Matumizi mabaya ya Sheria ya Ardhi

Matumizi mabaya ya Sheria ya Ardhi

NANCA

Member
Joined
Jun 23, 2023
Posts
92
Reaction score
100
  • Leo hii napoandika hapa eneo langu la ardhi lililopo karibu kabisa na halmashauri limekuja kupimwa ili kuweza kunyakuliwa kwaajili ya kinachosemwa mradi wa serikali
  • Halmashauri ilipima eneo lake ililokua inamiliki ikakata viwanja na ikauzia watu then wanakuja kunyakua eneo langu ili kuanzisha shule, je kwann ktk maeneo waliyouzia watu wasingetenga eneo la shule
  • Wakati mimi na wengine wanyonge tunawekwa ktk mpango wa kunyakuliwa maeneo yetu, pembeni yetu kuna eneo kuuubwa la mbunge, kwann wasingenyakua huko?
  • Wakati wanaendelea na harakati zao za unyakuzi bado kuna maeneo mengine ya Kijiji/ halmashauri yapo wazi na wangeweza kujenga shule yao.
  • Hivi niulize ni sisi wanyonge ndo hatuna haki ya kumiliki maeneo mazurimazuri na ya kuvutia? Ni sisi wanyonge ndo tunaofaa kunyakuliwa maeneo yetu? Mbna wakubwa sijasikia hata siku moja maeneo yeo yakinyakuliwa, ukiondoa awamu ya tano
-Hivi wabunge, na viongozi wakubwa wa kiserikali ndo wenye haki ya kumiliki maeneo ya kuvutia ila sisi tukionekana tunamiliki maeneo hayo basi mnaleta mradi wa kutuondoa.

- Hivi hii nchi ni ya nani, ni nyinyi tulowachagua au sisi? Mbana mnajipendelea wenyewe?

-Hivi sheria ya ardhi na unyakuzi imeeekwa ili nyie wenye nguvu ndo mtukomoe sisi wanyonge?
  • Je watoto wetu hawana haki ya kuandaliwa maeneo mazuri mazuri ya kuvutia ila nyie wabunge, mawaziri na marais wa nchi hii ya Tanzania ndo wenye haki ya kuandaa maisha bora ya watoto wenu kwa kuwaandalia ardhi nzuri?
  • Mwisho niseme tu kua vita vyangu vimeanza na kahuri langu nshalichimba niko tayari kupigana vita vya kutetea ardhi yangu kwa maslahi ya vizazi vyangu. Nilikopa, nkajinyima na nkannua ardhi heka moja karibu kabisa na mpaka wa halmashauri unapoishia ili njenge maduka na nyumba za makazi kwaajili yangu, familia na watoto wangu ila naona mtu ametumia jina serikali ili kurubuni watu apate maeneo hayo, pia serikali hii ya Rais Samia Suluhu hasani imeona ni vyema kunyakua maeneo ya wanyonge na kukwepa maeneo ya mbunge wao. Nipo tayari Sasa kuishia Miaka hii 35 hapa duniani ili kuipambania hatma yangu na vizazi vyangu ktk ardhi hii. Je ngekua mbunge, waziri au rais je mngekuja kunyakua maeneo yangu? Tafadhali tafteni eneo lingine la kujenga hiyo shule ya medium ila sio pahala pangu, mnamaeneo mengi na yanajulikana, acheni kuitumia vibaya sheria ya ardhi.
 
  • Leo hii napoandika hapa eneo langu la ardhi lililopo karibu kabisa na halmashauri limekuja kupimwa ili kuweza a maeneo ya wanyonge na kukwepa maeneo ya mbunge wao. Nipo tayari Sasa kuishia Miaka hii 35 hapa duniani ili kuipambania hatma yangu na vizazi vyangu ktk ardhi hii. Je ngekua mbunge, waziri au rais je mngekuja kunyakua maeneo yangu? Tafadhali tafteni eneo lingine la kujenga hiyo shule ya medium ila sio pahala pangu, mnamaeneo mengi na yanajulikana, acheni kuitumia vibaya sheria ya ardhi.
Survival of the fittest!!!
 
Kisheria ni lazima wakulipe fidia.Halmashauri ya Kijiji/Wilaya ni corporate body so you can sue them
Mfano umejenga tayari na wanataka wakunyang'anye eneo lako, wanakulipa pamoja na nyumba?
 
