Kimeumana Bungeni! Spika Ndugai ahoji kama kuna mgao wa umeme nchini

Hii nayo ni habari??

Mlitaka muwe na bunge la kijani sasa mnalo halina mvuto kabisa!

Sasa ni kuunga unga vihabari uchwara ili ionekane mpo binafsi sikua najua kama hicho kikao CCM NEC kimeanza
 
Hakuna Tanesco anayeihujumu serikali wewe, usiwasikilize hao kina Makamba na stori zao...

Nchi hii wanaokula nchi ni viongozi na michongo yao, huo unaoona mgao unakuta ni watu wanataka kuuza dizeli na majenereta...

Jaribu tu kufikiria hii nchi ina minara mingapi ya simu, fanya robo tatu ya minara yote nchini ina Diesel Generators, na hizo DG's ili zitembee zinahitaji diesel...na tanks za DG za minara kwa wastani huingiza lita 500 ambazo hulast within a month tu...

Ukiacha hilo, hiyo Tanesco ina madeni chungu nzima yaliyosababishwa na hao hao wanaohoji kukatika kwa umeme huko bungeni kutokana na mamikataba ya kiduanzi...
Nakuunga mkono, huyu waziri anavisingizio vingini visivyo na mantiki yoyote.

Suala ni kwamba mtoto wa 'elites' hakosei, kapelekwa pale kwa mbereko za baba yake ili kufanikisha biashara zao.

Eti anahujumiwa, wakati anaingia na mbwembwe za kufukuza aliowakuta kwa kuwatweza alifikiri ana akili sana na kwamba hakujua kwamba tangu 2016-Machi 2021 umeme haukuwahi kukaktika kijinga bila taarifa zozote?

Hakuna anayehujumu chochote isipokuwa jwamewekwa pale wasio na weledi wa kazi zaidi ya kuchimbua ni kwanini waliokuwepo walikuwa wanafanikiwa wameshindwa kupata jibu.

Huyo waziri aondoke kama hataki kjiuzulu basi asubiri kulengeshwa kwenye kashfa ambayo atajuta ni kwanini alikubali kupokea jukumu asiloliweza. Ukiingiza siasa kwenye kazi huwezi kufanikiwa kamwe
 
Anaulizwa kwa Nini umeme unakatikakatika anajibu ni kutokana na sababu mbalimbali hakika pengo linaonekana
 
Hakuna wizara iliyoongozwa na January ikafanikiwa, huyu dogo anachojua ni kutengeneza michongo ya kupiga tu.
Toka aingie ameshindwa kabisa kutembelea miradi ya kimkakati ya umeme. Ye kabakia kusafiri tu nje maana alizimiss sana hizo safari. Hapo wanatafuta pesa za kuhonga wapiga kura na uchaguzi kuelekea 2025.

Wateuzi wa mama wote ni base ya 2025..sii kupiga kazi.
 
TANESCO inapaswa ifumuliwe yote, inaonekana baadhi ya watumishi wa Tanesco wanaihujumu Serikali, hivyo waziri na watendaji wake watupie jicho kila kona ya Tanesco
Waziri mwenyewe jipu. Badala ya kutembelea miradi ya umeme anatembelea arabuni.
 
Anaulizwa kwa Nini umeme unakatikakatika anajibu ni kutokana na sababu mbalimbali hakika pengo linaonekana
Ww ulitaka akujibu vipi ? Ulitaka uambiwe mtambo mbovu pengo gani wakati NW Byabato alikuwepo tangia enzi za hayati ? ..au ww hufuatilii siasa za nchini hapa
 
Sasa mjomba Magu si alibana mianya yote ya wapigaji...

Lakini sasa msikilize bwana January anakwambia miaka mitano mitambo ilikuwa haizimwi kupisha kufanyiwa matengezo ya lazima (uongo mweupe kabisa...)
Wamechelewa. Magu alishatupa siri zote za migao ya umeme. Nilisema hii nchi atakayekuja kuongoza baada ya Magu atapata shida sana. Walikosea sana kumpa mtu nchi ambaye sio mwanasiasa.
 
Back
Top Bottom