SoC02 Kipaji ni nyota njema ambayo huonekana asubuhi

Stories of Change - 2022 Competition

Godfrey Constantine

New Member
Aug 30, 2022
2
2
MWENYE MASIKIO NA ASIKIE NA MWENYE MACHO NA AONE, NYOTA NJEMA HUONEKANA ASUBUHI.

Njia sahihi ya kukifahamu kipaji cha mtoto,kukiendeleza na kukikuza pamoja na kujua wakati sahihi wa kukitumia ilikuleta manufaa kwa jamii na yeye pia, ni pale hakiwa na umri mdogo. Hivyo tunatakiwa kwanza kujua kipaji ,kipawa ,namna sahihi ya kukikuza, katika njia sahihi na muda sahihi wa majukumu yake na wajibu wake bila kupishana na muda.

Mfano, Fid Q anashuhudia katika wimbo wa “mwanza mwanza “kwamba alizaliwa na kipaji cha kuimba ila alipokuwa mdogo alikuwa akiimbaimba hivyo watu na ndugu zake walimwona kama hivi anamapungufu (hana akili) kumbe ndio kilikuwa kipaji chake lakini sasa hivi ni msanii mkubwa na ndio kinaendesha maisha yake na ni kioo cha jamii katika maandishi yake.

Kipaji na kipawa ambavyo binadamu anavyo vimegawanyika katika sehemu tatu

kwanza ni cha kuzaliwa nacho peke yako ambacho hiki hakihusiani na urithi wa kipaji cha mzazi (wazazi).

Pili ambacho binadamu anakipata kutokana na wazazi wake baba au mama (kurithi) na

Tatu anakipata kutokana na mazingira, changamoto za mazingira alipo umjengea kipaji cha kufanya jambo fulani ambalo ni tafauti na jambo watu walivyokuwa wakifanya awali au kuboresha jambo fulani.

Haya yote yatupasa kufahamu mapema na kubainisha namna ya kumsaidia mtoto ili aweze kukiendeleza na kukikuza kipaji chake.

Yatupasa kufahamu kuwa kila mtu huzaliwa na kipaji na kipawa ambacho kimebeba majukumu (purposes) yake katika maisha.

Tumezaliwa kutatua matatizo yaliyopo kwenye jamii wala sio kuishi nayo na kuboresha suala fulani , hivyo kazi ya kipaji na kipawa nikukuza ufahamu,maarifa,busara,kuboresha,kuvumbua kitu kipya. Mzazi au mlezi yampasa kugundua kipawa au kipaji cha mwanae na kukiendeleza kwa namna yeyote kabla hakijafa.

Tufahamu kipaji na kipawa cha mtoto uhasiriwa na mazingira kwa kiasi kikubwa aidha kwa kukinyenyua au kukikuza. hivyo yatupasa kujenga mazingira ya kukinyenyua na kuviendeleza vipaji mbalimbali vya watoto (shule za vipaji).

Kwani kipaji kinaitaji muda mwafaka wa akili na mwili katika kuzaliwa,kukua na kutekeleza majukumu pale muda unapo fika , watu wengi wamekuwa na vipaji vyao na kushituka ambapo muda wa kukikuza umepita.

Pengine vikiiva pale ambapo mwili hauendani na akili hivyo vipaji vyao kushidwa kutekeleza majukumu mfano nchi nyingi za kiafrika zina maprofesa wenye vipaji ambao wamevijua uzeeni ,sasa umri wao ni mkubwa ambao awawezi kuisaidia jamii yao hii ni kwa sababu wana akili kubwa lakini mwili hauendani na akili zao katika utekelezaji umri mwingi utakuta miaka (45- nakuendelea ndio maprofesa). Kipaji na kipawa kinatakiwa kiive katika umri wa kufanya kazi katika utekerezaji wake, hapo mabadiliko ya jamii yataonekana mfano. kuanzia miaka (6-35)hapo ndio umri wa vijana.

Elimu ya madarasa tulioipokea imejikita kupata watu wenye akili kubwa wakiwa na umri mkubwa , ambapo hawana manufaa makubwa kwa jamii husika. Tunapoteza muda mwingi katika kutafuta elimu ya madarasa na kukosea na kujirekebisha wenyewe kwenye mambo tofauti tofauti ya kipaji bila ya ushauri sahihi nini kifanyike kuhusu vipaji vya watu.

Elimu yetu inatuchelewesha kufahamu kipaji na kipawa vyetu ,muda mwingi tunaupoteza katika upumbavu tuliamini ndio maisha yalivyo , sasa ni tofauti hii ndio maana watu uzeeka katika upumbavu bila kujua wajibu na majukumu yao yalio katika kipaji na kipawa chao.

