Kina dada, kwani kuolewa ni lazima?

Kina dada, kwani kuolewa ni lazima?

Kweli tuko hili ni janga la kitaifa....ila kuolewa sio lazima kila mtu na maisha yake.ila hapa bongo usipoolewa bana ooohhh cha moto utakiona hasa hawa mrs fulani bwana wakimuona mdada wa watu msingle lady, basi roho inakuruka,, oo huyu malaya kazi yake kutafuta waume za watu, hana mbele wala nyuma, hajatulia, yani sijui nani atamuoa na maneno kibao,, alikuambia anataka kuolewa? Kama sio umbea,, wewe kabla ya kuolewa hukuwa single lady? Huyo mumeo ulimtengeneza mwenyewe au na yeye alikuwa wa fulani, basi tu kaona unamfaa sana ndo akaamua kukuchukua muishi maisha yenu? Basi ndo mtoto wa kike jiamini, muache single lady wa watu na maisha yake, malaya yeye, anataka wa ume za watu yeye, inakuhusu nini? Wewe mumeo si unaye ndani si umfanye asiende bar, si umfanya asiwe na hao single lady? Sio vizuri kabisa, wewe kupata mume usifikiri kila mtu ana hobie ya kuolewa, mume bongooo!!!!!!!11

Mhhh kama si maneno ya mkosaji basi uko sahihi kabisa
 
wadau nimekuwa nikisikia ya kwamba msichana akiwa ameshafika miaka 25 au na zaidi lakini akiwa bado hajaolewa mara nyingi huwa anakuwa ni mtu mwenye wa kuwaza sana juu ya swala la yeye kuolewa. je hili jambo lina ukweli?
 
Kwani wewe ni me/ke?

Kwani na wewe umefikisha miaka 25?

Na kama umefikisha, umekuwa mtu wa kuwaza kuoa au kuolewa?

Jibu hayo maswali kwanza kisha nitarudi kukupa details kama nitaridhika na majibu yako.
 
Mbona hali kama hiyo haijamtokea Bi. Kiroboto bado?
 
Mbona mie na miaka 24 na nawaza sana kuoa??
Hata wanaume pia inatugusa
 
miaka 25 mtu si upo shule unafanya masters unawazaje kuolewa tena
 
miaka 25 mtu si upo shule unafanya masters unawazaje kuolewa tena

nani kagundanganya kuwa ukiwa chuo huwezi kuolewa? Watu wanazaa na chuo unaendelea kama kawa baada ya kumaliza kinachofuata ni kula bata tu na familia yako uku mkiwa bado vinaja sio unakuja kuzaa na miaka 35 au 40 mwanao badala akuite mama atakuita bibi sasa lol!
 
haa wapi mie nawaza salalio tu cjui nina homon za kiume????totally 90%ya maisha yangu ni vp nitoke kimaisha bila kuwa tegemezi
 
Inawezekana ikawa ni kweli kwa theory kwamba hata vyuoni nako mtoto wa kike akimpata mwanaume aliyeko serious soon anategesha mimba. Ukweli unajulikana .

Pia ukumbuke familia hii ya wanawake wa jamii forum ni ile walikuwa kwenye misingi ya kupewa nasaha na fursa kuwa mwanamke anaweza akajitegemea (Baadhi yao ) na wakaitumia vyema nafasi walizopata , ndio maana unawaona humu kwenye mitandao ya jamii wakiwa na mawazo na fikra chanya zenye mashiko sambamba na baadhi ya wanaume .

Jamii hii sio reference sahihi kwa mtazamo wangu katika kuwasilisha mawazo jinsi gani wanawake wananyanyasika na mfumo dume kwa baadhi ya makabila ,kwani hawapitia uhalisia wa ushenzi wanaofanyiwa wanawake huko vijijini (Wachache sana wanaweza wakawa good reference ).Mila na desturi zetu ndizo chanzao mambo kama hayo ,zipo fikra kuwa mwanamke ni mtu dhaifu hivyo lazima aolewe ndipo jamii itamwona amekamilika. Ila si kweli kwani mazingira ya sasa sio kama ya zamani ,tamaduni zinaingiliana sana kiasi kwamba tafsiri ya ndoa inatofautiana baina ya watu wawili wanaooana (Hapo ndio mtafaruku unapoanzaga ). Hivyo wanawake walio na uwezo wa kujua mbivu na mbichi ndoa sio priority kwao .

Ni hayo machache ,sorry kama nimetoka nje ya mada kidogo .
 
Back
Top Bottom