Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 5,738
- 15,211
Spika Job Ndugai amehoji tatizo la kukatika kwa umeme nchini na kuitaka kamati ya nishati kukutana haraka na bodi ya mpya ya Tanesco ili kuwaeleza kazi kubwa iliyoko mbele yao.
Sakata hilo liliibuliwa na mbunge wa Kilombero mh Abukary Assenga aliyetaka kujua ni kwa nini Tanesco wanakata umeme kila jumanne na Alhamis jimboni kwake.
----
Licha kukiri kuwepo kwa adha ya kukatika kwa umeme kwa mara nyingi nchini, lakini Serikali mesema hakuna mgawo wa umeme Tanzania.
Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato ameliambia Bunge leo kuwa, hakuna mgawo wowote wa umeme nchini kwa sasa.
Hata hivyo Spika Job Ndugai ameagiza kamati ya Nishati na Madini wakutane haraka na Wizara hiyo na Bodi mpya ya Nishati ili wajue ukubwa wa kazi iliyo mbele yao maana kukatika kwa umeme ni tatizo nchini.
Awali mbunge wa Kilombero, Abubakar Asenga alitaka Wizara kueleza sababu za msingi ni kwa nini umeme katika wilaya hiyo unakatwa siku za Jumanne na Alhamisi na kusababisha adha kubwa.
Mbunge wa Sengerema Hamisi Tabasamu amedai katika jimbo lake umeme hukatika mara 10 hadi 30 kwa siku bila kujua sababu za msingi na akaomba waunganishwe na umeme kutoka laini ya Geita.
Chanzo: Mwananchi