Vingunguti: Watu wawili wauawa kwa kupigwa na risasi

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
821
1,343
Watu wawili Wakazi wa mtaa wa Majengo, kata ya Vingunguti, wilaya ya Ilala, Dar es Salaam wamefariki baada ya kupigwa risasi jioni ya Jumatano, Desemba 27.2023. Akizungumza na Jambo TV leo, Ijumaa Desemba 29.2023 Kaka wa mmoja wa marehemu hao aliyejitambulisha kwa jina la Omari Shomari ambaye anadai kushuhudia 'ndugu zake' wakipigwa risasi amesema baada ya watenda kuwajeruhi marehemu hao awali waliondoka nao kwenye gari bila ndugu kujua watu hao ni kina nani na wamewapeleka wapi.

Hata hivyo hisia za awali za ndugu zilidhani ni Maafisa wa Polisi, hivyo kuchukua hatua ya kufuatilia kwenye vituo kadhaa vya Polisi na baadhi ya Hospitali bila mafanikio, kabla ya siku iliyofuata (Alhamisi, Desemba 28.2023) kupokea taarifa kuwa ndugu zao wamefariki na miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Amana; Jambo TV inaendelea kufuatilia zaidi kuhusiana na tukio hili, ikiwemo kupata taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam

Chanzo: Jambo TV

View: https://x.com/jambotv_/status/1740760090917863855?s=46&t=oRmMsM7qro-rKCtBSefuig
 
Probably BANDITS or wezi.
Hata iwe ni wezi hakuna justification ya kuua watu ambao hawana silaha. Jaribu kuingia YouTube usikiliza maelezo ya huyo kaka mtu ndiyo utajua ni mauaji ya kinyama. Wanasema polisi walikuwa wanafanya doria tangu mchana na walishawakamata na kuwaweka chini ya ulinzi. wakaanza kuwapiga risasi za miguuni na baadae mwilini tena mbele za watu. Mimi ndiyo maana huwa nasema watanzania tuko kama manyumbu. Mtu anaua na watu wanaona ni sawa tu.
 
Kwani wale wananchi wenye HASIRA KALI waliishia kizazi gani?

Oooh, sorry; kumbe tuko kwenye BEHIND THE CURTAIN WARRIORS generation.....well done TZN
 
Kama ni wezi, vibaka wale wanatoboa wenzao na visu kisa simu tu acha watwangwe risasi tu.
 
Kama ni wezi, vibaka wale wanatoboa wenzao na visu kisa simu tu acha watwangwe risasi tu.
Si usome kwanza kabla ku comment.haraka ya nini?? Siku moja atauliwa ndugu yako halafu utasikia vile wenzio walikuwa wanasikia. Kuwa binadam kidogo.
 
Hata iwe ni wezi hakuna justification ya kuua watu ambao hawana silaha. Jaribu kuingia YouTube usikiliza maelezo ya huyo kaka mtu ndiyo utajua ni mauaji ya kinyama. Wanasema polisi walikuwa wanafanya doria tangu mchana na walishawakamata na kuwaweka chini ya ulinzi. wakaanza kuwapiga risasi za miguuni na baadae mwilini tena mbele za watu. Mimi ndiyo maana huwa nasema watanzania tuko kama manyumbu. Mtu anaua na watu wanaona ni sawa tu.
Kama ni wezi hakuna cha huruma maana hata wao wezi wanaumiza wengi!! Mwizi siyo wa kumhurumia, dawa ni kupiga risasi tu!
 
washukiwa wote wa vitendo vya uwalifu hawana nafasi kwa sasa

pongezi kwa jeshi la polisi
 
Kama ni wezi hakuna cha huruma maana hata wao wezi wanaumiza wengi!! Mwizi siyo wa kumhurumia, dawa ni kupiga risasi tu!
Mahakama zimewekwa za nini? Utajua fulani ni mwizi bila kumfikisha mahakamani? Huoni utaratibu wa aina hii unatoa mwanya kwa polisi kuua mtu yeyote kwa kisingizio kuwa ni mwizi? Hivi kama mna ugomvi na mtu, na huyo mtu akampa polisi fedha nyingi ili akupige risasi kwa kisingizio cha kuwa wewe ni mwizi huoni unaweza kuuawa bila sababu?
 
Back
Top Bottom