Taaluma,ujuzi wa maisha , kipaji ni vitu tofauti ndio maana tunaona maprofesa (wasomi) ambao hawana tija kwa jamii kwa sababu wamejazwa taaluma tu. Mtu anaweza kuwa na taaluma kubwa lakini akawa sio msaada kwa jamii husika , kumekuwa na elimu ya kujaza taaluma peke yake katika nchi za kiafrica na kusahau ujuzi wa maisha na vipaji.

Mbali na hapo ni mabigwa kwenye hili kusifiwa kujaza taaluma kwa watoto lakini watoto wengi inapo fika muda wa kufanya majukumu hushidwa kukizi wajibu na majukumu yake na baadae kugundua amekosa ujuzi wa maisha na kipaji kwa suala husika hapa msomi huyo anashidwa kuisaidia jamii yake ipasavyo .

Nyota ni ujuzi wa kuzidi wa mtu ambao utampatia riziki yake na kwa jamii yake .Kipaji ni nyota ya mtu , kutotumikia nyota ni kutofanya wajibu na majukum yako hivyo usababisha kujenga jamii isiyojua majukumu na wajibu wake (wapumbavu) hivyo kuchangia kuongezeka kwa matatizo katika jamii kwani hakuna matatizo yanayotatuliwa.

Kila mtu anazaliwa ilikufanya wajibu na jukumu lake ambalo limebebwa na nyota au kipaji kulingana na wakati wake husika. Hivyo kushidwa kufanya wajibu na jukumu lako kwa wakati, matatizo urundikana kutoka kizazi kwenda kizazi,kutokana na watu wa vizazi vilivyopita kushidwa kuweka mabadiliko kwenye muda wao.

Adui wa yote ni upumbavu,jamii yenye viongozi wenyetamaa na imani ya kishilikina .wapumbavu ni wale hawajui wafanye nini kwa watoto wao ili kunyenyua vipaji na vipawa . Pia wao kwa sababu hawafahamu basi ata watoto wao hawaangaikii vipaji vyao mpaka vinakufa nakupotea kabisa .

Kundi la pili lenyewe usafiria vyota za wenzao kwa kuziua ili kupoteza nafasi zao au ajira zao kwasababu wanajua kitu hicho , hawa wengi ni viongozi wenye tamaa hivyo kuongoza jamii isiyobadilika kwa muda mrefu ili waendelee kwenye nyazifa zao. Na watu wapumbavu inafikia kuamini kuwa wao ndio wanavipaji cha kuongoza au kufanya kazi fulani katika jamii kumbe ndio wauaji wa mifumo ya mabadiliko sahihi ya jamii yao .

Mfano.”Mathayo2:2-20” yesu alipozaliwa mfalme wa kipindi hicho alitambua kuzaliwa kwake na jukumu lake hivyo aliamua kuwa watoto wote wauwawe ndani ya uyahudi ya bathlehemu kwa sababu alijua kuwa huyo mtoto atakuwa mwiba kwake na kwa watawala hii yote nikutokana na tamaa zao. Na watoto wao ndio huwaingiza katika kazi.

Upande mwingine kuua vipaji na vipawa vya jamii huku watoto wao wakiwaandaa kwa siri kushika nafasi au nyazifa mbalimbali .

Hakuna jambo zuri kama kufanya kitu ambacho moyo wote na mwili unaridhia kukifanya .Kitu hicho hapo ndipo kipaji hulalia bali mtu asiyekuwa na kipaji au kipawa hufanya kwa kusukumwa na bila kupenda basi hutoa matunda mabaya. Mtu mwenye kipaji anatakiwa haongozwe na misingi ambayo aitamzuia bali itamtengenezea njia katika kutoa matokeo mazuri.

Nchi zilizoendelea asilimia kubwa ya watu wenye vipaji huvitumia katika umri ambao akili na mwili vina fanya kazi pamoja na kwa ufanisi ndio maana suala la maendeleo lipo juu. Nchi ambazo azijaendelea unakuta mtu anaumri mkubwa ndio huwa mstari wa mbele kuisaidia jamii kumbe alitakiwa kuwa mshaurii na mtoaji wa uelekeo wa jamii sio mtendaji kazi.

Hivyo inatupasa kubadilika na kujua suala zima la kipaji yani kuzaliwa kwake,kukua na muda sahihi wa kutumika.

Imeandaliwa na,GODFREY CONSTANTINE MASANJA,0762460956.
 
Nimepiga kura nikiunga mkono suala LA kujua na kukuza vipaji vya watoto..in muhimu sana..lakini elimu ya darasani in muhimu pia.. Elimu hii husidia kukuza uwezo was kiakili wa mtu. Ni rahisi kukuza kipaji cha mtu mwenye elimu ya darasani kuliko ikiwa tofauti. Hats nchi zilizoendelea bado wanaithamini elimu hii. Tafadhali naomba usome andiko langu pia. Ikikupendeza unipigie kura. Andiko linaitwa SoC 2022 - Acheni kutusimanga sisi wasomi wa Tanzania bonyeza io link utaliona.. Asante bwana GODFREY

Back
Top Bottom