Kiongozi wa Serikali ya Tanganyika Soma Hii; kwa Nini Viwanda Vidogo Nchini Pakistan ni Vingi?

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,832
21,431
Viwanda vile huitwa Cottage au SSI's kiufupi ni households industries, Karibia asilimia 45 ya vijiji vya Pakistan vinajitosheleza kwa mahitaji ya Viatu, Pamba kutoa nguo, spare za pikipiki, Cherehani, na vifaa vya kilimo, Kila familia ina Kiwanda kidogo na havifanani bidhaa.

IPI NI FAIDA YA VIWANDA VIDOGO

LABOUR INTENSIVE
🔹Hapa tunamaanisha, katika ufanyaji wa kazi ndani ya viwanda hivi idadi ya Watu ni kubwa kuliko idadi ya mashine, Pakistani katika research nyingi inaonekana 80 asilimia ya kiwanda watu ndio hufanya kazi, Hii inasaidia kupunguza idadi ya watu wasiokua na ajira, Pia inasaidia kujiajiri sababu mtu anapokua akifanya kazi yeye mwenyewe anajua nini kinafanyika ili kuzalisha bidhaa.


GAINFULL EMPLOYMENT TO WOMEN
🔹Ujue katika nchi za Pakistan na india mwanamke au watoto wadogo hawaruhusuwi kabisa kufanya kazi nje ya nyumbani, lakini ukiangalia videos nyingi za huko kwao utaona watoto na Wanawake, Hii ni kwa sababu wanafanya kazi nyumbani, kiwanda kinapatikana nyumbani, Hii inaongeza active labour-force. Pia Wanawake wamekua waanzilishi wa viwandaa vingi vya kuunda Makapeti na mishumaa.

RE-USE OF LARGE SCALE INDUSTRIES WASTE
🔹Mara nyingi viwanda vidogo hutumia hata mabaki ya viwanda vikubwa kutengeneza bidhaa, mfano viwanda vya sukari vikubwa India baada ya kukamua miwa, yale mabaki huchukuliwa na wamiliki wa viwanda vidogo kwenda kutengeneza spirit (Vilevi).

MEET THE DEMANDS OF LOCAL MARKET
🔹Kwa Pakistani pekee na India ni ngumu sana kuzalisha vitu vyako vikauzwe huko, Imagine mpaka vijijini watu wanaunda Feni na cherehani je Mjini watakua wakiunda nini? Kiufupi jamaa wanaokoa nchi yao katika foreign exchange maana pesa nyingi wana spent palepale na si kuinports.

FOREGN INCOME EXCHANGE
🔹Kwa research kadhaa inaonekana bidhaa kama Rugs, Carpets, Brassware nakadhalika zinasosafirishwa duniani, basi asilimia 30 hutoka Pakistan na india, hii ni kwa mujibu wa “export receipts”

REDUCES RULAL - URBAN MIGRATION
🔹Kama kijijini kuna Kazi, then bidhaa zinapatikana kwa urahisi, Ni nani atatoka Kijijini kwenda mjini asijue anaenda kufanya nini, ndio maana kuna point huitwa “disparity in income” yaani maeneo mengi ya vijijini yatakua na center zilizoendelea, maana watu watakua wengi, na huduma zitapatikana.

🔹Mwaka 2020 Serikali ya India kupitia Ministry of Statistics and Programme Implementation ilitoa matokeo ya research yao ambayo ilionyesha;

🔹Katika unit 100% za viwanda kiujumla vinavypatikana India, Basi Unit 95 ni viwanda vidogo wanvyoviita (SSI)
Pia waligundua kuwa vimeajiri jumla ya watu 175 lakh (Watu milioni 17,500,000)
Viwanda Vidogo ndani ya India vinachangia jumla ya asilimia 30% ya GDP, Huku vikichangia 33.4% ya bidhaa zinazozalishwa India kiufupi kwa sasa wanaviita “backbone of the Indian economy”


CP: ElimikaWikiendi na Mdemu Polycarp
 
Naambiwa hapa kwetu viongozi wote wanachaguliwa na mkuu wa nchi hapo tunapata watu ambao hawana creativity, hawa ni watu ambao hawajui nini wanaweza kufanya ili kuibadilisha Tanganyika yetu.
 
Nakubaliana na wewe nilikua naangalia clip moja wanakijiji huko nepal wanatengeneza nyuzi ..vikoi na mashuka ..kwa kiwanda local kwa style unayosema mleta mada
 
Jiwe alikuja na sera ya Tanzania ya viwanda mkamuita dictator na majina mabaya mabaya mengi mpaka mkamuua.

Mwingine akasema hata cherehani nacho ni kiwanda, mkamzomea.

Muda mwingine watanzania wanakuwaga kama madem, hawajui wanachokitaka.
 
Jiwe alikuja na sera ya Tanzania ya viwanda mkamuita dictator na majina mabaya mabaya mengi mpaka mkamuua.

Mwingine akasema hata cherehani nacho ni kiwanda, mkamzomea.

Muda mwingine watanzania wanakuwaga kama madem, hawajui wanachokitaka.
Sure mwamba alikuwa on the way, mimi nilimuelewa sana shida kubwa ni aina ya binadamu sisi ngozi nyeusi.
 
Wapakistan wametupita mbali sana, ni vyema tukajifunze kwao na si kuzurura kuleta wawekezaji ambao miaka nenda miaka rudi tutabaki kuwa tegemezi.
 
Back
Top Bottom