlionywea kikombe cha babu mkatubu haraka maana wakati wa kurudi kwake mwana wa Adamu kumefika.Kwa babu hakuna uponyaji bali ni kupiga watu upofu ili wamsujudie shetani!
   
 10. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  X-Paster et al

  Hivi unapokuwa usingizini huwa unakuwa wapi? {In real terms} Je, unaweza ku-prove kisayansi mahali unapokuwa? Au ni basi tu tunakubali kwamba tupo kitandani tumelala. Je, ni wangapi wanakufa kila siku wakati wanatumia dawa za mahospitalini? Au kwa sababu dawa hizo zimekuwa packed vizuri? Je kuna dawa yoyote ile ambayo ipo hospitalini ambayo haitokani na mmea wowote? Je matibabu mazuri na yanayoponyesha ni lazima yatoke kwa wazungu tu?

  My pick kama dawa za babu zinafanya kazi ataendelea kupata wateja sambamba na hospitalini, lakini kama dawa zake hazifanyi kazi wateja watakoma.
   
 11. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,931
  Trophy Points: 280
  You missed the point. Dawa ya babu ni neno. Dawa ya hospitali ni tangible. Think again. The two can't be compared. Angekuja na kudai kuwa anapiga ramli jamii ingepata sehemu ya kumweka. Lakini amekuja na vague statement kwamba anatoka kwa Mungu ilhali anatenda sawasawa na wapiga ramli. Anatakiwa ama kuwa baridi, ama moto na si vuguvugu. Simple logic.
   
 12. N

  Newvision JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Upo mkanganyiko! ila wako wanaoshuhudia kuwa wamepona magonjwa mbali mbali ikiwapo UKIMWI nadhani tusubiri kama uongo upo utajitenga tu muda si mrefu. Hakuna haja ya sisi kugombana
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hii ishu bado inachanganya, wakati kuna watu wanaripotiwa kufa baada ya kunywa kikombe wapo pia wanaoripotiwa kupona kabisa magonjwa yaliyokuwa yanawasumbua..
   
 14. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #14
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kaka nadhani Nyenyere amekujibu vyema kabisa, ila ilo la usingizini unakuwa wapi, jibu lake ni kuwa unakuwa umelala kimwili na unapokuwa unaona unakuwa kwenye ulimwengu mwingine wa kiroho, ilo halina mjadala, na sina uhakika linaingiaje hapa...!

  Kama utakuwa umenisoma vizuri, utakuwa umekutana na maneno haya kwenye paragrafu ya 10.
  Sasa nakuuliza kwani hizo dawa za hospitalini hazina baraka za kiMungu?

  Ndio maana nikasema kwenye paragrafu nyingine kuwa hakuna mtu mwenye uwezo wa kuzuiya vifo, lakini je kufa kwa uzembe wa kutotumia dawa muwafaka si kujitakia mwenyewe...?

  Watu kufa wanakufa sana tu, wapo wengine kwa kujinyonga au kula sumu, vyote hivyo ni vifo lakini kila kifo kina uzito wake na ndio maana ukitaka kujiuwa na ikatokea watu wakakuokoa utashtakiwa na serikali, na sie ambao tunaamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, kujiuwa kwa makusudi ni dhambi. Je unawashauri vipi wale wote ambao wapo kwenye dose ya HIV na wale wenye kuugua kisukari, ni sawa kuacha kula dawa zao kwa kuwa wamekunywa dawa ya huyu babu kwa kuamini tu kuwa watapona!?
   
Loading...