Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,813
- 4,544
IGP Mstaafu Balozi Simon Sirro baada ya kuagwa rasmi na Jeshi la Polisi leo Dar es salaam amesimulia tukio ambalo hatolisahau akiwa kazini ambalo amesema ni la Askari Polisi kupigwa risasi na Majambazi baada ya kushambulia kwa risasi gari la Polisi katika Kijiji cha Uchembe, Kata ya Mjawa Wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani.
Sirro amesema “Tuliwapata Wahusika na bahati mbaya na wao walishatangulia mbele ya haki, hili ni tukio ambalo sitolisahau, ukienda ukakuta Askari tisa wote wamepigwa risasi wamelala sio jambo dogo”