DC Ole Sabaya aunguruma Star TV; atoa ufafanuzi kuhusu kampuni ya Q-net, kumshambulia Diwani Arusha

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Mwandishi Wetu,

Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameibuka na kuzungumzia masuala mbalimbali zikiwemo tuhuma za kumshambulia diwani wa kata ya Sombetini jijini Arusha,Bakari Msangi huku akisisitiza ya kwamba kuna baadhi ya watu wamekuwa wakipika majungu kila uchwao dhidi yake.

“Pale Arusha kuna kandarasi ya majungu, kuna watu kazi yao ni kupika majungu kila siku na Mimi nitashangaa sana siku wakinishangilia nitajiuliza sana “alisema Ole Sabaya

Ole Sabaya ametoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali wakati akihojiwa na mtangazaji wa kipindi cha The Big Agenda, Aloyce Nyanda ndani ya kituo cha Star Tv hivi karibuni.

Akitoa ufafanuzi huo alisema kwamba mara zote akifanya jambo baya au zuri watu husema tu na kusisitiza kwamba viumbe vyenye nguvu ndio hupigwa vita na sio viumbe dhaifu.

“Mimi nikifanya jambo baya au nikifanya jambo zuri watu watasema tu, tena mambo mabaya ndio unafahamika zaidi ndio maana dunia inamjua Osama Bin laden kuliko Papa anafanya mambo mazuri “ alisema Ole Sabaya.

Alisema kwamba taarifa za yeye kumpiga diwani ni uzushi na kupika na zimekuwa zikisambazwa na Ansbert Ngurumo mtu ambaye alimtaja kwamba amekimbilia nje ya nchi na kukubali kulipwa ujira na mabeberu ili aifedheheshe na kuitukana nchi yake.

Ole Sabaya amezungumzia pia suala la kampuni ya Q-net aliloliibua hivi karibuni na kuzua gumzo ambapo aliitaja kampuni hiyo kuwa ni ya kilaghai na wala haijasajiliwa Brela.

“Q-net haijasajiliwa Tanzania, Q-net kwa Tanzania ni kampuni ya kilaghai. Qnet haijawahi kutoa returns wala kulipa corporate tax ya asilimia 30 ya faida na hata kwa wakala wa usajili wa biashara na leseni (Brela)haijasajiliwa.

Ole Sabaya alizungumzia kuhusu taarifa za kuzushiwa kifo hivi karibuni na mtu anajiita Kigogo na kufafanua kwamba amewasamehe wote waliomzushia kifo na anawaombea.

Pia Ole Sabaya alizungumzia suala la baadhi ya watu kuchukulia kawaida mambo mbalimbali yanayofanywa na Rais John Magufuli katika nyanja za kimaendeleo huku akisisitiza kuwa saa inakuja watu hao watajua thamani na watakuwa wamechelewa.

“Sasa hivi watu wanachukulia poa kila kitu kinachofanywa na JPM, Ubungo interchange poa, stendi ya Mbezi poa, Sekenke iliyokuwa inaua watu poa, airport ya Mwanza poa, mirabaha ya madini poa lakini saa inakuja watajua thamani yake na watakuwa wamechelewa “akisisitiza Ole Sabaya

Mwisho.

IMG-20210311-WA0009.jpg
 
Tusubiri anaowaweka Mjini aombe Maji halafu hawa watarudi Vijijini kulima
 
Back
Top Bottom