Kinachosababisha JK aogopwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kinachosababisha JK aogopwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by akashube, Oct 17, 2010.

 1. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Huyu jamaa ni mlipa visasi namba moja nchi hii, na pia ni mlipa fadhila mkubwa.

  1. P. Mang'ula aliyekuwa mkti wa kampeni za CCM 2005 alionyesha kutomkubali matokeo yake kila alikojaribu kugombea kwenye chama kapigwa chini. Mkono wa JK haukumwacha Ikiwemo kwenye kugombea uenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa. Leo hii kakaa benchi mpaka amegeuka benchi yeye mwenyewe.

  2. S. A. Salim alipoamua kugombea urais 2005, JK alimuona kama msaliti na kumzushia kuwa ni mwarabu wa Oman hivyo hastahili kuwa Rais. Hili limerudiwa kwa Bashe ambaye hata ugomvi wake haukuwa na JK bali na kundi la RK. Lakini JK mwenyewe akarudia yale ya Salim, kwamba Bashe, kada wa CCM ati ni msomali......

  3. Prof. F. Sarungi katika moja ya mikutano ya mwisho ya bunge 2005 aliombwa na JK wakiwa bungeni, wote wakiwa mawaziri ili amsaidie kwa kuwa JK alikuwa na nia ya kugombea. Prof alikataa ombi hilo kwa dharau kubwa, matokeo yake tunayaona leo Sarungi kafifishwa kabisa.

  4. E.N Lowasa, B.P Mramba, A. Mgonja, A. Chenge, J. Mungai na wengineo walionyesha kuanza kuleta fukuto za chini chini za kuhoji utendaji kazi wa JK, kilichotokea ni kwamba katika jambo lililohusu serikali nzima ya JK wametolewa kafara wao. Swahiba wake Z. Meghji ambaye ni muhusika mkuu, tena siku zote ndiye mweka hazina wa pesa za wizi zinazotumika kumuweka JK ikulu ikiwemo zile za EPA, yeye hakuguswa. Na Rostam je? Na Kagoda je? wakiguswa nchi itapasuka????? Na hapa Watanzania wamepigwa changa la macho......

  5. H. Mwinyi na uwaziri wa ulinzi ni matokeo ya kulipa fadhila kwa Mzee A. H. Mwinyi.

  Mengineyo utajaza mwenyewe kama:

  i) V. Kamata na kanafasi ka BOT, na ubunge viti maalum, na kusomeshwa nje, fadhila kwa kazi gani?

  ii) Mrema alivyolamba miguu ya JK na kusaidiwa matibabu, kisha karudi, sifa zote kwa JK, JK tayari katoa ridhaa yake kuwa CCM wamsaidie Vunjo apate ubunge.

  iii) N. Nnauye mambo vipi? hapa siongezi neno....maana ya juzi haya unayakumbuka???

  iv) L. Masha muajiri wa RK naye ni muajiriwa wa baba yake RK au ikoje?.....

  v) Unadhani wabunge waliotetea sana kiswahili bungeni walifanya hivyo kwa uzalendo??? no..no...no... usidanganyike kirahisi, hapo watu walikuwa wanamkingia kifua mama.....mama....mama jamani hamuelewi....mama SK ebo? fadhila zinatafutwa.

  Shibuda shibuda, naona kalamu inagoma goma

  USIONE WATU WANAUNGA UNGA MKONO CCM NA JK HUMU NA KWINGINEKO. MOYONI HAWAMTAKI LAKINI WANAHOFU KUBWA JUU YA KITAKACHOJIRI AKICHUKUA NCHI.

  NCHI HAITAWEZA KUENDELEA BILA WATU KUACHA UNAFIKI NA WOGA HUU WA KIPUUZI!!!!

  JK wapi Babu Seya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 2. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imetulia! Yule balozi wa Italia...professor nani vile M...? Visasi!
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hivi wewe jaribu kuangalia hali halisi ya kisiasa, je unaweza kuwachaguwa watu ambao hawajakuunga mkono kwenye kutafuta uongozi au madaraka...? Itakapotokea kuwa umewachaguwa tena na kukuendea kinyume utasemaje...!?

  Malalamiko mengine hayana maana hata kidogo.
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Major Ganeral Lupogo . Alimfanyia mavisa hadi leo . Jk ni Hoolgan
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Obama kamchagua Mama Clinton, Mkapa alimchagua Kikwete na hata Dr.Slaa atamchagua Kikwete kuwa balozi wetu Marekani!...
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  duh....mambo ni mengi
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Liyumba alimchukulia Bibi miaka hiyooo....................

  Mwaka 2005 walipotangaza matokeo, Lipumba akaanza kulia.......

  Akasema wazi kabisa kuwa "mwenzenu ni mfungwa sasa.............."

  Mwakawago yalimpata hayahaya na Mzee FMes alitumwagia hapa shule alivyofanyiwa Unyama.

  RIP Mwakawago.
   
 8. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Uwe mwepesi wa kusoma mada lakini sio kujibu, inahitaji uwe 'great thinker' na ninaamini ndivyo ulivyo, ila hapa hukujitendea haki. Jiulize yafuatayo:

  1. Unahalalisha mtu aambiwe si raia wa Tanzania na kunyimwa haki yake ya kuchaguliwa kwa kuwa tu ametumia haki yake kwa kuamua kugombea cheo unachogombea wewe au pengine amekupinga???

