Kinondoni Makaburini: Mazishi ya Mwana JF, Mzalendo Sanctus Mtsimbe

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,614
Wana JF
Niko hapa Kinondoni Makaburi, kuwaletea pumziko la milele la mwana JF, Mzalendo Sanctus Mtsimbe.

View: https://www.youtube.com/live/PA4ndBZNpIE?si=EeOI7LGNCd2OU0J2

Tangu nimejiunga JF ile 2006, hii ndio mara yangu kwanza kuja kumzika mwana jf makaburi ya Kinondoni. Kwa jinsi makaburi ya Kinondoni ndani ya uzio yalivyojaa, whoever anayepata nafasi ya kizikwa Kinondoni, then either a VIP or a well connected person.

Tumewazika wana JF wenzetu wengi, ila hii ndio mara yangu ya kwanza tunazika mwanajf makaburi ya Kinondoni.

Mwili wa Marehemu umewasili Kinondoni makaburini tayari kwa mazishi kupumzishwa kwenye makao yake ya milele.

Sasa Jeneza lenye mwili wa marehemu limeishawekwa juu ya kaburi, ni jeneza la kisasa imported, na kaburi la kisasa ambalo limejengewa with tiles za white marble.

Sasa jeneza la mwili wa marehemu linashushwa kaburini kwa mashine ya motor ya umeme, mke wa marehemu analia sana huku anasema kitu....
Pia mama wa Marehemu analia sana,

Familia wanaweka udongo.
Ni kawaida kwa watoto kuwazika wazazi wao, inapotokea mtoto, ametangulia, na mzazi ndio anamzika mtoto, its very sad!, ni huzuni ya double tragedy kwasababu mzazi anajiuliza nani atamzika?.

Zoezi la kuzika limekamilika,
Sasa zoezi la mashada limeanza.
Shada la kwanza ni la mke wa marehemu mama JJ akiongozana na JJ.

Shada la pili ni Mama mzazi wa marehemu akiandamana pacha wake
Shada la tatu ni la madada na makaka wa marehemu na wenza wao.
Shada la 4 ni la viongozi wa Kanisa.
Shada la 5 ni la mwajiri, Wananchi Group

Toka msiba umetokea sikuwahi kuuliza cause of death, ila nilipoelezwa, nimemnyanyulia Mtsimbe mikono juu, huyu ni bonge la shujaa wa uhai hadi kifoni, kumbe alikuwa anakabiliwa na changamoto qya kiafya ya ugonjwa ambao ni terminal, hivyo alikuwa unaupigania uhai wake kimya kimya, na hakuwahi kuutaja na wala hakuwahi kuonekana with sick face, aulibeba ugonjwa wake moyoni mwake kimya kimya hadi amekufa kishujaa.

Kwa vile akiwa hai, mwenyewe hakuwahi kusema ana changamoto hiyo ambayo ni terminal illness, kwa heshima ya marehemu, naomba tuheshimu his right to privacy, hivyo naomba msiulize marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani, ila moja ya magojwa terminal, ila sio ugonjwa wa kuambukiza, na sio ngoma!.

Katika mabandiko yangu yaliyopita kumhusu Sanctus Mtsimbe, nilisema tuna fanana mambo mengi,
- Tribute to Sanctus Mtsimbe: Sio tu ni smart kwa mavazi na muonekano, pia ni smart kwa mawazo, maneno, na matendo, na very smart upstairs!

- Pumzika Sanctus Mtsimbe, Kazi Umekamilisha, Mwendo Umeumaliza. Asante Kutuachia Hazina Kubwa ya Maarifa Humu JF Tutakuishi Milele!. Pumzika

Leo msibani tumezidi kufanana, kumbe first wife yuko Marekani, na mini first wife yuko Marekani. Mtoto mkubwa alikuwa Marekani, na mimi watoto wakubwa wako Marekani.

Bongo akavuta kitu, dogo dogo, kitu white, chombo kweli kweli, mimi pia Bongo nimevuta kitu, white...
RIP Rafiki yangu Mzalendo Comred

Karibuni.

Paskali
 
Wana JF
Niko hapa Kinondoni Makaburi, kuwaletea pumziko la milele la mwana JF, Mzalendo Sanctus Mtsimbe.

Tangu nimejiunga JF ile 2006, hii ndio mara yangu kwanza kuja kumzika mwana jf makaburi ya Kinondoni.

Karibuni.

Paskali
Sote tunaopitia huu uzi tunaona, kwahiyo tafadhali tulete karibu picha zisipungue kwa kila update Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom