Kingai Pekee ndiye aliyeweza kupambana na Mbowe akishia kupandishwa cheo; wengine wote wameishia pabaya

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Mbowe ameweza kupambana na watu wengi wa mfumo chinichini Bila kuonyesha adharani mashinikizo yake. Waliobomoa Mashamba yake huko Hai wote wameondolewa kwenye mfumo, viongozi waandaminizi waliokuwepo wakati ananyanyasika nao wametupwa nje Kwa fedhea. Walioitwa viongozi WA dola waliamini mfumo unaweza kuwaacha kumbe lilikuwa suala la muda Tu.

Yeye Leo hii yupo kwenye headlines akijadiliana hoja na mkuu WA nchi wao wapo huko walipo awajui watadumu Kwa muda gani.

Siku Mhe. Rais anazungumza na viongozi WA vyama vya siasa, alimaliza akafanya uteuzi. Nani ajuaye kama uteuzi ule ndio unaomfanya Mbowe aseme anampongeza Mhe. Rais? Nani ajuaye hayo mazungumzo yaliwaweka kikaangoni viongozi wangapi?

Najadili hii hoja Leo nikukumbuka kwamba hata DCI wa SASA amekuwa mkiamya Sana ofisini tangia ateuliwe tofauti na namna alivyokuwa anatenda kabla ya uteuzi.

Kauli ya Mbowe Mwanza imebeba ujumbe mzito Sana kwamba maridhiano yanaambatana na mabadiliko ya viongozi tuje na safu mpya ndani ya utumishi wa umma.

Yaonekana hayakuwa maridhiano ya kisiasa ,yalikuwa maridhiano yenye lengo la kutoruhusu watu kuumizwa kama ilivyotokea hapo nyuma. Haya maridhiano siyo ya chadema Vs CCM Mayaona yakiwa NI maridhiano ya walioumizwa ndani na nje ya CCM Vs wale waliowaumiza.

Maridhiano haya yanakwenda kubomoa kabisa nyoyo za wale waliojichukulia sheria mkononi, yanawanyima Amani wale waliokuwa mstari wa mbele kuumiza au kubambikia kesi watu. Yanakwenda kuweka misingi ya matajiri kutokuishi kama mashetani.

Tusubiri kichapo cha maridhiano kiendelee kutembea kwenye barua za Zuhura Yunus......ninyi mdhaniao mmesimama na kuaminiwa mnajidanganya time imefika yakukabidhi Ofisi.

Ishini na na watu vizuri
 
Back
Top Bottom