Kimbelembele cha CHADEMA kimewatokea puani

Ngoja nikusaidie picha za watoto....

A%5B1%5D.JPG

Vizuri sana mkubwa.Kama zipo zingine tupia mkuu.
 
Mwaka huu kazi ipo kwa hiyo tusadiki pasi ushahidi kuwa kihelehele kimewaponza .....eti watu wachache bila kulinganisha na watu wa wapi

Tambua kuwa tanga Chadema ndiyo wanaanza huwezi linanganisha na sehemu ambazo wananchi wamaesha komboka kifikra kama Mbeya, Iringa kifipi miji mikuu huwezi linganisha na vijijini
 
Ugonjwa wa Propaganda ni mbaya!!! Badala ya kuleta hoja za kuwakomboa wakulima wa Bongo ambao ni 80% mnaendeleza Propaganda tuu Nilifikiri thread kama hii inajibu matatizo halisi ya wakulima wa Mkonge, kumbe upambe tu. shit!
 
Historia yangu inanikumbusha kuwa vibarua wa mashamba ya mkonge, chai na miwa walikuwa wanatoka sehemu za mbali na yalipo mashamba, anachotetea Mh. Zitto kina mantiki si kwa wakazi wa Tanga bali hata maeneo ya mbali kama kwa Wasafa, Wafipa nk. Huwezi juvunia uchumu kukua pasipo shughuliza za uzalishaji mali kuonekana. Mtoa mada aendelee tuu kucheza bao kwa kuwa ana pesa ya nyanya chungu na dagaa haitaji kufanya kazi
 
Mimi kama mwanachama wa kilimo ninatilia shaka reasoning yako! Umuhi wa hoja haupimwi kwa mahudhuri ya watu peke yake kama unavyotaka kutuaminisha!

Kilimo ndio kinachotoa zaidi ya asilimia 90 ya ajira TZ. Lakini wewe pia ni shahidi kwamba kilimo ndio sekta inayodharaulika kuliko zote. Yaani "mkulima" ni tusi kwa vijana wa Tanzania, kama huamini mwambie kijana yeyote mtaani kwenu hivi "we mkulima nini?" au "we mkulima tu", usipopigwa ngumi ujue umeogopwa.

Najaribu kukupa picha tu ya watanzania. Nakumbuka mwaka fulani bei ya kahawa iliposhuka watu walikata miti. Jan Waziri mkuu analia na bei ya korosho.

Nadhani tatizo si CDM ni sera mbovu. Watu wakichukia mkonge haimaanishi kwamba sasa kila mtu afunge mdomo, kama CDM wanatumaini jipya kuhusu mkonge ninatilia shaka mantiki ya kuandika kwamba watoto tu ndo walihudhuria. Nadhani unahitaji kukishughulisha kichwa chako vizuri juu ya hoja hii.

NB: Hekima ya mtu mmoja haipinduliwa na upumbavu wa watu mia kwa idadi yao.
Kelele Zote ambazo Zitto,mnyika,pro-cdm mulizokuwa munapiga kuhusu mkonge nilijua wananchi wa Tanga wapo upande wenu kumbe kimbelembele chenu ndicho kilichokuwa kinawasumbua.
Wananchi wa Tanga hawapo tayari kuhusika kwenye kilimo cha MkONGE,ushaidi wakimazingira unaonesha wazi kabisa jinsi wananchi walivyokataa kuitikia kwenye mkutano wa CDM.Picha zilizooneshwa kwenye media mbalimbali utagundua ninachonena.
Kwanza,mkutano uliuzuliwa na watu wachache,tofauti na mikutano mingi ya Cdm.
Pili,hata hao tunaosema ni wachache kwenye uchache wao huohuo watoto wadogo ambao hawawezi kupiga kura hata baada ya 2015 kufikia ndio walikuwa weng kuliko hao watu wazima.
My take:
-kesheni mukiomba wa CDM cha chenu kiwe na mvuto sehemu mbalimbali ya Tz.
-Wabunge wenu wasipende kutia chapuo vitu ambavyo hawajafanyia uchunguzi.
 
CDM ni wachemfu sana, hilo mie nalijua tangia long time. Ila wachache wasio jua na ambao hufuata mkumbo kibubusa ndio waliobakia huko. Ngoja uone watakavyo kuja juu muda si mrefu


Sasa mlitaka wote wawe na nyie huko CCM?
Bakini huko pa tangu miaka 50 ya uhuru,bado nchi yetu ni changa... Mpaka tuje kutambaa,itakuwa karne 2 zijazo!

Bakini huko wasipochemka... BAKINI!
 
Kelele Zote ambazo Zitto,mnyika,pro-cdm mulizokuwa munapiga kuhusu mkonge nilijua wananchi wa Tanga wapo upande wenu kumbe kimbelembele chenu ndicho kilichokuwa kinawasumbua.

Wananchi wa Tanga hawapo tayari kuhusika kwenye kilimo cha MkONGE,ushaidi wakimazingira unaonesha wazi kabisa jinsi wananchi walivyokataa kuitikia kwenye mkutano wa CDM. Picha zilizooneshwa kwenye media mbalimbali utagundua ninachonena.
Kwanza, mkutano uliuzuliwa na watu wachache,tofauti na mikutano mingi ya CDM.

Pili,hata hao tunaosema ni wachache kwenye uchache wao huohuo watoto wadogo ambao hawawezi kupiga kura hata baada ya 2015 kufikia ndio walikuwa weng kuliko hao watu wazima.

My take:
-kesheni mukiomba wa CDM cha chenu kiwe na mvuto sehemu mbalimbali ya Tz.
-Wabunge wenu wasipende kutia chapuo vitu ambavyo hawajafanyia uchunguzi.

Mimi ni mwana CCM lakini ningependa kuhoji:
  • Umati wa watu unatumikaje kama kigezo kikuu cha kubaini iwapo wananchi wa Tanga wameitikia au hawajaitikia wito wa Zitto kwa serikali kushughulikia zao la mkonge Tanga?
  • Iwapo hicho ndio kigezo cha muitikio, maana yake nini sasa kwa serikali - isishughulikie yale iliyo ahidi bungeni?
  • Kidogo mimi hili lina nitatiza kwani kwa upeo wangu ambao pengine ni duni, suala la kilimo cha mkonge Tanzania sio suala la kisiasa, bali ni suala la kiuchumi, ambalo ingawa limepelekwa bungeni na Chadema, inatakiwa sote tuliangalie beyond partisan politics, hasa iwapo hoja za Zitto bungeni juu ya umuhimu wa zao hili kwa uchumi wetu bado inasimama.
Vinginevyo nasimama kupingwa.
 
Wambea mpooooooooooo...... tupoooooooooooo....... kusutwa sunnnnnnnnaaaaaaa!!!!!
 
Back
Top Bottom