Kinachosababisha JK aogopwe

Uwe mwepesi wa kusoma mada lakini sio kujibu, inahitaji uwe 'great thinker' na ninaamini ndivyo ulivyo, ila hapa hukujitendea haki. Jiulize yafuatayo:

1. Unahalalisha mtu aambiwe si raia wa Tanzania na kunyimwa haki yake ya kuchaguliwa kwa kuwa tu ametumia haki yake kwa kuamua kugombea cheo unachogombea wewe au pengine amekupinga???

2. P. Mang'ula kwa mfano ujue hakuwa mnafiki, alimwonyesha wazi JK kuwa hamuungi mkono, je unahalalisha kwa hilo kuwa afanyiwe fitina kwa mkono wa JK hata pale alipotumia haki yake kugombea nafasi ndani ya chama chake. Ukumbuke hii ilikuwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM, na alipopita JK, Mang'ula alimuunga mkono kama mgombea wa chama chake....na alichangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta ushindi...kumbuka alikuwa ni mwenyekiti wa kampeni. Sasa visasi hivi unaviunga mkono.

Yaani mtu awe anapita kwa asilimia 100% yaani asipingwe? anayekupinga ni adui? hiyo ni demokrasia au domokrasia?

3. Uswahiba na unafiki ndio iwe 'qualification' ya watu wa karibu na wewe. Halafu matokeo yake unabadilisha badilisha baraza la mawaziri, tena si kwa matakwa yako bali kwa sababu Dr. Slaa amekuja juu na hataki mambo yenu ya uendeshaji serikali kipuuzi.

Suala hapa ni ule upofu na jazba ya kulipa fadhila au kisasi badala ya kufanya kazi ya nchi.

Hey 'THINK'. acha ushabiki.
naziona hekima za Baba wa taifa hapa.
Thanx sana AKASHUBE umetoa assumption ya karne sana hapo.
Asomaye na afahamu

 
kiongozi anachaguliwa na mungu bwana no matter what, mtasema mengi lakini hata slaa akiingia utashangaa ya firauni tupiganie kuondoa uovu ndani ya nchi yetu kwa amani si kwa kubezana, hakuna aneweza kutawala 100percent bwana,

Huyo mungu unayemuongelea ni yupi make Mungu wetu hataki kabisa mambo ya rusha na dhuluma kwa ujumla.

CHADEMA hawana akili kama za sisiem za kugawana madaraka kama pipi...Usitegemee kuwa Dr. Slaa atafanya hivo.
Na bado mbona mtasema mengi!!
 
Akashube uko juu sana. Nimejifunza kuwa we una uchungu na nchi yako pia ni mpenda haki na mzalendo wa kweli. Kuna watu kama X Pasta wasaliti wananufaika na mfumo huu mbovu wa uendeshaji wa nchi na hao hata uwambie vipi hutabadili msimamo wao. Mungu huyu yuko wapi tunamlilia mbona hatusikii? tumechokaaaaaaaaa!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom