Ushauri wangu kwa Chadema

SUTAGI-

JF-Expert Member
Nov 9, 2018
269
511
Nianze kwa pongezi kwa vyama vyote vya siasa kwa kupokea "go ahead" ya kufanya mikutano ya hadhara baada ya katazo la muda mrefu.

Nimpongeze pia Rais Samia Suluhu kwa uamuzi huo wa busara.

Zaidi nimpongeze Mwenyekiti wa CDM Mheshimiwa Mbowe kwa hekima na busara kubwa ktk kukiongoza chama kikuu cha Upinzani kwa kipindi chote cha zuio la mikutano ya kisiasa na vurugu zingine zinazoshabihiana na hayo.

Lengo langu ni ushauri kwa CDM kama chama pinzani kilichojipambanua ktk kuwapambania wananchi.

Katika kutekeleza jukumu lenu la kufanya siasa za majukwaa nawaomba mzingatie yafuatayo kwa ustawi wa chama chenu na Taifa letu.

1. Mikutano ya sasa ya siasa ijikite ktk kuwashukuru wananchi kwa sapoti yao kwenu kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2020 na kuelezea sababu zilizofanya kuchukua uamuzi wa kususia chaguzi zingine zilizojitokeza.

Wananchi waelezwe kwanini CDM haiwatambui wale akina Mama 19 waliopo bungeni.

2. Mikutano ihamasishe wananchi kuhusu umuhimu wa Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi pia waelezwe madhara yote yaliyojitokeza kwa sababu ya Katibu yetu iliyopo.

3. Epukeni kuweka msimamo wa wazi unaomuhusisha Marehemu Magufuli na yaliyojitokeza kipindi cha utawala wake bali ilaumiwe serikali ya kipindi hicho. Hii itawatengenezea wananchi imani ya kujua mbaya wao ni CCM na si mtu.

4. Kwa sasa epukeni kuzungumzia utekelezaji mbovu wa miradi, ugumu wa maisha, bei za vyakula kuwa juu, bei za mafuta na ufisadi uliopo serikalini badala yake tumieni majukwaa mbalimbali kukusanya taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu utekelezaji mbovu wa miradi.

Taarifa hizo zitumike mwishoni wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi mbalimbali.

Kuibua taarifa hizo kwa sasa itawapa nafasi kubwa CCM kurekebisha mapungufu yao na kwa bahati mbaya wananchi wetu ni wepesi wa kusahau makosa ya CCM mara tu wanaporekebisha makosa hayo pia wananchi wetu ni wepesi wa kuzoea na kusahau ajenda za vyama pinzani.

5. Endeleeni kusajiri wanachama wapya hususani vijijini, kujaza nyomi kwenye mikutano yenu kusiwafanye mbweteke.

Pandeni itikadi zenu kwa wananchi wa chini kwa sababu wengi wenye status za juu wanajua umuhimu wenu na wanatamani kuwaunga mkono lakini si washiriki wazuri wa mikutano ya siasa na walio wengi si wapiga kura.

6. Tundu Lisu arejee nchini mwaka mmoja kabla ya uchaguzi, na awe mgombea wenu wa Uraisi. Yeye aje kuibua ajenda za maisha magumu wanayopitia Watanzania.

7. Umakini unahitajika ktk kuzungumzia mabaya tu ya The Late Magufuli..

kumbukeni wafuasi wake wamejeruhiwa na baadhi ya kauli na matendo ya viongozi waliopo serikalini na kwenye chama chake, ni wajibu wenu kuona hiyo fursa ya kundi hilo la wapiga kura na kuwa na mkakati wa kuwa_win.

8. Msidharau vyama vingine vya upinzani na epukeni kauli za kuvidharirisha au kuvitweza, hata hivyo mnaweza kuwa na muungano wa vyama vingine ktk uchaguzi ujao lakini umakini zaidi uzingatiwe katika kufikia uamuzi huo.

Kipindi kigumu tulichopitia kiwe funzo kubwa kwenu katika kuainisha watu wa kushirikiana nao na kushirikisha mipango yenu.

Mungu ibariki CHADEMA, Mungu wabariki Watanzania wafunguliwe ufahamu kuwa tunahitaji mabadiliko ili kuleta ushindani chanya katika siasa, utakaozaa maendeleo ya wananchi wote na si watu wachache watakaojiona wana mamlaka na haki zaidi ya wananchi wengine.
 
Back
Top Bottom