Kinondoni, Dar: Hamza mohammed, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

Kuna tukio limetokea hivi punde la mtu hasiejulikana kufyatua risasi hovyo na kuuwa askari , katika tukio hilo mpaka sasa hakuna taarifa za ndani juu ya tukio hilo zaidi ya mitandao ya kijamii kurusha picha za mtu huyo akiwa hai na nyingine akiwa amekufa. Sasa masikio na hamu tele kwa watanzania kujua huyo ni nani ? ametokea wapi? alikuwa anazungumza nini kabla ya tukio kutokea na kabla kuuwawa ? kwanini alielekea ubalozi wa ufaransa au kwanini alikuwa maeneo hayo ya darajani ? kwanini ameanza kushambulia askari ? Interlijensia ya Polisi nchini inasemaje kwa tahadhari? Je, umbo la Interlijensia linasema walikuwa wangapi na walipanga nini hasa? maswali mengi tunayo na tunawasubiri waandishi wetu hapa nchi , mana Marekani kupitia Ubalozi wao wameisha toa tahadhari kwa Raia wake , Je, Raia wa Tanzania wafanye nini ?
 
Ugaid
 
Lakini mkuu mgonjwa wa akili anawezaje kuseti bunguki mpaka kujua kurusha risasi,alafu mgonjwa wa akili akudhuru kabisa raia?,maswali ni mengi sana tusubiri uwenda tukapata taarifa nzuri zaidi.
Inategemea ugonjwa. Kuwa mgonjwa wa akili siyo lazima uwe kichaa.
 
Mkuu nimeangalia video ya yule askari aliyeuwa kuna makosa mengi kayafanya utafikiri hana mafunzo kabisa
 
Huyu jamaa siyo mjinga, kuna ujumbe alikuwa anaufikisha. Vyombo vyetu vya usalama vinabidi kwenda extra miles, wasiishie tu kusema tumemuua.
Natamani tupate ushahidi wa watu walio kuepo kwenye lile basi.Kuna maneno alikua anayaongea pale huenda yaka sugest alikua anataka kufikisha ujumbe gani.
 
Wamagharibi wamebadilisha title waonekane mabeberu ndio wamelengwa kwanin title isiwe TERROR ATTACK AT STANBIC BANK, TERROR ATTACK AT TTB haya mapimbi yanazinguaga sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…