  2. P. Mang'ula kwa mfano ujue hakuwa mnafiki, alimwonyesha wazi JK kuwa hamuungi mkono, je unahalalisha kwa hilo kuwa afanyiwe fitina kwa mkono wa JK hata pale alipotumia haki yake kugombea nafasi ndani ya chama chake. Ukumbuke hii ilikuwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM, na alipopita JK, Mang'ula alimuunga mkono kama mgombea wa chama chake....na alichangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta ushindi...kumbuka alikuwa ni mwenyekiti wa kampeni. Sasa visasi hivi unaviunga mkono.

  Yaani mtu awe anapita kwa asilimia 100% yaani asipingwe? anayekupinga ni adui? hiyo ni demokrasia au domokrasia?

  3. Uswahiba na unafiki ndio iwe 'qualification' ya watu wa karibu na wewe. Halafu matokeo yake unabadilisha badilisha baraza la mawaziri, tena si kwa matakwa yako bali kwa sababu Dr. Slaa amekuja juu na hataki mambo yenu ya uendeshaji serikali kipuuzi.

  Suala hapa ni ule upofu na jazba ya kulipa fadhila au kisasi badala ya kufanya kazi ya nchi.

  Hey 'THINK'. acha ushabiki.
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Kwani Hillary Clinton alimuunga mkono Obama.?we vipi bana
   
 10. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Huyu sidhani kama ali'think' kama great thinker, naona alikurupuka kujibu. Kama ameamua ku'think' atakuwa amejifunza ili aje na hoja ng'amuzi.

  Hili swali lako litamwamsha.
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Jamani si kila mtu huwa na vipa umbele vyake linapokuja suwala la kuchaguwa wasaidizi au viongozi!? Hapa mimi nashindwa kuelewa, alipaswa kuchaguwa vile alivyo ona yeye inafaha, vile mnavyo ona nyinyi inafaha?
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mambo yenu tena, mbona hapo sijakuelewa, mambo yenu yapi?
   
 13. s

  sirgeorge Member

  #13
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF nasikia kwa mama Mbega nayo ni Fadhila, mwenye data please. Maana nilikuwa naongea na jamaa mmoja toka Iringa alinigusia hilo kuwa ni fadhila toka uchaguzi wa mwaka 2000 mpaka leo mama huyo huwa anabebwa katika kugombea ubunge kitu ambacho kimetokea kwa mwakalebela kupigwa chini ingawaje kutokana na maneno ya Makamba kuwa wote walitoa rushwa ingawaje walitofautiana, Sasa kwa mama huyo rushwa yake ilizidi ile Mwakalebela?au ndo mambo ya fadhila?

  Vipi tena kuhusu mpiganaji selelii? usikute naye ni kisasi maana si yeye aliyehoji kuhusu upanuzi wa barabara ya chalinze-segera wakati ndo njia ya JK? Mwenye data please!

  All da best
   
 14. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Kuna tofauti kubwa sana katika siasa za marekani na tzn "afrika kwa ujumla" sula la kuzushiwa uraia siliungi mkono ila swala zima la kumchaguwa mpinzani wako serikalini..??? Acha weweee... Waafrika sisi tukichuklia tumechukiwa anaweza akaharibu mipanga yako yoote ilimradi kukudhalilisha kwenye ndio akaweka sio na kwenye sio akaweka ndio
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  wewe ndio hujaelewa mleta mada, umeamua kuelewa kivyako... sikiliza usikilizwe!!
   
 16. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hapa kwa Selelii nadhani inabidi tumuulize Dr. Rosti tamu ya mzizi.....kumradhi ninamaanisha R.Aziz mwenye kuvuna asichopanda kupitia Caspian, jamaa wanachimba dhahabu na hawalipi chochote serikalini zaidi ya kuongeza ajira kwa watoto wa mafisadi na kutoa 'takrima' kwa JK....sasa muulize Rosti ya Mzizi...Selelii alihoji nini juu ya hili???

  CCM kunanuka mambo nyie....ndo mana kuna watu wako radhi watoe mtu roho lakini sio CCM itoke madarakani maana wanajua uozo wao mwingi utajulikana.

  Selelii kashadanganywa saa hizi kuwa atapewa ukuu wa mkoa......na advertise ya kwanza ni Nape, JK kweli noma...anaujua vyema mchezo wa karoti na fimbo.....jamaa wanachezewa kama ngedere wa kufugwa.
   
 17. S

  Subira Senior Member

  #17
  Oct 18, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  nakuaminia X hawa wenzetu wanataka nini, hakuna hata mkuu mmoja anaefanya tofauti hata huyo slaa akiingia naona watu jf wengi watakuwa mawaziri
   
 18. S

  Subira Senior Member

  #18
  Oct 18, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kiongozi anachaguliwa na mungu bwana no matter what, mtasema mengi lakini hata slaa akiingia utashangaa ya firauni tupiganie kuondoa uovu ndani ya nchi yetu kwa amani si kwa kubezana, hakuna aneweza kutawala 100percent bwana,
   
 19. S

  Subira Senior Member

  #19
  Oct 18, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mi nawauliza wenye kutaka mabadiliko, haya yametokea kwenye nchi zetu nyingi za kiafrica,Zambia n.k wamebadilisha vyama viliyooriginate kuleta uhuru, lakini kuna nini cha ajabu mlichokiona kimebadilika jamani tusijidanganye, tutatue matatizo yetu kwa njia sahihi. CCM hadi sasa haijakaa vyema tokaa ichukue nchi,miaka zaidi ya hamsini, hilo ni wazi , lakini tukiitoa madaraka leo tutegemee miaka mingine sitini au zaidi kwa chama kingine kukaa sawa,
   
 20. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 849
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Vipi kuhusu Mzee Mandela na Chifu Buthelezi wa Inkhata?
   
Loading...