Kinachoendelea Zanzibar ni aibu kwa nchi

Kinachoendelea Zanzibar ni aibu kwa nchi

hv kuna nchi yoyote ya Africa iliyowahi kuitawala nchi ingine hapa africa zaidi ya TANGANYIKA?
Mi siogopi jina lako hata kidogo,kwa kukujibu,kama hoja ni kutawala tu,Tanzania iliitawala kwa muda Uganda mara baada ya Vita ya ukombozi. Pia Tanzania ilitawala Anjuani kabla hawamuweka Rais wanayemtaka na pote huko palitawaliwa na maafisa wa jwtz wenye vyeo vya kanali. Sheli sheli pia ilishawahi kushikwa na Tanzania kwa miezi kama mitatu,kwahiyo sioni la ajabu as long kwamba Zanzibar ina undergo security unrest kuelekea uchaguzi wa marudio[emoji4]
 
Kwanza kampita kwa kura 25,000. Wewe unazungumzia yaliyotangazwa na jecha pale bwawani hujuwi kuwa uchaguzi ulikwisha tokea tarehe 25 Oktoba saa kumi na moja za jioni na matokeo yote yalikwishapatikana tarehe 26 oktoba 2015.

Uliza uambiwe nini kilikuwa kinaendelea pale kisiwandui. Baada ya kupata taarifa KUWA UPINZANI KWA MUJIBU WA MATOKEO YA NCHI NZIMA MAJIMBONI ulishashinda ulizia kama una vyanzo vya kutosha.

Hii ni aibu kwa nchi
Seifu mwenyewe amesema kuwa amempita kwa kura hizo
 
Umeongea vizur sana.Sisi tuliopo Unguja hali ipo kama kawaida.Pemba ulinzi umeimarishwa baada ya matukio ya uchomaji moto ya hivi karibuni.Ila nachukia siasa coz zinatutenganisha na washakaji zetu.
 
Yaani kasoro za uchaguzi na criteria za kuharibika anazijuwa jecha peke yake dunia nzima akuisaidiwa na vuai Ali Vuai Naibu Katimbu Mkuu wa CC....
Nilibahatika kukutana na watu waliokuwepo kwenye uangalizi wa uchaguzi na ambao walishiriki mazungumzo ya usuluhishi kabla Maalim Hajajiengua wanasema hawapingani na tuhuma kwamba cuf kwa namna moja ama nyingine kuna maeneo walicheza rafu za wazi kabisa unasemaje kuhusiana na hilo?
 
Nilibahatika kukutana na watu waliokuwepo kwenye uangalizi wa uchaguzi na ambao walishiriki mazungumzo ya usuluhishi kabla Maalim Hajajiengua wanasema hawapingani na tuhuma kwamba cuf kwa namna moja ama nyingine kuna maeneo walicheza rafu za wazi kabisa unasemaje kuhusiana na hilo?
Yaani rafu za wazi dunia nzima wasizione azione jecha pekee? hii sio sawa.

Tena baada ya tarehe 28 Oktoba na tena kwamba hata fomu za malalamiko sizijazwe tena na chama tawala ambacho wako kila idara?

Kwamba CUf wawe na uthubutu huo halafu chama dola kisubiri tu?
 
Yaani rafu za wazi dunia nzima wasizione azione jecha pekee? hii sio sawa.

Tena baada ya tarehe 28 Oktoba na tena kwamba hata fomu za malalamiko sizijazwe tena na chama tawala ambacho wako kila idara?

Kwamba CUf wawe na uthubutu huo halafu chama dola kisubiri tu?
Mwenye Jukumu la kuziconfirm hizo rafu ni Jecha pekee kwa dunia nzima....yeye ndiye mwenyekiti wa zec na mwenyekiti wa zec yupo mmoja dunia nzima...
 
Mwenye Jukumu la kuziconfirm hizo rafu ni Jecha pekee kwa dunia nzima....yeye ndiye mwenyekiti wa zec na mwenyekiti wa zec yupo mmoja dunia nzima...
Umeona eee

Kwamba rafu za wazi zilikuwa invisible kwa tume yenyewe kule majimboni, mawakala, waangalizi na wana -CCM katika majimbo husika kiasi cha kushindwa hata Kujaza fomu za kulalamika na kufuata taratibu sio? basi itakuwa jecha ana macho ya ajabu ya dunia .

Hizo rafu za wazi zimekuja tarehe 28 baada ya kushindwa?

Aibu kwa nchi
 
Usisumbuke bure.

