Wiyelelee
JF-Expert Member
- Nov 9, 2012
- 1,071
- 347
Wana JF,
Kuna thread nyingi sana humu ambazo wanawake wamedai wanawapenda wanaume wenye pesa, magari and kupenda kuolewa na mwanaume ambaye ana nyumba, tena sio hiyo ya pale Gongolamboto au Vingunguti au hapo Mbagala mwisho wa upepo! Wanapenda nyumba iwe Mbezi, Mikocheni au maeneo ya huko Tegeta! Sawa utampata!
Wanaume nasi tunapenda mteremko ati! Eti na sisi tunataka mwanamke awe na ki vitz kwa ajili ya kudandia kila siku!
Lakini, mimi kwa uzoefu wangu nimegungua kwamba kumbe interests ambazo zimeoana au zinafanana (or hobbies) ni muhimu sana katika kudumisha mapenzi. Mfano, iwapo unaoa au unauhusiano na mwanamke ambae hapendi kusoma novels, au magazines, inakuwia taabu sana pale ambapo unasoma na yeye anamangamanga macho tu! Mara nyingi utamskia akilalamika kwamba "We nawe, uko busy kama unachukua PhD?
Pia, mfano unapenda kutoka, na unakuwa na mwanamke/mwanaume ambe yeye akitoka ni kwenda Disco tu. Ukimpeleka beach au sehemu nzuri za kupunga upepo huku ukishushia kidogo yeye ananuna! Anataka achezeshe kiuno pale kwa akina Ngwasuma! Sasa hapa mnakuwa hamuendani kabisa. Wengi ambao walioa bila kuangalia iwapo interest zina match hawana furaha katika ndoa zao. Wanarushiana madongo kwamba " Mama au Baba fulani ni mshamba!"
Chukulia kama mke/mme anaimba kwaya na mmojapo kanisani ni kituo cha Polisi, ataona faida gani ya kuwa nawe karibu? Sasa tusikumbuke haya pale ambapo maji yamemwagika, wengine tuliochemka tuzidi kuvumilia haya maji ya moto la sivyo labda ni kujitafutia ka air conditioner kakupoza kidogo! ....
Hivyo sio vizuri kuangalia material tu maana hayatakuwa na maana kama interests zenu zina differ! Mwezenu juzi ndo nimemuona ambaye kweli angekuwa suitor wangu kiukweli. Ana interest zangu zoooote! Sasa imenibidi mdomo uwe zege, nikaishia kujing'ata na kumeza mate!
Asalaam aleikum.