Kisheria ni lazima wakulipe fidia.Halmashauri ya Kijiji/Wilaya ni corporate body so you can sue them
-Hilo neno fidia linatumika kwa wanyonge tu, ushawai kusikia mbunge au waziri anadai fidia? Hyo sheria ishapitwa na wakati, pia hyo sheria inatumika vibaya na kwa maguvu kupokonya maeneo ya wanyonge. Kuna haja gani kumletea umasikini mwananchi akati bado serikali inamaeneo. Na kwann wasingechukua upande wa mbunge ila wakachagua upande wetu? Kwann kila siku pande za watu wasio na vyeo na mamlaka ndo huchaguliwa kuwekwa miradi ya kijamii?

- Pia nimewaambia fidia ya fedha siitaki nataka fidia ya ardhi yenye ukubwa, dhamani, hadhi na matumizi kama hyo wananiambia hayo ni mambo ya kizamani. Mungu wangu hyu hapa, nipo tayari kufa maana ukihoji tu wanaita polisi. Mchakato unaendeshwa hata haueleweki, pia Kuna fununu kua mbunge hutumia neno serikali ili kunyakua maeneo hayo aweke mradi wake. Hivi sisi na watoto wetu ni mbuzi na nguruwe ktk nchi hii ila wao wenye mamlaka na watu wa serikali ndo hupashwa kulindwa maslahi yao?

Kimsingi nipo ktk mapigano binafsi na ni mkono wa Mungu tu ndo muamuzi, haki za binadam sisi wanyonge hazitiliwi maanani kabisa, watu hao hutumia sheria kutufanya tuzidi kua masikini. Rais, na watu ktk serikali yake huneemeshwa na sheria hizi kandamizi
 
Mkuu, wakati mwingine jifunze hata kunyenyua panga ili kuonyesha kwamba hauwezi ukaruhusu haki na utu wako utwezwe
 
-Hilo neno fidia linatumika kwa wanyonge tu, ushawai kusikia mbunge au waziri anadai fidia? Hyo sheria ishapitwa na wakati, pia hyo sheria inatumika vibaya na kwa maguvu kupokonya maeneo ya wanyonge. Kuna haja gani kumletea aanani kabisa, watu hao hutumia sheria kutufanya tuzidi kua masikini. Rais, na watu ktk serikali yake huneemeshwa na sheria hizi kandamizi
Acha kulalamika hapa,tafuta mwanasheria,peleka kesi mahakamani.
Kama huna ubavu,potezea tu kama umetoa sadaka kanisani au msikitini.
Hii Dunia ni mbwa kala mbwa
 
Kisheria ni lazima wakulipe fidia.Halmashauri ya Kijiji/Wilaya ni corporate body so you can sue them
Hii nchi imekua ni ya waowaowao na wanatumia sheria hizi kutufanya tuwe masikini, humlamua mambo kwa mapenzi yao. Nooo, ktk ile ardhi nimeweka hatma ya maisha ya vizazi vyangu, ktk ardhi ile nimejipanga kuondokana na umasikini, ktk ardhi ile ndo uhai na hatma yangu, kunipokonya ardhi ile kwa kutumia sheria hizi ni kunikatisha uhai wangu, na Sasa nipo tayari. Kwanini kila siku ni sisi tusio na mamlaka na pesa ndo sheria hyo ituguse. Mungu amenipa mimi ardhi ile kwa makusudi hvyo makusudi hayo yatatimia. Nipo tayari kuifia ardhi ile
 
Acha kulalamika hapa,tafuta mwanasheria,peleka kesi mahakamani.
Kama huna ubavu,potezea tu kama umetoa sadaka kanisani au msikitini.
Hii Dunia ni mbwa kala mbwa
Yeyote unaemuona mahakamani basi ujue alilalamika mahala fulani kwanza ndipo baadae sana akaenda mahakamani. Mahakama pia ni mali yao hao wenye mamlaka.
 
Hii nchi imekua ni ya waowaowao na wanatumia sheria hizi kutufanya tuwe masikini, humlamua mambo kwa mapenzi yao. Nooo, ktk ile ardhi nimeweka hatma ya maisha ya vizazi vyangu, ktk ardhi ile nimejipanga kuondokana na umasikini, ktk ardhi ile ndo uhai na hatma yangu, kunipokonya ardhi ile kwa kutumia sheria hizi ni kunikatisha uhai wangu, na Sasa nipo tayari. Kwanini kila siku ni sisi tusio na mamlaka na pesa ndo sheria hyo ituguse. Mungu amenipa mimi ardhi ile kwa makusudi hvyo makusudi hayo yatatimia. Nipo tayari kuifia ardhi ile
Ardhi siyo yako ni ya umma
Muda wowote unaweza kunyang'anywa kama itahitajika kufanya jambo lenye manufaa kwa wengi
Lakini wakikunyang'anya ni lazima wakulipe fidia
 
Wakati mwingine sheria hyo hutumika vibaya. Nadhani unajua juu ya mtawanyo wa huduma za jamii na utaratibu wake ila wenye nguvu wanaweza kujisogezea karibu yao huduma hyo bila wao kuathirika, ndicho kinacho endelea. Huo unakua uonevu na matumizi mabaya ya sheria kwa manufaa binafsi
 
Usiwe mnyonge sana,pambana
Kapige mkwara halmashauri
Waeleze kuhusu fidia na mipango ya kwenda wizarani na mahakamani
 
Sawa, huo ndo ushauri mzuri kwa sisi masikini. Masikini anaefanikiwa nchi hii ni yule mbishi ila sie anelaefuata sheria maana sheria za nchi hii zipo kwaajili ya kumfeva rais, wabungu, mawaziri, other high government officials na wenye pesa nyingi sana. Hivyo siyo suitable kwa sisi wapiga debe
 
Umepigwa wewe
Watumishi wengi wa idara ya Ardhi ni matapel,pambania haki yako,Kama wamechukua eneo lako Sheria inasema ulipwe fidia,komaa ,nenda Hadi takukuru kawaripot uwe na ushahidi .
 
  • Leo hii napoandika hapa eneo langu la ardhi lililopo karibu kabisa na halmashauri limekuja kupimwa ili kuweza kunyakuliwa kwaajili ya kinachosemwa mradi wa serikali
  • Halmashauri ilipima eneo lake ililokua inamiliki ikakata viwanja na ikauzia watu then wanakuja kunyakua eneo langu ili kuanzisha shule, je kwann ktk maeneo waliyouzia watu wasingetenga eneo la shule
  • Wakati mimi na wengine wanyonge tunawekwa ktk mpango wa kunyakuliwa maeneo yetu, pembeni yetu kuna eneo kuuubwa la mbunge, kwann wasingenyakua huko?
  • Wakati wanaendelea na harakati zao za unyakuzi bado kuna maeneo mengine ya Kijiji/ halmashauri yapo wazi na wangeweza kujenga shule yao.
  • Hivi niulize ni sisi wanyonge ndo hatuna haki ya kumiliki maeneo mazurimazuri na ya kuvutia? Ni sisi wanyonge ndo tunaofaa kunyakuliwa maeneo yetu? Mbna wakubwa sijasikia hata siku moja maeneo yeo yakinyakuliwa, ukiondoa awamu ya tano
-Hivi wabunge, na viongozi wakubwa wa kiserikali ndo wenye haki ya kumiliki maeneo ya kuvutia ila sisi tukionekana tunamiliki maeneo hayo basi mnaleta mradi wa kutuondoa.

- Hivi hii nchi ni ya nani, ni nyinyi tulowachagua au sisi? Mbana mnajipendelea wenyewe?

-Hivi sheria ya ardhi na unyakuzi imeeekwa ili nyie wenye nguvu ndo mtukomoe sisi wanyonge?
  • Je watoto wetu hawana haki ya kuandaliwa maeneo mazuri mazuri ya kuvutia ila nyie wabunge, mawaziri na marais wa nchi hii ya Tanzania ndo wenye haki ya kuandaa maisha bora ya watoto wenu kwa kuwaandalia ardhi nzuri?
  • Mwisho niseme tu kua vita vyangu vimeanza na kahuri langu nshalichimba niko tayari kupigana vita vya kutetea ardhi yangu kwa maslahi ya vizazi vyangu. Nilikopa, nkajinyima na nkannua ardhi heka moja karibu kabisa na mpaka wa halmashauri unapoishia ili njenge maduka na nyumba za makazi kwaajili yangu, familia na watoto wangu ila naona mtu ametumia jina serikali ili kurubuni watu apate maeneo hayo, pia serikali hii ya Rais Samia Suluhu hasani imeona ni vyema kunyakua maeneo ya wanyonge na kukwepa maeneo ya mbunge wao. Nipo tayari Sasa kuishia Miaka hii 35 hapa duniani ili kuipambania hatma yangu na vizazi vyangu ktk ardhi hii. Je ngekua mbunge, waziri au rais je mngekuja kunyakua maeneo yangu? Tafadhali tafteni eneo lingine la kujenga hiyo shule ya medium ila sio pahala pangu, mnamaeneo mengi na yanajulikana, acheni kuitumia vibaya sheria ya ardhi.
Mkuu pale inapojidhihirisha kuwa unafanyiwa hujuma ya wazi ili kutaka kuporwa haki yako kwa hila na wenye mamlaka, hupaswi kuishia kulalamika tu.

