King'amuzi cha Zuku

King'amuzi cha Zuku

stephot

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2012
Posts
17,746
Reaction score
27,214
Wadau hawa jamaa wa Zuku wametoka hapa kwangu sasa hivi kujipigia debe ili ninunue king'amuzi chao,sasa kwa anaejua tafadhali anijuze vipi kuhusu ubora wa matangazo yao na uzuri wa channel zao,naombeni mniwahi jamani kabla jamaa hawajanilia hela zangu maana tumekubaliana waje tena Ijumaa.
 
Shillingi ngapi wamekuambia..! Kiukweli kiko poa sana aisee na wana station zao kama dstv na local ipo tbc tu...

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums[/QUOTE
Wameniambia ni 140,000/=
 
Wadau hawa jamaa wa Zuku wametoka hapa kwangu sasa hivi kujipigia debe ili ninunue king'amuzi chao,sasa kwa anaejua tafadhali anijuze vipi kuhusu ubora wa matangazo yao na uzuri wa channel zao,naombeni mniwahi jamani kabla jamaa hawajanilia hela zangu maana tumekubaliana waje tena Ijumaa.

POINT OF CORRECTION
Zuku si king'amuzi..Kuna ving'amuzi vya aina tatu tu

1.Digitek
2.Startimes
3.ATN

Zuku ni sawa na Dstv, Eazy Tv etc
 
Binafsi bado sijaamua kama ninunue king'amuzi gani.Ila kwa waliotumia kuna wanaosema wakati wa mvua kinazingua.Na kuhusu channels inategemeana na wewe uko interested na nini.Kama ni soccermania,hapo sio mahali pako,ila kama ni moviemania kinaweza kukufaa.

Ila nakataa,huwezi kukilinganisha na DSTV kwa namna yoyote.Dstv kwa africa bado sana kupata mpinzani.
 
Mkuu kingamuzi maana yake ni decoder(ingawa nasikia tumeambiwa tuite jina gani vile, sijui).Mtoa mada yuko sahihi wewe ndio unaelewa vibaya.Hata mediacom,strong etc vyote ni ving'amuzi.Ungeeleweka kama ugesema kuna kampuni na decoder maana hata ATN decoder yao inaitwa Ting.
 
Hold on,em tueleze zuku ni nini kama si king'amuzi??
 
Ni service provider wa pay TV kama ilivyo kwa Easy TV, Ting, Dstv, CTV ama Startimez. Ushaelewa?

Mule mule...
Kweli nakubali,tulikuwa hatujajiandaa kwa ajili ya mabadiliko haya ya kidigitali..
 
Hold on,em tueleze zuku ni nini kama si king'amuzi??

@Idimi kamaliza kila kitu..na hata vituo kama Dtv, Clouds Tv, C2C etc..ni public broadcasters tu kuna vituo vi 5 tu kama taifa vimesajiliwa..ITV, EATV..Channel 10. TBC1 NA sTAR tV
 
Shillingi ngapi wamekuambia..! Kiukweli kiko poa sana aisee na wana station zao kama dstv na local ipo tbc tu...

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

hapana bwana local channel zipo 3 tbc chanel ten na clouds
 
Binafsi bado sijaamua kama ninunue king'amuzi gani.Ila kwa waliotumia kuna wanaosema wakati wa mvua kinazingua.Na kuhusu channels inategemeana na wewe uko interested na nini.Kama ni soccermania,hapo sio mahali pako,ila kama ni moviemania kinaweza kukufaa.

Ila nakataa,huwezi kukilinganisha na DSTV kwa namna yoyote.Dstv kwa africa bado sana kupata mpinzani.
Mkuu huyu jamaa kaniambia wana chanells 5 zinaonyesha premier ligue live ndio ikanifanya nikubali aje hiyo ijumaa,is there any truth?
 
@Idimi kamaliza kila kitu..na hata vituo kama Dtv, Clouds Tv, C2C etc..ni public broadcasters tu kuna vituo vi 5 tu kama taifa vimesajiliwa..ITV, EATV..Channel 10. TBC1 NA sTAR tV

Busara iko hivi: Ukipenda kukosoa wenzako,ni vema na wewe ukakubali kukosolewa.
Wewe umeulizwa swali:Zuku ni nini kama sio king'amuzi? Hujamjibu.Idimi kasema Ting ni service provider,wewe umekubali,je tuna kampuni hapa Tanzania inayoitwa Ting? Zuku ni kampuni,hilo wote tunafahamu,je decoder(ving'amuzi) zinaitwaje?

Halafu pia utuambie maana ya puplic broadcasters.Je ITV,EATV,CH10,TBC1 na Startv wenyewe si public broadcasters?Na kama sio sio,wao ni akina nani?
 
Mkuu huyu jamaa kaniambia wana chanells 5 zinaonyesha premier ligue live ndio ikanifanya nikubali aje hiyo ijumaa,is there any truth?

Mkuu sijajua ni channels gani hizo 5 zinazorusha Premier Ligue. Kwa package ya Kenya kuna KISS TV inayorusha mechi moja tu ya EPL kila wiki kama ilivyo kwa Star TV.Wanaweza wakawa wanakupiga sound tu,lakini uwezekano wa kuwa na chanels 5 zote zinarusha Premier Ligue mimi naona haiwezekani.Labda zinarusha recorded games lakini haiwezekani kurusha live games kwenye channels 5.Au labda wakuambie Primier Ligue ya wapi,labda ya uarabuni na Asia.

Hapo ndugu,akili za kupewa.....!!!
 
Mkuu kingamuzi maana yake ni decoder(ingawa nasikia tumeambiwa tuite jina gani vile, sijui).Mtoa mada yuko sahihi wewe ndio unaelewa vibaya.Hata mediacom,strong etc vyote ni ving'amuzi.Ungeeleweka kama ugesema kuna kampuni na decoder maana hata ATN decoder yao inaitwa Ting.

Uko sawa Mkuu...
 
POINT OF CORRECTION
Zuku si king'amuzi..Kuna ving'amuzi vya aina tatu tu

1.Digitek
2.Startimes
3.ATN

Zuku ni sawa na Dstv, Eazy Tv etc

Msaada tafadhali! Sifa za king'amuzi ni zipi mpaka ukasema ving'amuzi ni aina tatu tu ulivyovitaja!
 
Mkuu kingamuzi maana yake ni decoder(ingawa nasikia tumeambiwa tuite jina gani vile, sijui).Mtoa mada yuko sahihi wewe ndio unaelewa vibaya.Hata mediacom,strong etc vyote ni ving'amuzi.Ungeeleweka kama ugesema kuna kampuni na decoder maana hata ATN decoder yao inaitwa Ting.

Mzee wanataka tuite KISIMUZI! badala ya KINGA'MUZI
 
Back
Top Bottom