"Mwenyekiti alikuwa hajisikii akaondoka ofisini, wenzake wanaendelea na zoezi la kuhakiki wakiongozwa na makamo mwenyekiti ambae ni jaji wa mashakama kuu, wakashtushwa na tangazo la jecha la kufuta uchaguzi akiwa peke yake kwenye ZBC TV. Hafla Ofisi za tume za bwawani ziliwekwa undersiege na JWTZ na makamo mwenyekiti alikamatwa kwa muda. hayo yakifanyika tayari uchaguzi ulishaisha siku tatu"

Sasa wewe endelea kuamini lakini hii ni Aibu
 
Umeona eee

Kwamba rafu za wazi zilikuwa invisible kwa tume yenyewe kule majimboni, mawakala, waangalizi na wana -CCM katika majimbo husika kiasi cha kushindwa hata Kujaza fomu za kulalamika na kufuata taratibu sio? basi itakuwa jecha ana macho ya ajabu ya dunia .

Hizo rafu za wazi zimekuja tarehe 28 baada ya kushindwa?

Aibu kwa nchi
Hukujibu swali nililokuuliza mwanzo, je Cuf haikuhusika katika kuvuruga uchaguzi uliofutwa ama la?
 
Kwanza kuna matukio hayapati nafasi katika vyombo vya habari vingi kuhusu kile kinachoendelea Zanzibar. Zikiwa zimebaki siku sita tu kufanyika kile kinaitwa uchaguzi wa marudio hali ya Zanzibar ni Aibu.

Kwa sasa kumepelekwa vyombo vya ulinzi kwa wingi wakiwemo wanajeshi hasa kisiwani pemba na tayari vyombo hivyo vinaonekana wazi wazi kuleta athari. Kumeripotiwa taarifa za vifaru vya jeshi kuonekana vikitembea barabarani mchana kweupe na wananchi kuingiwa hofu.

Hali hii hujitokeza Zanzibar pekee katika Tanzania hii. Lengo lake halijulikani kama ni huu uchaguzi wa marudio au kuna zaidi ya uchaguzi.

Kuna mpasuko mkubwa wa kijamii. Imefika wakati hasa kisiwani Pemba watu wameshaanza kususiana mambo mbali mbali.

Mifano.

i. Kususiwa baadhi ya wananchi kusafirishwa kwa kivuko kutoka kisiwa kidogo (Kisiwa Panza) kwenda chokocho. Ifahamike mgogoro huu unafukuta na unahusishwa na siasa za uchaguzi wa marudio.

ii Kususiwa kwa baadhi ya mambo ya kijamii ikiwemo maziko na shughuli ya harusi. Maeneo mbali mbali yamejitokeza kwa njia baridi huko Pemba.

iii. Kuna taarifa za viongozi wa kitaifa Zanzibar (Sitaji Majina) kususiwa misikiti zaidi ya mara mbili pale inapopatikana habari kuwa wanakwenda kuswali jamii inasusa kwenda na kuwaachia viongozi wa serikali peke yao. Zipo taarifa ni hapa majuzi kiongozi mmoja alisusiwa ufunguzi wa msikiti hali iliyolazimu kuletwa askari wa kikosi fulani kuongeza idadi ya watu.

iv Kuzomewa baadhi ya viongozi wa kitaifa huko kisiwani Pemba na kususiwa kwenye shughuli za
maendeleo

Kwa ufupi kuna hali mbaya Zanzibar imeanza kujitokeza na inatarajiwa kukua na kuongeza uhasama zaidi. Watu wameanza kuchoma nyumba moto na baraza za vyama vya siasa.

Kuna hali ya kutiliana mashaka na ukimya wa kutisha unaoashiria shari, kuna kutishana kwa kutumia vyombo vya dola. Kumeanza kupigwa marufuku mikusanyiko katika baadhi ya maeneo Zanzibar.

Kuna masuali ya kujiuliza Nini hatima ya Zanzibar ikiwa hali iko hivi sasa kabla ya kufanyika uchaguzi wa marudio uliosusiwa na wadau wakubwa wa Zanzibar? jee Kutakuwa na suluhu yoyote?

Haya yanatokea viongozi ni kama hawapo, wana dini ni kama hawapo, taasisi za kiraia ni kama hazipo, taasisi za haki za binadamu ni kama hazipo, taasisisi za kisheria ni kama hazipo, vyama vya siasa ni kama havipo na wengineo.

Tutegemee nini? hii aibu kwa nchi

POLENI sana kwa yote hayo. Lakini kwa kiwango kikubwa uwepo wa TPDF huko Zanzibar ni jambo jema kabisa tena basi msiwe na wasiwasi kabisa. Ni waovu tu wataogopa TPDF, watu wema kamwe hawawezi kuogopa jeshi hilo na ambalo ni la ulinzi wa wananchi. Wale wanaoweka X na kuchoma nyumba za wenzao ndio wataogopa lakini sio wale raia wema.
 
