Kimeumana Bungeni! Spika Ndugai ahoji kama kuna mgao wa umeme nchini

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
3,502
2,000
Spika Job Ndugai amehoji tatizo la kukatika kwa umeme nchini na kuitaka kamati ya nishati kukutana haraka na bodi ya mpya ya Tanesco ili kuwaeleza kazi kubwa iliyoko mbele yao.

Sakata hilo liliibuliwa na mbunge wa Kilombero mh Abukary Assenga aliyetaka kujua ni kwa nini Tanesco wanakata umeme kila jumanne na Alhamis jimboni kwake.

----
Licha kukiri kuwepo kwa adha ya kukatika kwa umeme kwa mara nyingi nchini, lakini Serikali mesema hakuna mgawo wa umeme Tanzania.

Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato ameliambia Bunge leo kuwa, hakuna mgawo wowote wa umeme nchini kwa sasa.

Hata hivyo Spika Job Ndugai ameagiza kamati ya Nishati na Madini wakutane haraka na Wizara hiyo na Bodi mpya ya Nishati ili wajue ukubwa wa kazi iliyo mbele yao maana kukatika kwa umeme ni tatizo nchini.

Awali mbunge wa Kilombero, Abubakar Asenga alitaka Wizara kueleza sababu za msingi ni kwa nini umeme katika wilaya hiyo unakatwa siku za Jumanne na Alhamisi na kusababisha adha kubwa.

Mbunge wa Sengerema Hamisi Tabasamu amedai katika jimbo lake umeme hukatika mara 10 hadi 30 kwa siku bila kujua sababu za msingi na akaomba waunganishwe na umeme kutoka laini ya Geita.

Chanzo: Mwananchi
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
58,445
2,000
TANESCO inapaswa ifumuliwe yote, inaonekana baadhi ya watumishi wa Tanesco wanaihujumu Serikali, hivyo waziri na watendaji wake watupie jicho kila kona ya Tanesco

Hakuna Tanesco anayeihujumu serikali wewe, usiwasikilize hao kina Makamba na stori zao...

Nchi hii wanaokula nchi ni viongozi na michongo yao, huo unaoona mgao unakuta ni watu wanataka kuuza dizeli na majenereta...

Jaribu tu kufikiria hii nchi ina minara mingapi ya simu, fanya robo tatu ya minara yote nchini ina Diesel Generators, na hizo DG's ili zitembee zinahitaji diesel...na tanks za DG za minara kwa wastani huingiza lita 500 ambazo hulast within a month tu...

Ukiacha hilo, hiyo Tanesco ina madeni chungu nzima yaliyosababishwa na hao hao wanaohoji kukatika kwa umeme huko bungeni kutokana na mamikataba ya kiduanzi...
 

bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
4,054
2,000
Hakuna wizara iliyoongozwa na January ikafanikiwa, huyu dogo anachojua ni kutengeneza michongo ya kupiga tu.
Kwani amewahi kuongoza wizara ngapi?
  • Sayansi na teknolojia alikuwa naibu waziri (hakuwa na mamlaka ya uamuzi)
  • mazingira alikuwa waziri katika ofisi ya makamu wa rais (hakuwa na mamlaka kamili ya uamuzi)
..... nyingine?
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
59,584
2,000
Hakuna Tanesco anayeihujumu serikali wewe, usiwasikilize hao kina Makamba na stori zao...

Nchi hii wanaokula nchi ni viongozi na michongo yao, huo unaoona mgao unakuta ni watu wanataka kuuza dizeli na majenereta...

Jaribu tu kufikiria hii nchi ina minara mingapi ya simu, fanya robo tatu ya minara yote nchini ina Diesel Generators, nna hizo DG's ili zitembee zinahitaji diesel...na DG za minara kwa wastani huingiza lita 500 ambazo hulast within a month tu...

Ukiavha hilo, hiyo Tanesco ina madeni chungu nzima yaliyosababishwa na hao hao wanaohoji kukatika kwa umeme huko bungeni kutokana na mamikataba ya kiduanzi...
Ohh mabwawa maji yamepungua

Sasa inabidi tutumie mitambo tuzalishe umeme😂

Soon utasikia hiyoo

Ova
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom