Hili bango karibu na Ubalozi wa Ufaransa limenifikirisha

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,130
7,901
Juzi nilipita maeneo ya karibu na Ubalozi wa Ufaransa nikaona bango moja limeandikwa "Kifo cha Imam Husain kinatukumbusha umuhimu wa Uhuru". Huwa nina kawaida nikiona mabango ya dini napendaga kufuatilia zaidi maandiko yale hasa kama kuna ujumbe ambao umenigusa wakati huo.

Ila kuna kitu zaidi kilinigusa pale. Miaka kama 2 iliyopita kuna jamaa mmoja aliyejulikana kama "Hamza" alizua taharuki maeneo yale akarushiana risasi na polisi hadi akauawa. Hili tukio huwa nalikumbuka kila nikipita maeneo yale.

Baadae nilivyotulia nikasema embu ngoja nigoogle kama nitapata maarifa yoyote kuhusu maandiko yale na nimejifunza machache ya kunipa mwanga kidogo:

"Iman Hussein alikuwa mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Hussain (as) aliyeuawa Karbala, Iraq , siku ya Ashura."

"Alisimama kidete dhidi ya mtawala dhalimu wa wakati ule, Yazid bin Muawiya, akatoa fundisho la kukataa kumpigia magoti mdhalimu huyo, Ndipo akajitolea maisha yake, akauawa ili kunusuru ubinaadamu na utu."

"Imam Hussein (a.s) hakujitoa Muhanga yeye na familia yake kwa ajili ya Ummah wa Kiislam tu, bali alijitoa muhanga kwa ajili ya manufaa ya Ummah wote duniani."

Sasa mimi sina shida na maandiko hayo wala ndugu zangu wenye imani tofauti na mimi. Nimewaza tu busara ya kuweka bango lile mahali pale ukizingatia kumbukumbu ya tukio lililotokea mazingira yale na hapa simaanishi kama tukio lile lina uhusiano wowote wa masuala ya imani maana sidhani kama tuliwahi kuambiwa hivyo.

Kwa kumalizia, natamani kujifunza Uislamu. Naomba mwongozo naweza kuanzia wapi.
 
Juzi nilipita maeneo ya Namanga karibu na Ubalozi wa Ufaransa nikaona bango moja limeandikwa "Kifo cha Imam Husain kinatukumbusha umuhimu wa Uhuru". Huwa nina kawaida nikiona mabango ya dini napendaga kufuatilia zaidi maandiko yale hasa kama kuna ujumbe ambao umenigusa wakati huo.

Ila kuna kitu zaidi kilinigusa pale. Miaka kama 2 iliyopita kuna jamaa mmoja aliyejulikana kama "Hamza" alizua taharuki maeneo yale akarushiana risasi na polisi hadi akauawa. Hili tukio huwa nalikumbuka kila nikipita maeneo yale.

Baadae nilivyotulia nikasema embu ngoja nigoogle kama nitapata maarifa yoyote kuhusu maandiko yale na nimejifunza machache ya kunipa mwanga kidogo:

"Iman Hussein alikuwa mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Hussain (as) aliyeuawa Karbala, Iraq , siku ya Ashura."

"Alisimama kidete dhidi ya mtawala dhalimu wa wakati ule, Yazid bin Muawiya, akatoa fundisho la kukataa kumpigia magoti mdhalimu huyo, Ndipo akajitolea maisha yake, akauawa ili kunusuru ubinaadamu na utu."

"Imam Hussein (a.s) hakujitoa Muhanga yeye na familia yake kwa ajili ya Ummah wa Kiislam tu, bali alijitoa muhanga kwa ajili ya manufaa ya Ummah wote duniani."

Sasa mimi sina shida na maandiko hayo wala ndugu zangu wenye imani tofauti na mimi. Nimewaza tu busara ya kuweka bango lile mahali pale ukizingatia kumbukumbu ya tukio lililotokea mazingira yale na hapa simaanishi kama tukio lile lina uhusiano wowote wa masuala ya imani maana sidhani kama tuliwahi kuambiwa hivyo.

Kwa kumalizia, natamani kujifunza Uislamu. Naomba mwongozo naweza kuanzia wapi.
Duh.....🚶‍♂️
 
Kuna nyuzi nyingine ni ujinga mtupu. Hapo unajiona umefikiria kinyama..!!! Hamza alikuwa mhalifu na hakuwa na umuhimu. Sehemu walipofia watu waliokuwa na umuhimu kwa taifa pamejengwa minara ya kuwakumbuka.
Acha kukurupuka, soma kwanza na uelewe
 
Kuna nyuzi nyingine ni ujinga mtupu. Hapo unajiona umefikiria kinyama..!!! Hamza alikuwa mhalifu na hakuwa na umuhimu. Sehemu walipofia watu waliokuwa na umuhimu kwa taifa pamejengwa minara ya kuwakumbuka.
afande kidevu mbona povu
 
Mkuu unstupoteza France Embassy na Namanga ni parefu labda ungesema ulipita maeneo ya Feel Free Church pale jirani jirani na ubalozi wa ufaranzsa.
Ni jirani kabisa na ubalozi. Bango liko baada ya tu ya kituo cha ubalozi kama unaelekea Morocco
 
Hizo ni siasa za kijinga za Kisunni na Kishia zinqzowagawa Waislam toka aiku aliyofariki Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi wasalam.

Waislqm tunatakiwa tuwe Waislam. Full stop.

Siasa za kijinga hizo zisiwe na sehemu katika Uislam.

Nashukuru, mimi siyo sunni siyo shia. Mimi ni Muislam.
 
Hata hao mashia wanajiita waislamu

Swala wewe ni muislamu wa Aina gani??

Madhehebu yapo hayafichiki

Ndio maana Kuna Ile Hadith ya makundi 73
 
Hizo ni siasa za kijinga za Kisunni na Kishia zinqzowagawa Waislam toka aiku aliyofariki Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi wasalam.

Waislqm tunatakiwa tuwe Waislam. Full stop.

Siasa za kijinga hizo zisiwe na sehemu katika Uislam.

Nashukuru, mimi siyo sunni siyo shia. Mimi ni Muislam.
Kwa hiyo kuna Waislam hamuamini na hamkubaliani na ujumbe ulioko katika bango lile?

Pia naomba utuambie, lile bango lina uhusiano wowote na tukio lililotokea maeneo yale?
 
Hizo ni siasa za kijinga za Kisunni na Kishia zinqzowagawa Waislam toka aiku aliyofariki Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi wasalam.

Waislqm tunatakiwa tuwe Waislam. Full stop.

Siasa za kijinga hizo zisiwe na sehemu katika Uislam.

Nashukuru, mimi siyo sunni siyo shia. Mimi ni Muislam.
Si useme tu ukweli wewe ni Sunni!! Nyinyi ndiyo kila kitu ni kupinga pinga tu! Halafu mnajifanya wajuaji sana.
 
Hizo ni siasa za kijinga za Kisunni na Kishia zinqzowagawa Waislam toka aiku aliyofariki Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi wasalam.

Waislqm tunatakiwa tuwe Waislam. Full stop.

Siasa za kijinga hizo zisiwe na sehemu katika Uislam.

Nashukuru, mimi siyo sunni siyo shia. Mimi ni Muislam.
Nawe uliolewa na miaka 9 kama bi "A'isha"!!?
 
Hizo ni siasa za kijinga za Kisunni na Kishia zinqzowagawa Waislam toka aiku aliyofariki Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi wasalam. Waislqm tunatakiwa tuwe Waislam. Full stop. Siasa za kijinga hizo zisiwe na sehemu katika Uislam. Nashukuru, mimi siyo sunni siyo shia. Mimi ni Muislam.
Vipi msimamo wako kuhusu maulid? Maana kuna watu wanatoka povu hadi kuandaa munaqasha. Mimi sio muisilamu ila huko mitandaoni huwa nashuhudia malumbano si ya kitoto kuhusu maulidi, wengine wakisema ni ushirikina
 
Back
Top Bottom