Kama watawala wameamua kukufanyia hivyo, una njia mbili tu za kufanya, ama uende kuwashtaki kwa Mola wako, la sivyo nenda kafanye hivyo kwa shetani. Chukua hatua mapema ili haki yote pia ipate kutendeka dhidi yao.
 
  • Leo hii napoandika hapa eneo langu la ardhi lililopo karibu kabisa na halmashauri limekuja kupimwa ili kuweza kunyakuliwa kwaajili ya kinachosemwa mradi wa serikali
  • Halmashauri ilipima eneo lake ililokua inamiliki ikakata viwanja na ikauzia watu then wanakuja kunyakua eneo langu ili kuanzisha shule, je kwann ktk maeneo waliyouzia watu wasingetenga eneo la shule
  • Wakati mimi na wengine wanyonge tunawekwa ktk mpango wa kunyakuliwa maeneo yetu, pembeni yetu kuna eneo kuuubwa la mbunge, kwann wasingenyakua huko?
  • Wakati wanaendelea na harakati zao za unyakuzi bado kuna maeneo mengine ya Kijiji/ halmashauri yapo wazi na wangeweza kujenga shule yao.
  • Hivi niulize ni sisi wanyonge ndo hatuna haki ya kumiliki maeneo mazurimazuri na ya kuvutia? Ni sisi wanyonge ndo tunaofaa kunyakuliwa maeneo yetu? Mbna wakubwa sijasikia hata siku moja maeneo yeo yakinyakuliwa, ukiondoa awamu ya tano
-Hivi wabunge, na viongozi wakubwa wa kiserikali ndo wenye haki ya kumiliki maeneo ya kuvutia ila sisi tukionekana tunamiliki maeneo hayo basi mnaleta mradi wa kutuondoa.

- Hivi hii nchi ni ya nani, ni nyinyi tulowachagua au sisi? Mbana mnajipendelea wenyewe?

-Hivi sheria ya ardhi na unyakuzi imeeekwa ili nyie wenye nguvu ndo mtukomoe sisi wanyonge?
  • Je watoto wetu hawana haki ya kuandaliwa maeneo mazuri mazuri ya kuvutia ila nyie wabunge, mawaziri na marais wa nchi hii ya Tanzania ndo wenye haki ya kuandaa maisha bora ya watoto wenu kwa kuwaandalia ardhi nzuri?
  • Mwisho niseme tu kua vita vyangu vimeanza na kahuri langu nshalichimba niko tayari kupigana vita vya kutetea ardhi yangu kwa maslahi ya vizazi vyangu. Nilikopa, nkajinyima na nkannua ardhi heka moja karibu kabisa na mpaka wa halmashauri unapoishia ili njenge maduka na nyumba za makazi kwaajili yangu, familia na watoto wangu ila naona mtu ametumia jina serikali ili kurubuni watu apate maeneo hayo, pia serikali hii ya Rais Samia Suluhu hasani imeona ni vyema kunyakua maeneo ya wanyonge na kukwepa maeneo ya mbunge wao. Nipo tayari Sasa kuishia Miaka hii 35 hapa duniani ili kuipambania hatma yangu na vizazi vyangu ktk ardhi hii. Je ngekua mbunge, waziri au rais je mngekuja kunyakua maeneo yangu? Tafadhali tafteni eneo lingine la kujenga hiyo shule ya medium ila sio pahala pangu, mnamaeneo mengi na yanajulikana, acheni kuitumia vibaya sheria ya ardhi.
Kwanza nakuunga mkono, haki haiombwi wala huletewi kwenye kisahani cha chai, haki inapiganiwa!.

Pili hiyo ni njama tuu ya mtu kutumia mgongo wa halmashauri, serikali haitengi wala kutwaa maeneo ya kujenga private entity kama school ya English Medium!, sheria ya ardhi ya Vijiji inasema ardhi inaweza kutwaliwa kwa ujenzi wa public entities kama Shule, Hospital, solo, uwanja, ofisi ya umma, au kutenga eneo la uwekezaji SEZ, lakini eneo la kujenga private school, huyo mtu akatafute eneo anunue!.

