Kina mama wa CCM walivyogalagala chini mbele ya Waziri Mkuu na Bw. Kinana!!

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,252
113,645

View: https://youtu.be/ldflyzj-0S4?si=KSG3nRgnKOUhTRrM

CCM wenye akili kidogo ndo wanapenda mambo kama haya sasa - kuongoza watu walio wajinga na wapumbavu.

Ni vigumu sana kwa mtu mwenye akili zake timamu, mwenye busara na hekima tu za kawaida, kufanya upumbavu wa kugalagala chini mbele ya viongozi.

Na ithibati ya kuthibitisha kwamba hao viongozi wachache wa CCM walio na vijiakili kidogo kuwa wanapenda kuona mambo kama hayo toka kwa watu wanaowaongoza, ni ukimya wao dhidi ya huo upumbavu.

Mtu mwenye akili akiona watu wapumbavu na walio wajinga wakifanya mambo ya kipumbavu na kijinga, ana wajibu wa kimaadili wa kuyakemea na kuyapinga na kutoa fundisho kuwa hayo mambo si sawa.

Kwa vile haya mambo yanajirudia rudia sana, nashawishika kabisa kuamini kuwa viongozi wa CCM wanayapenda.

Wangekuwa wanayapinga, yasingekuwa yanajirudia rudia sehemu mbalimbali nchini.

CCM ni janga kwa mustakabali wa nchi.

Lakini janga kubwa zaidi ni idadi ya watu walio wajinga na walio wapumbavu.
 
Tanzania ina makabila mengi na kila mahali wana namna zao za kuonesha furaha au kuwapokea viongozi wao.

Mikoa mingine huwezi kuta mambo kama hayo.

Hivyo wanavyofanya haimaanishi kuwa ni wajinga.

Hapana ni tamaduni.

Mwaka Jana nilikua pale ndanda, nilikua nacheka tu maana kila kitu jamaa wanasema nashukulu, nakushukulu.

Ifahamu nchi yako.
 
you get it wrong bra, ni swala la namba tu hata mimi naweza kugalala na hata kulia na kuruka ruka kwenye miti kama nyani kama dau ni kubwa, hivyo hapo walio immoral ni hao politburo wa CCM waliotayari kuudhalilisha utu na heshima ya mwanamke lkn siyo hao akina mama kwani wanafamilia za kulisha pia, hakuna anayeza kufanya hivyo bure hata hao wamama wanalijua hilo …
 
Back
Top Bottom