.
Mimi nafikiri ungeweka bayana nini kingunge amesema badala ya kumuhukumu na kumwita kachanganyikiwa.
Hakika hata mimi nilipousoma niliona kuna athari kubwa sana katika jamii ya watanzania. Athari hizo ni :
1. Kwa kuwa umetolewa na madhehebu ya kidini, ulikuwa na lengo la kuelimisha waumini wake nini wafanye katika kuchagua viongozi wa kisiasa. Sasa nilijiuliza vipi wao viongozi wa kikatoliki, je walichaguliwa na nani kuwa viongozi, je waumini walishiriki katika kutoa mapendekezo au hata kuwachagua? au Pope aliwachagua ?
2. sasa nilijiuliza kama wao wliingia katika madaraka ya kuwa mapadr au hata maaskofu kwa kuchaguliwa na Pope , sasa vp waingile mambo ya kisiasa?
3. je kama Padre au Askofu anafundisha kuhusu Yesu vipi mtu huyu atasema achaguliwe mtu wa dhahebu lingine?
4. waraka ulikuwa na mengi yaliyojificha na yenye viashiria za ubaguzi ingawa yalipambwa na maneno mazuri sana.
Kijumla waraka ule ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa hususan kipindi hichi cha kupamba kwa UDINI huko Tanzania.
Namuunga mkono mzee Kingunge. maneno yake kuntu
Nikusaidie:
1. Kuna vijitabu viwili: Kimoja kinaitwa Mpango wa Kiuchungaji... Kijitabu hiki kina 'cover' ya kijani. Hiki kijitabu, kinachoelezea vipaumbele 7, kinaonyesha jinsi Kanisa lenyewe lilivyojipanga kutoa hiyo elimu ya uraia na kuwapata viongozi waadilifu na wenye sifa za uongozi hata ndani ya Kanisa lenyewe (yaani, ngazi mbalimbali za Kanisa). Wakati Kanisa linatoa elimu hii ya uraia kwa waamini wake, linataka pia viongozi wa Kanisa wchaguliwe kwa kufuata njia hiyohiyo ya uadilifu na sifa za uongozi!
Wewe unadhani waamini wa kawaida hawashirikishwi kuwachagua viongozi wa Kanisa. Siyo kweli. Soma The Code of Canon Law, linatoa mwongozo wa jumla nani anapaswa kuchaguliwa kuwa deacon (shemasi), padre na askofu. Kwa kifupi waamini wanashirikishwa katika ngazi mbalimbali.
Hata padre wa sehemu anakuwa anapata assessment kulingana na jinsi anavyoishi na kufanya kazi yake. Kama hafai, waamini wanaweza kimkataa na akishurutisha kukaa pale wanasusia kazi zake! Kwani hujasikia katika baadhi ya maparokia, waamini wanenda kumwona askofu kwamba hawamtaki padre fulani? Hata askofu asipokubalika ni hivyo tu.
Kwa taarifa yako: kijana anayejisikia ana wito anaomba kwenye jumuiya yake, ikimkubali anajaza fomu zinapelekwa parokiani. Viongozi wa parokia wanazipitisha na kisha kijana huyo jina lake linapelekwa kwa mkuu wa seminari. Kisha anaitwa kufanya mitihani kwa masomo yale ya sekondari. Muda wote anapoenda likizo, anakuwa na fomu inayopelekwa kwenye jumuiya yake ili waweze kuandika juu ya tabia yake na maendeleo yake na kisha inasainiwa na paroko.
Akimaliza masomo ya sekondari, anatuma maombi kwenda seminari kuu. Hayo maombi anayapeleka jumuiya ndogondogo (kwa Wakristo anaosali nao) ili wathibitishe kuwa wanamfahamu na anashiriki shughuli za kanisa na pia ana tabia nzuri.
Kabla ya kumaliza masomo ya seminari kuu, anaomba kuwa deacon (shemasi). Jumuiya yake inakuwa 'contacted' kama kuna pingamizi lolote. Kama hakuna na kama wanaona hawana shaka yoyote juu ya imani, tabia na wito wake anaitwa kuwa padre.
Kila padre ana faili lake pia na ripoti yake inatumwa Vatican kila mwaka kutoka jimboni mwake. Kulingana na kazi ya yule padre na kukubalika kwake katika Kanisa, kama kuna haja ya kupata askofu, anapendekezwa padre (kutoka jimbo lake) ambaye ana sifa na 'experience' ya kutosha ya kazi yake (including, pamoja na masomo mengine, awe ameshasoma na kufaulu vizuri Moral Theology na Canon Law).
Huu ndio utaratibu wa kuwachagua viongozi kama mapadre na maaskofu na wanakuwa kwenye 'screening' kali sana. Hivyo usidhani, padre, askofu au kardinali wanachaguliwa na papa (in fact, papa anapitisha jina lililopendekezwa na wengi by merit). Huwa kuna mapendekezo ya candidates kadhaa. Hata papa anachaguliwa kwa kura!
2. Kijitabu kingine - ILANI - kinatoa vipaumbele 7. Hiki kimetolewa kwa kila mtu anayeoona anaweza kukitumia. Hiki hakina maelezo mengine kama kile cha kijani kwa vile watumiaji wake wanaweza pia kuandaa utaratibu wao wa kutoa elimu hiyo kulingana na jinsi inavyowafaa wenyewe na siyo lazima wafuate maelezo yaliyomo ndani ya kile cha kijani kinavyoeleza kwani inawezekana mazingira na 'structures' za dhehebu au dini nyingine zikawa tofauti.
Ila cha muhimu ni elimu ya uraia ili wananchi wachague kwa utashi - yaani, watumie haki yao ya kupiga kura vizuri na wasidanganywe na hela, vitenge au pombe - vitu vinavyotolewa na baadhi ya viongozi. Kama wote hatutashiriki kuhakikisha tunachagua viongozi waadilifu ni sisi wenyewe tutakaokubali kuendelea kuongozwa na viongozi wabovu. Kwa hiyo, tunapolipinga Kanisa katoliki tujue tunachotaka kufanya ni kujipumbaza ili tuendelee kutawaliwa na viongozi wabovu!