P
 
  • Leo hii napoandika hapa eneo langu la ardhi lililopo karibu kabisa na halmashauri limekuja kupimwa ili kuweza kunyakuliwa kwaajili ya kinachosemwa mradi wa serikali
  • Halmashauri ilipima eneo lake ililokua inamiliki ikakata viwanja na ikauzia watu then wanakuja kunyakua eneo langu ili kuanzisha shule, je kwann ktk maeneo waliyouzia watu wasingetenga eneo la shule
  • Wakati mimi na wengine wanyonge tunawekwa ktk mpango wa kunyakuliwa maeneo yetu, pembeni yetu kuna eneo kuuubwa la mbunge, kwann wasingenyakua huko?
  • Wakati wanaendelea na harakati zao za unyakuzi bado kuna maeneo mengine ya Kijiji/ halmashauri yapo wazi na wangeweza kujenga shule yao.
  • Hivi niulize ni sisi wanyonge ndo hatuna haki ya kumiliki maeneo mazurimazuri na ya kuvutia? Ni sisi wanyonge ndo tunaofaa kunyakuliwa maeneo yetu? Mbna wakubwa sijasikia hata siku moja maeneo yeo yakinyakuliwa, ukiondoa awamu ya tano
-Hivi wabunge, na viongozi wakubwa wa kiserikali ndo wenye haki ya kumiliki maeneo ya kuvutia ila sisi tukionekana tunamiliki maeneo hayo basi mnaleta mradi wa kutuondoa.

- Hivi hii nchi ni ya nani, ni nyinyi tulowachagua au sisi? Mbana mnajipendelea wenyewe?

-Hivi sheria ya ardhi na unyakuzi imeeekwa ili nyie wenye nguvu ndo mtukomoe sisi wanyonge?
  • Je watoto wetu hawana haki ya kuandaliwa maeneo mazuri mazuri ya kuvutia ila nyie wabunge, mawaziri na marais wa nchi hii ya Tanzania ndo wenye haki ya kuandaa maisha bora ya watoto wenu kwa kuwaandalia ardhi nzuri?
  • Mwisho niseme tu kua vita vyangu vimeanza na kahuri langu nshalichimba niko tayari kupigana vita vya kutetea ardhi yangu kwa maslahi ya vizazi vyangu. Nilikopa, nkajinyima na nkannua ardhi heka moja karibu kabisa na mpaka wa halmashauri unapoishia ili njenge maduka na nyumba za makazi kwaajili yangu, familia na watoto wangu ila naona mtu ametumia jina serikali ili kurubuni watu apate maeneo hayo, pia serikali hii ya Rais Samia Suluhu hasani imeona ni vyema kunyakua maeneo ya wanyonge na kukwepa maeneo ya mbunge wao. Nipo tayari Sasa kuishia Miaka hii 35 hapa duniani ili kuipambania hatma yangu na vizazi vyangu ktk ardhi hii. Je ngekua mbunge, waziri au rais je mngekuja kunyakua maeneo yangu? Tafadhali tafteni eneo lingine la kujenga hiyo shule ya medium ila sio pahala pangu, mnamaeneo mengi na yanajulikana, acheni kuitumia vibaya sheria ya ardhi.
Unayo TP Drawing ya eneo lako? Mchoro ulitayarishwa lini?
Ulihusishwa? Kama hukuhusishwa na Hamna kikao/mkutano uliofanyika na minutes zake basi ni kosa lao.
Ardhi yako imepimwa? Kama imepimwa, basi Ile hela unayolipia Kodi ndiyo itathaminisha ardhi yako na valuer mtafute anayetambulika ili afanye valuation ya nyumba yako.
Ikiwezekana, uwe na mbuzi, ng'ombe hata kuku wa kienyeji ili uongeze thamani ya ardhi yako ambayo haipo covered na jengo.

Valuer atairhaminsha zaidi kwa sababu ni source ya malisho na habitation ya mifugo yako.
Pia mifugo yako ilipiwe hela kwa sababu wakitwaa ardhi hutakuwa na sehemu labda ukodi kabla ya kusettle.
Wakikuona unajua haki zako watatwaa kwa mwingine,.
But make sure you get a lot of money.
 
Acha kulalamika hapa,tafuta mwanasheria,peleka kesi mahakamani.
Kama huna ubavu,potezea tu kama umetoa sadaka kanisani au msikitini.
Hii Dunia ni mbwa kala mbwa
Wanasheria nao ni waongo, wahuni and to crown it all most of YOU (including you, may be) are shyster lawyers! Lakini umempa ushauri mzuri ....
 
Back
Top Bottom