Kimya Hiki, Is Not Right!, There Must Be Something Wrong Somewhere! Or Am, I Wrong!?

Kimya Hiki, Is Not Right!, There Must Be Something Wrong Somewhere! Or Am, I Wrong!?

Heri tu akae kimya maana si ajabu akiongea ataanza kulaumu kuna watu wamesababisha tetemeko na hivyo atahakikisha amewashughulikia kwa nguvu zake zote!
 
Mambo yakizidi mtu inabidi afanye meditation. Yawezekana kuna novena inafanyika au kuna mfungo fulani kuombea nchi yetu.
 
Mkuu ukiunganisha Dot......bandarini.......Dot..........
Maisha ya watu kuwa magumu .....ukaongezea kuwatukana wafanya biashara alafu janga limekuja ndio inabidi wakuchangie .................
Hata kama ningekuwa Mimi ningekaa kimya !!!
 
Ni heri pia akae kimya maana akizungumza ataanza kuwalaumu na kuwasimanga watoa huduma mbalimbali wanaohangaika usiku na mchana kuhudumia wahanga wa tetemeko
 
Atasema nini huko ikiwa kule Mwakata Kahama aliwaambia kuwa hatawapatia msaada wowote ule uliokuwa umeahidiwa na mtangulizi wake, sasa ili kuonekana haegemei upande inabidi akae kimya
 
Huu sasa ndio ushirikina, kumbe mmesha mstopisha mkulu.... hamtafanikiwa uzima moto wa mafuta kwa maji!
Kuna hadithi flani inazungumzia maisha ya mzee mbabe na mchawi katika kijiji flani......

"Mzee huyo alikuwa ni mbabe na mpenda sifa na alijiita MTUKUFU jambo ambalo ni kufuru kwa imani ya watu wa kijiji hicho, kwani watu hao waliamini kuwa jina MTUKUFU ni maalumu kwa Mungu wao tu.
Basi wale wanakijiji waliamua kumuomba Mungu wao ashushe adhabu kwa huyu anayemdhihaki.
Siku moja mvua kubwa na radi ya kutisha ilishuka kwenye kijiji hicho. Mvua na radi ile ilikuwa na madhara makubwa kwenye maisha na mali za wanakijiji hao.
Cha kushangaza ni miezi kadha na kadha kupitia bila yule Mzee mbabe na mchawi kuonekana wala sauti yake kusikika.
Siku moja ikaja bainika kuwa mzee huyo mbabe alikuwa amepatwa na Ugonjwa usiofahamika uliomfanya alale tu, kwani viuongo vyote vya mwili vilisimama kufanya kazi.
Kumbe ile mvua na radi zile ilikuwa ni adhabu iliyoshushwa na Mungu wa wale wanakijiji dhidi ya yule mzee mbabe na mchawi."

Mtanisamehe GT wote, kwa kuwapotezea muda kuisoma hadithi hii isiyohusiana na chochote kwenye mada hii.
 
Update
Wanabodi, hatimaye kimya kimerushwa na neno limesemwa ila sio tuu na roho zetu zimeponywa bali nimejiridhisha pasi shaka kuwa Mhe. Rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli anasoma jf, kwenye mazungumzo yake nimemsikia akizijibu hoja za jf kiaina, hivyo wana JF, tuitumie jf more responsibly tukitaka kumfikishie ujumbe rais, unapost tuu humu jf na rais anasoma na majibu utayapata kama mimi nilivyomsikia kwa masikio yangu mwenyewe jinsi akijibu hoja za jf! .
Naomba kuchukua fursa hii kuushukuru uongozi wa JF ambao umetoa hadi a direct access kumwambia chochote rais wetu na akatujibu.

Pasco
 
Nilikuwa na mashaka na kimya hiki maana binadamu tuna changamoto nyingi sana kiroho,kimwili na kiakili.Afya ni maisha na maisha ni afya.....
 
Back
Top Bottom