Yaniuwia vigumu kukaa kimya napoitazama Zanzibar ya leo. Kuna hali ya kibaguzi kwa baadhi ya Viongozi wa vyama vya Siasa na Serikali ya Zanzibar ambao kama kwamba bado wanaishi karne ya 15.
Nasema haya kwa sababu sielewi sababu ya wao kusifia Utawala wa kifalme wa Sultan kama kwamba Zanzibar hii imepoteza mwelekeo! Kipi kipo nyuma ya Siasa hizi na kwa nini sasa?
Kibaya zaidi maneno haya yanatolewa mitandaoni na Viongozi wa ACT Wazalendo chama kinachojinasibisha na UJAMAA. Huu Ujamaa wao unahusiana vipi kiitikadi na Ufalme wa Oman? ama hii ACT Wazalendo ni ufufuo wa chama cha Hizbu ambacho kilivunjwa baada ya Mapinduzi?
Wako wapi viongozi wa ASP na Baraza la Mapinduzi? au wao pia wamejitosa bora kuishi karne ya 15 kama jamaa zetu wa huko South Afrika ambao wamesahau kabisa jitihada ya kuikomboa nchi yao kutoka kwa Wakoloni Makaburu?
Mimi sii mtabiri, lakini naiona Zanzibar itakuja kuwa nchi ya Unaguzi kuchukia Wageni ilihali Zanzibar inategemea sana Utalii kwa Uchimi wake, Isifike mahala wakasema hata hao Watalii ngozi nyeusi hawatakiwi kuja Zanzibar!
Haya ni maoni yangu binafsi ni mtazamo wangu kufuatia mambo yanayopiganiwa na baadhi ya Wanasiasa na Viongozi wa Zanzibar..
Maasalaam