Mambo yanayohusu ulinzi na usalama ni classified, hayapaswi kupewa media attention, vifaru ni silaha za kivita na sio vifaa vya kutunzia usalama, hivyo ukiona vifaru, ujue tayari taarifa za kiintelijensia zimeishawafikia, na wanausalama makini kote dunia, hujipanga kukinga ni bora kuliko tiba, hivyo vifaru huko ni kwa ajili ya tahadhai kabla ya hatari, kuna mambo fulani kuna magaidi fulani wamepanga kufanya ugaidi fulani, hivyo kitendo tuu cha kuviona vifaru na ulinzi ulioimarishwa, hao magaidi, hawataendelea tena kutekeleza nia zao ovu!.

Kwa hayo yanayotokea kwa vile Wanzanzibari wenyewe wapo na wameyakubali, ulitaka wafanye nini?!. Viongozi sio ni kama hawapo, bali kiukweli hawapo kikatiba na kisheria, muda wao ulikwisha asmi November 4, sasa wapo wapo tuu kama hawapo!. Wana dini pia wapo kuwafikisha watu mbinguni na sio kuwaingiza magaidi ikulu!, taasisi za kiraia zipo kufanya kazi za kiaia na sio kuingilia mambo ya siasa!, taasisi za haki za binadamu zipo na zinasubiri malalamiko yoyote rasmi kuhusu ukiukwaji wa haki za binaadamu, na hakuna malalamiko yoyote so far!, hii inamaanisha watu wote wameridhika na yote yanayotendwa!. Taasisisi za kisheria pia zipo, taratibu za taasisi zozote za kisheria ni kwa watu wenye malalamiko yoyote ya kisheria kuzifuata kuomba msaada wa kisheria, lakini kwa yote yanayotokea Zanzibar, hakuna yoyote aliyechukua hatua yoyote kulalamika popote, hivyo ulitegemea taasisi hizo zifanye nini?!, yaani daktari atoke hospitalini aanze kutembelea majumbani kuulizia wagonjwa?!, kikawaida kama mahali kuna mgonjwa, mgonjwa huyo ndie atakwenda hospitali kufuata tiba na sii vinginevyo!. Vyama vya siasa ndio kabisa, vipo kama havipo kwa sababu wao ndio waathirika wakuu, sheria taratibu na kanuni wanazijua, hawakufanya lolote zaidi ya kuitisha press conference na kupiga mikelele tuu, unategemea nini?!.

Usalama kwanza, mengine yote baadae!.

Pasco
Vifaru havijawahi kua njia salama ya kuleta amani popote pale duniani.
 
Jamani tuwe wakweli. Hivi hili figisu kalianzisha nani? Hebu kwanza naomba mtafakari haya matokeo yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kutoka majimbo 31 kati ya 54 wakati wakiendelea kupokea mengine[Matokeo hayo yaliyokuwa yametangazwa kufikia saa mbili jioni Oktoba 27 ni kama ifuatavyo:
Matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Zanzibar (Majimbo31/54)]

Jina Chama Kura Asilimia
Khamis Iddi Lila ACT-W 189 0.1
Juma Ali Khatib ADA-TADEA 93 0.0
Hamad Rashid Mohamed ADC 252 0.1
Said Soud Said AFP 223 0.1
Ali Khatib Ali CCK 240 0.1
Ali Mohamed Shein CCM 139,557 57.9
Mohammed Massoud Rashid CHAUMMA 257 0.1
Seif Sharif Hamad CUF 93,699 38.9
Taibu Mussa Juma DM 118 0.0
Abdalla Kombo Khamis DP 86 0.0
Kassim Bakar Aly JAHAZI 227 0.1
Seif Ali Iddi NRA 63 0.0
Issa Mohammed Zonga SAU 127 0.1
Hafidh Hassan Suleiman TLP 107 0.0
Zanzibar ina jumla ya wapiga kura 503,860 waliojiandikisha kupiga kura, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

Halafu twendeni kwenye matokeo aliyotangaza maalim seif
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ameitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema kuwa baada ya chama chake kukusanya fomu zote za matokeo kutoka vituoni, yeye amepata kura 200,007 dhidi ya kura 178,363 za mgombea wa CCM anayetetea nafasi yake, Dk. Ali Mohammed Shein.

