Kipi bora kati ya Meta AI na ChatGPT?

Kipi bora kati ya Meta AI na ChatGPT?

Anachoniboa Meta ni muongo muongo sana alafu namna fulani kama anajiona sana kuna muda unamuuliza kitu anakujoboa .

Ila open Al hana shida yule jamaa yeye kila kitu anafanya vile utakavyo ila nikaja kugundua kuwa hapo utofauti wake ni kuwa open Al ni kijana tena barobaro ila Meta ni lizee tena nahisi la kijijini huko lililpvamia mji maana liongo alafu linaweza kukukanusha mpaka ukajisikia vibaya
 
Mpaka sasa hakuna AI inayofikia ChatGPT, watu wana compare na Deepseek!
Lakin bado Deepseek haijafikia umahiri wa ChatGPT kwa utajiri wa kukusanya taarifa na kiwasilisha.

Analysis inayofanywa na ChatGPT ni yakiwango cha juu sana compared to Deepseek.
 
Mimi natumia chatgpt, sina maelezo mengi ya kuisifia ila kusema tu ni bora kuliko zote.
 
AI nzuri ni ile unayoiuliza chochote na inakujibu sio inakupa limitations na restrictions za kijinga hio sio AI nzuri..
Hata Gpt kwa baadhi ya issue anabana mbupu, hadi ukabane naye ndio anaachia
 
Mpaka sasa hakuna AI inayofikia ChatGPT, watu wana compare na Deepseek!
Lakin bado Deepseek haijafikia umahiri wa ChatGPT kwa utajiri wa kukusanya taarifa na kiwasilisha.

Analysis inayofanywa na ChatGPT ni yakiwango cha juu sana compared to Deepseek.
Umejaribu Gemini 😁
 
Umejaribu Gemini 😁
Hio naitumia kila siku haifikii Open AI yaan GPT.. uzuri Gemini ina vitu vingine extra mfano sauti, picha na video ila kwenye picha inafeli pia mfano ukiiambia ipige screenshot inapiga ila ukiiambia ikwambie kwenye hio picha ya screenshot kuna kitu gani inakwambia kwamba hata yenyewe haijui kwenye hio picha kuna nini, na hapo imepiga screenshot yenyewe hapo nilichoka mimi... unabisha jaribu uone
 
Hivi hapa mnajadiliana nini? JF ya siku hizi bure. Hamna mada za mapenzi tena na zakupelekeana moto.

Max mtu wangu jitafakari.
 
Nikiwa kama muhitimu wa zama hizi za AI naweza sema chatGPT ni baba lao.

1.Deepseek
2.Gemin zamani bald
3.Perplexity huyu nampendea anakupa na michoro
4.Co pilot la Microsoft
5.Grok la bwana elon musk
6.Meta Ai hii sijaitumia sana maana imekuja kutoka mwishon kumaliza chuo.

Na ma AI mengine nimeyasahau ila mwisho wa siku chatGPT ndio alikuwa anakamlisha kazi zangu, uzuri wa chat GPT linatunza kumbukumbu story za mwaka jana linakukumbusha vizuri tu, ukianza kuchati nae mpe taarifa zako za msingi kama majina yako, umri,fani yako na mengineyo utafurahi mbona.

AI ukitaka upate majibu mazuri inabidi na ww muuliza swali uwe umenyooka...

Kwa kumalizia GPA yangu ya 4.1 chatGPT limeshiriki kwa asilimia 50. Vijana tumieni AI vizuri zina manufaa sana sana.
 
Hivi ukiwa una access gpt premium ina maana unakuwa unatofautiana na huyu anaetumia free?
Tofauti ni nini?
1766819401358.png

---
Tofauti:
- FREE version inaweza kukupeleka chaka kwa kukupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Kumbe Majibu ni ya kubuni kama inavyo someka hapa ". I fabricated an analysis to match your claim instead of honestly evaluating the code."

Yaani AI itaendelea kutoa majibu hata kama sio sahihi ilimradi tu. Na ukiipa facts kuwa hapo umekosea inapswa kuwa hivi na hivi. basi hapo kwa hapo itaomba radhi.
 
Usimfananishe Open AI na Meta AI.. Open AI yaan GPT ni next level ingawa inakosea kuna wakati inaweza ikupe majibu yasiyo sahihi.. hilo Meta AI limewekewa limitations na restrictions kuna maswali ukiliuliza linakwambia habari za policy sijui nini upuuzi tu wakati Open AI ukiuliza chochote linakufungukia bila wasiwasi
Huu upuuzi hata kwenye AI Video generator upo wa kuambiwa mambo ya policy,mkuu unaijua AI video generator isiyo na viji-policy?
 
Huu upuuzi hata kwenye AI Video generator upo wa kuambiwa mambo ya policy,mkuu unaijua AI video generator isiyo na viji-policy?
Hizo ni limitations and restrictions tu wameziweka...
 
Mpaka sasa hakuna AI inayofikia ChatGPT, watu wana compare na Deepseek!
Lakin bado Deepseek haijafikia umahiri wa ChatGPT kwa utajiri wa kukusanya taarifa na kiwasilisha.

Analysis inayofanywa na ChatGPT ni yakiwango cha juu sana compared to Deepseek.
Chatgpt ukiilipia ni inajua hadi inakera.
 
Back
Top Bottom