John Pambalu: Ufafanuzi juu ya kusitishwa kwa kipindi cha agenda, kinachorushwa na kituo cha Star TV

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
JOHN PAMBALU, UFAFANUZI JUU YA KUSITISHWA KWA KIPINDI CHA AGENDA, KINACHORUSHWA NA KITUO CHA STAR TV, AMBAPO JANA KILIKUWA NA MAADA ISEMAYO UCHAMBUZI WA MIAKA 5 YA BUNGE LA 11

Ndugu zangu wapenzi wa demokrasia na Uhuru wa habari, salamu. Kufuatia kukatwa kwa matangazo yaliyokuwa yakirushwa mubashara na kituo cha Star TV kuhusu uchambuzi juu ya miaka 5 ya bunge la 11 (Bunge la Ndugai) nimepokea simu na jumbe nyingi zenye kutaka kujua ni nini kilitokea.

Nimejibu SMS na simu nyingi naomba niandike kwa kifupi nini kilitokea ili ipunguze maswali kwa watanzania wenzangu, ndugu, jamaa na marafiki zangu.

Jana majira ya saa 11 jioni nilipokea simu ya Mtozi Aloyce Nyanda aliyeniomba niwe mgeni katika kipindi chake. Licha ya kwamba nilipewa mwaliko kwa muda mfupi sana lakini kwa mapenzi makubwa kwa nchi yangu nilikubali kuwa mgeni wake. Nikajiandaa nikaenda studio.

Nikatambulishwa kuwa tutakuwa wageni wawili mmoja kutoka Dodoma na mimi nitakuwa studio ya Mwanza.

Mjadala ukaanza nikitoa hoja yangu ya kwanza kwa nini niliona Bunge la 11 halikuwa Bunge bora. Nikaahidi kutoa hoja 5 na hoja ya kwanza ilikuwa ni kuwa Bunge la kumi 11 badala ya kuisimamia serikali, serikali imelisimamia bunge.

Nikatoa mifano 2 wa kwanza ni maelekezo aliyopewa spika ya kuwashughulikia wabunge wa upinzani ndani ya bunge ili washughulikiwe kwa namna nyingine nje ya Bunge. Mfano wa pili nikazungumzia manunuzi yanayofanywa na dola bila kupitishwa ndani ya bunge nk.

Wakati tunaendelea na mjadala. Nikasikia sauti katika microphone ya Nyanda ikumuelekaza aage ili kipindi kifike mwisho, sauti ilikuwa ikisema Nyanda aga, aga.

Tukapigwa na mshangao. Akaingia dada mmoja mfupi mweupe ndani ya studio akamwambia Nyanda aga kwa ishara. Badae akaingia kijana mweusi, mwembamba mrefu kidogo mara matangazo yakakatwa. Wakamwambia Nyanda soma meseji kwenye simu yako.

Tukahoji kwa nini wanakata kipindi zaidi ya dk 40 kabla ya muda wake wa kawaida. Wakadai ni maelekezo, Nyanda akachukua simu yake asiyejua nini cha kufanya nikamuaga na kuachana naye usiku ule.

Niseme nini, sioni sabuba yoyote ya kumlaumu Nyanda kama ninavyoona katika mitandao mingi ya kijamii. Lakini kama taifa tujiulize, "Tumefikaje huku tulikofika?".

Wasalaam,

John Pambalu
Mkt Bavicha taifa.
 
Ndio kisingizio chenu!.

Hata mngeitana wote na M/kiti wenu taifa mngepigwa tu, siku zote ukweli ni sawa na mwanga, giza haliwezi kushinda.
Tukutane kwenye sanduku la kura Jimbo la Nyamagana na huyo Pambalu wenu si anagombea Ubunge Nyamagana, CCM wanamleta Makonda, Pambalu anapigwa mapema saa nne asubuhi
 
Return Of Undertaker,

Mimi nilikuwa Live nafuatilia na niliona upepo ulivokuwa unaenda. Dogo Pambalu upo vizuri ,simama kwenye mstari you have a bright future!

Kuna watu wanaendelea kuishi kiujanja ujanja wanataka na Chama Kokongwe kiishi hivyo. Lakini Sayansi inatuambia kuwaTaasisi /Chama hakiwezi kuishi kiujanja ujanja kwa muda wote!
 
Tukutane kwenye sanduku la kura Jimbo la Nyamagana na huyo Pambalu wenu si anagombea Ubunge Nyamagana, CCM wanamleta Makonda, Pambalu anapigwa mapema saa nne asubuhi
Bashite hawezi kwenda Mwanza wana mafaili yake mengi. Thii Thii eeem oyeee
 
Mbowe huwa anawaweka chambo Vijana wengi wa kanda ya ziwa,alianza na katambi then huyu naye kaingia mzima mzima labda azinduke mapema
Inaelekea umekurupuka usingizini na haujui nini kinazungumziwa, endelea kulala tutakuamsha muda ukifika.
 
Return Of Undertaker,

StarTV ni ya Mwenyekiti wa Chama kwa hiyo hurusha matangazo kufuatana na maagizo toka juu zaidi. Sasa hivi hata ITV, EATV, CapitalTV na BBC Tz zote zinaunga mkono juhudi. Taarifa za kuaminika ni zile za BBC London kwa akina Kikeke tu.
 
Back
Top Bottom