Sasa twendeni kwenye tafakuri
1 Tume ilitangaza kuwa wapiga kura wote waliojiandikisha walikuwa 503,860
2. Kwenye majimbo 31 kati ya 54 iliripotiwa kuwa Dr. Shein alipata kura 139,557[57.9%] na Maalim Seif
alipata kura 93,699[38.9]
3 Vyama vingine vidogo vilipata kwa pamoja chini ya asilimia 3 ya kura zote

Alipotangaza ushindi maalim alidai kuwa alipata kura 200,0007 na shein alipata 178,363 hizi hesabu ni kwa zanzibara na pemba.
Hakuna kura zilizoharibika wala kura za vyama vingine

Hivi ndugu zangu hapa ni nani wa kulaumiwa? Hivi mlitaka tume ikubaliane na hesabu za maalimi seif ambazo alidai ni za visiwa vyote 2?

Maoni yangu ni kuwa[naomba msitukane ila mtafakari maana hili ni jamvi la 'those who dare to speak'
Maalim baada ya kuona hali ya matokeo kutoka majimbo 31 hadi tarehe 27 yalionyesha dhahiri kuwa ulikuwepo uwezekano mkubwa kwa chama chake kushindwa na ili afe kiume alipreempt tume kwa kuanza kutangaza yeye wakati akifahamu kuwa kwa sheria zilivyosasa ni tume pekee ambayo inahaki ya kutangaza matokeo.
Ikiwa seif alivunja sheria kwa kujitangazia ushindi adhabu yake ndo iwe kufuta uchaguzi?,imeandikwa wapi kua mgombea urais akijitangazia matokeo adhabu yake ni kufuta uchaguzi.ukweli utakuweka huru
 
Mwenye Jukumu la kuziconfirm hizo rafu ni Jecha pekee kwa dunia nzima....yeye ndiye mwenyekiti wa zec na mwenyekiti wa zec yupo mmoja dunia nzima...
Kwanini asifute miaka yote mpaka asubiri cuf washinde ndo aseme uchaguzi ulikuwa na rafu wakati waangalizi wa uchaguzi wanaona ulikuwa huru na haki
 
Kwanini asifute miaka yote mpaka asubiri cuf washinde ndo aseme uchaguzi ulikuwa na rafu wakati waangalizi wa uchaguzi wanaona ulikuwa huru na haki
Sidhani kama matokeo ya uchaguzi uliopita kuna mamlaka zilitangaza mshindi...
 
Ikiwa seif alivunja sheria kwa kujitangazia ushindi adhabu yake ndo iwe kufuta uchaguzi?,imeandikwa wapi kua mgombea urais akijitangazia matokeo adhabu yake ni kufuta uchaguzi.ukweli utakuweka huru
Adhabu yake ni kifungo au faini au vyote kwa pamoja je unajua ni kwa namna gani amani ingevurugika kama hatua hizo zingefanyika? ilikua busara kufuta, hata mimi nakubali...
 
Hivi wewe ukoje yaani wote wasione rafu isipokuwa jecha pekee?
Unaposema wote unamaanisha nini mkuu? maana kama unanijumuisha na mimi basi inakua sio wote maana tutabaki mimi na jecha...
 
Vifaru havijawahi kua njia salama ya kuleta amani popote pale duniani.
Kama ulinisoma na kunielewa, kazi ya vifaru sio kuleta amani, vifaru viko pale ili kutoa tahadhari kabla ya hatari, yaani ni kinga ambayo ni bora kuliko kinga, hao magaidi kile walichokipanga kukifanya, baada ya kuona vifaru, hawatakifanya tena, na uchaguzi utapita salama!, sasa kama watakuja kuyafanya baada ya uchaguzi, sasa hayo yatakuwa ni mengine, concern kwa sasa ni uchaguzi umalizike salama!.

Pasco
 
Kama ulinisoma na kunielewa, kazi ya vifaru sio kuleta amani, vifaru viko pale ili kutoa tahadhari kabla ya hatari, yaani ni kinga ambayo ni bora kuliko kinga, hao magaidi kile walichokipanga kukifanya, baada ya kuona vifaru, hawatakifanya tena, na uchaguzi utapita salama!, sasa kama watakuja kuyafanya baada ya uchaguzi, sasa hayo yatakuwa ni mengine, concern kwa sasa ni uchaguzi umalizike salama!.

Pasco
Eti "uchaguzi umalizike salama" kwani uchaguzi mkuu wa october haukumalizika salama?iwapo mreno na mkoloni mweupe walifurushwa zanzibar basi elewa na mkoloni mweusi hatobaki salama zanzibar.
 
Back
Top Bottom