Kinondoni, Dar: Hamza mohammed, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

Kuna tukio limetokea hivi punde la mtu hasiejulikana kufyatua risasi hovyo na kuuwa askari , katika tukio hilo mpaka sasa hakuna taarifa za ndani juu ya tukio hilo zaidi ya mitandao ya kijamii kurusha picha za mtu huyo akiwa hai na nyingine akiwa amekufa. Sasa masikio na hamu tele kwa watanzania kujua huyo ni nani ? ametokea wapi? alikuwa anazungumza nini kabla ya tukio kutokea na kabla kuuwawa ? kwanini alielekea ubalozi wa ufaransa au kwanini alikuwa maeneo hayo ya darajani ? kwanini ameanza kushambulia askari ? Interlijensia ya Polisi nchini inasemaje kwa tahadhari? Je, umbo la Interlijensia linasema walikuwa wangapi na walipanga nini hasa? maswali mengi tunayo na tunawasubiri waandishi wetu hapa nchi , mana Marekani kupitia Ubalozi wao wameisha toa tahadhari kwa Raia wake , Je, Raia wa Tanzania wafanye nini ?
 
Sawa tu hata wakitudanganya ila wakae wakijua hili tukio sio la kuchukulia masihala. Huenda akawa ni mmoja kati ya wengi ambao hawajajulikana bado.

Acha tumsubirie Mambo Sasa. Ila kwa Polisi wetu hawashindwi kutuambia alikuwa na Tatizo la Akili
Ugaid
 
Lakini mkuu mgonjwa wa akili anawezaje kuseti bunguki mpaka kujua kurusha risasi,alafu mgonjwa wa akili akudhuru kabisa raia?,maswali ni mengi sana tusubiri uwenda tukapata taarifa nzuri zaidi.
Inategemea ugonjwa. Kuwa mgonjwa wa akili siyo lazima uwe kichaa.
 
Huyu Jamaa hakupandwa na Malaria wala haumwi huyu mtu ni TIMAMU.

Naendelea kuangalia tukio hili ila nabaki na maswali ambayo Polisi wanatakiwa kujiuliza zaidi yetu.

Jamaa alikuwa na silaha 3 kuna video ambayo nimeipata na inaonesha jamaa ana mashine kubwa 2 na bastola moja.

Huyu jamaa anaijua bunduki vyema kwa jinsi ambavyo alikuwa anaonekana akiitumia huyu hakuwa CHIZI. Polisi wasichukulie poa hili tukio kuna maswali mengi sana ambayo yanahitaji jicho la tatu kupata majibu.

Kuna raia ambao walikuwa ndani ya daladala mita chache na alipo jamaa na hakuwadhuru kabisa japo angeweza. Alionekana akiongea maneno yenye kuashiria kitu na kujipiga kifua.

Polisi waulizeni hao raia waliokuwa karibu ni kipi alikuwa anakisema ili mjue mnapambana na tukio la aina gani.
Mkuu nimeangalia video ya yule askari aliyeuwa kuna makosa mengi kayafanya utafikiri hana mafunzo kabisa
 
Huyu jamaa siyo mjinga, kuna ujumbe alikuwa anaufikisha. Vyombo vyetu vya usalama vinabidi kwenda extra miles, wasiishie tu kusema tumemuua.
Natamani tupate ushahidi wa watu walio kuepo kwenye lile basi.Kuna maneno alikua anayaongea pale huenda yaka sugest alikua anataka kufikisha ujumbe gani.
 
Wamagharibi wamebadilisha title waonekane mabeberu ndio wamelengwa kwanin title isiwe TERROR ATTACK AT STANBIC BANK, TERROR ATTACK AT TTB haya mapimbi yanazinguaga sana
 
Back
Top Bottom