Kimya Hiki, Is Not Right!, There Must Be Something Wrong Somewhere! Or Am, I Wrong!?

Kimya Hiki, Is Not Right!, There Must Be Something Wrong Somewhere! Or Am, I Wrong!?

Janga la tetemeko ni la kustukiza sana, inawezekana kuna mambo anayafuatilia kimya kimya kuhusiana na mapokezi ya janga kama hili haswa kwa vikosi husika vinavyopaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanaathirika wanafarijika. Vinginevyo tusubiri kujulishwa.
 
Bila shaka nilisikia mtendaji mkuu wa shughuli zote za serikali alifika kwenye tukio husika ingawa sina uhakika Kama alitoa tamko lolote kwa wahanga.

Huu ukimya inawezekana ukawa unakuja na kitu kizuri kwa wahanga au kukawa kuna kitu kimeenda ndivyo sivyo.

Hakika wote hapa hatujui anachofikiria kwa kwa wakati huu. Cha msingi tuwe na subira huenda anajipanga aje.

Ingawa wakati mwingine subira huponza sana na ukiangalia wahanga wapo katika hatari kubwa sana.
 
Kuapishwa sio lazima picha ziwepo bana,mkuu yuko salama salimini anachapa kazi kama kawaida
 
Huu ni ochonganishi, Yule ni kiongozi wa taasisi muhimu inchini na chini yake wako watendaji wengi, majanga na ajali nchi hii hayajaanza jana wala leo, tumeona ajali na majanga ya mafuriko, tumeona ajali za Sepide etc, hapa naona mnatafuta lawama kwa kuwa tukio limetokea kanda ile ili badaye mseme, Mods naomba mfute Uzi huu.
Kwani ni kiongozi gani unaye mzungumzia ndugu yangu GT?
 
Siye wa darasa la pili tumeshafikiria labda sababu tulichagua wapinzani ambao kiafrika wanaitwa VIBARAKA,kwa hiyo ndiyo tunasomeshwa number.

Halafu tunanyooka maana hii baridi na mvua za baada ya Tetemeko si mchezo.Mbaya zaidi vile vibranketi tulivyopewa na Kibaraka mkuu wetu vimenyang'anywa ni shida,bora umeuliza labda Mzee wetu Mtukufu kabisa atakujibu
 
Huu ni ochonganishi, Yule ni kiongozi wa taasisi muhimu inchini na chini yake wako watendaji wengi, majanga na ajali nchi hii hayajaanza jana wala leo, tumeona ajali na majanga ya mafuriko, tumeona ajali za Sepide etc, hapa naona mnatafuta lawama kwa kuwa tukio limetokea kanda ile ili badaye mseme, Mods naomba mfute Uzi huu.
ifutwe ili ?tulia ikuingie
 
Uso umeumbwa na aibu kina Ruge mzee wa Escrow ndio wenye uwezo wa kuiponya Bukoba ndani ya dakika tu lakini umeshatangaza unataka waishi kama mashetani.

Mabalozi waliambiwa wasiingilie mambo ya ndani wanashangaa wameitwa jumba jeupe kuombwa msaada baba mwenye nyumba haonekani, na mkumbuke wenzetu wazungu ni watu wa kukeep record, bado wana kumbukumbu na walimsikia Baba mtukufu akitamba Tanzania hatutaki misaada, je hata wewe Pasco utaanza vipi kuwaface watu kama hao uliowatambia?

Maskini hana kiapo na Shabaan Robert alituhasa tuweke akiba ya maneno.

Yale mapesa ya MCC zaidi ya dollar millioni 800 tuliyapiga teke leo kumfuata mzungu kumuomba msaada inaweza kusababisha waanzishe research center ya kuzifanyia research akili zetu.

Cha msingi tuendelee kumuombea tu.
 
Waziri mkuu si alishawakilisha Kagera? ikumbukwe Tanzania ina majanga kila siku tena ni mengi mno. sasa huo ukimya mnao question mngependa mtu ajigawanye mara ngapi? jipe mfano wewe na familia yako, ni mara ngapi mmeweza kuwepo kwenye tukio wote kwa pamoja iwe msiba, sherehe, kuona mgonjwa N.K? mimi nahisi Pasco unalo unalolitafuta au unalo unalojua na kama unalo unalojua basi kufwa free ku share nasi. After all sharing is caring. Sambaza upendo mkuu.
Kama ndivyo hivyo... basi asingekatisha ziara ya kukutana na wenzake Lusaka. Angeenda kwa amani kulitumikia taifa.

Kuahirisha safari kwa sababu ya maafa... afu bado kimya kikatawala hili ndo linapasua kichwa kwenye huu mjadala.

Kwanini kimya kwenye janga la kitaifa? Kuna tatizo??
 
Back
Top Bottom