Kwanza kuna matukio hayapati nafasi katika vyombo vya habari vingi kuhusu kile kinachoendelea Zanzibar. Zikiwa zimebaki siku sita tu kufanyika kile kinaitwa uchaguzi wa marudio hali ya Zanzibar ni Aibu.
Kwa sasa kumepelekwa vyombo vya ulinzi kwa wingi wakiwemo wanajeshi hasa kisiwani pemba na tayari vyombo hivyo vinaonekana wazi wazi kuleta athari. Kumeripotiwa taarifa za vifaru vya jeshi kuonekana vikitembea barabarani mchana kweupe na wananchi kuingiwa hofu.
Hali hii hujitokeza Zanzibar pekee katika Tanzania hii. Lengo lake halijulikani kama ni huu uchaguzi wa marudio au kuna zaidi ya uchaguzi.
Kuna mpasuko mkubwa wa kijamii. Imefika wakati hasa kisiwani Pemba watu wameshaanza kususiana mambo mbali mbali.
Mifano.
i. Kususiwa baadhi ya wananchi kusafirishwa kwa kivuko kutoka kisiwa kidogo (Kisiwa Panza) kwenda chokocho. Ifahamike mgogoro huu unafukuta na unahusishwa na siasa za uchaguzi wa marudio.
ii Kususiwa kwa baadhi ya mambo ya kijamii ikiwemo maziko na shughuli ya harusi. Maeneo mbali mbali yamejitokeza kwa njia baridi huko Pemba.
iii. Kuna taarifa za viongozi wa kitaifa Zanzibar (Sitaji Majina) kususiwa misikiti zaidi ya mara mbili pale inapopatikana habari kuwa wanakwenda kuswali jamii inasusa kwenda na kuwaachia viongozi wa serikali peke yao. Zipo taarifa ni hapa majuzi kiongozi mmoja alisusiwa ufunguzi wa msikiti hali iliyolazimu kuletwa askari wa kikosi fulani kuongeza idadi ya watu.
iv Kuzomewa baadhi ya viongozi wa kitaifa huko kisiwani Pemba na kususiwa kwenye shughuli za
maendeleo
Kwa ufupi kuna hali mbaya Zanzibar imeanza kujitokeza na inatarajiwa kukua na kuongeza uhasama zaidi. Watu wameanza kuchoma nyumba moto na baraza za vyama vya siasa.
Kuna hali ya kutiliana mashaka na ukimya wa kutisha unaoashiria shari, kuna kutishana kwa kutumia vyombo vya dola. Kumeanza kupigwa marufuku mikusanyiko katika baadhi ya maeneo Zanzibar.
Kuna masuali ya kujiuliza Nini hatima ya Zanzibar ikiwa hali iko hivi sasa kabla ya kufanyika uchaguzi wa marudio uliosusiwa na wadau wakubwa wa Zanzibar? jee Kutakuwa na suluhu yoyote?
Haya yanatokea viongozi ni kama hawapo, wana dini ni kama hawapo, taasisi za kiraia ni kama hazipo, taasisi za haki za binadamu ni kama hazipo, taasisisi za kisheria ni kama hazipo, vyama vya siasa ni kama havipo na wengineo.
Tutegemee nini? hii aibu kwa nchi