Hae Mosu

Member
Dec 23, 2019
36
25
Salaam! Sisi baadhi ya wakazi wa mtaa wa Kimanilwentemi kata ya Bugogwa WILAYA ya Ilemela Tuna tatizo ambalo tunahisi Kuna harufu ya rushwa. Iko hivi, Kuna shule ya serikali imejengwa hapa mtaani inaitwa shule ya SEKONDARI IGOGWE.

Eneo la shule hii ni dogo na ilionekana kuwa inapaswa eneo liongezwe Kwa kuchukua maeneo ya wananchi. Sis tuliona ni kweli Kuna uhitaji wa kuongezwa eneo la shule kwani shule hii Inahitaji kuwa na mabweni ambapo Moja limeshajengwa kwenye eneo la mwanachi hata kabla hajafanyiwa tathmini ya eneo lake. Tunachosikitika ni Kwamba tulikubali kutoka maeneo YETU na tulizuiwa kuyaendeleza Toka mwaka 2020 na hivyo tukasubiri kuja kufanyiwa tathmini.

Tathmini ilifanyika mwezi wa saba mwaka huu 2023. Tuliambiwa kuwa Kwa ardhi, mita Moja ya mraba itakuwa ni shilingi 5000/= miti ya matunda 100,000, Kila migomba mitano ilikuwa inahesabika kama shina Moja Kwa 35,000, na katani (mkonge) Kwa 4500 na MENGINEYO. Sasa kabla hatujapewa jumla YETU tulianza kutishiwa na mkuu wa shule hii Mwalimu Athanas na mtendaji wa kata ya Bugogwa kuwa iwe isiwe kuwa lazima maeneo YETU yachukuliwe na Kwa GHARAMA YOYOTE watakayoamua wao.

Mwezi uliopita tuliitwa halmashauri ya Ilemela na Afisa ardhi na tukaambiwa kuwa serikali imebadili utaratibu wa kulipa fidia na hivyo ardhi italipwa Kwa 3,500 Kwa Kila mita Moja ya mraba na pia vitu vingine kama majengo, miti, na vingine vyote walikadilia tu bila kutupa mchanganuo.

Sasa tunawaimba RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN na WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA mtusaidie Ili tupate stahiki zetu. Kwanikwa tathmini ya mwanzo tulivyokokotoa ni Kwamba tungepata pesa kubwa kidogo ila Sasa hivi pesa tuliyolazimishwa Kuisaini ni kidogo mno na wanatumia mabavu.

Hivyo, tunaomba msikie kilio chetu.
 
Salaam! Sisi baadhi ya wakazi wa mtaa wa Kimanilwentemi kata ya Bugogwa WILAYA ya Ilemela Tuna tatizo ambalo tunahisi Kuna harufu ya rushwa. Iko hivi, Kuna shule ya serikali imejengwa hapa mtaani inaitwa shule ya SEKONDARI IGOGWE. Eneo la shule hii ni dogo na ilionekana kuwa inapaswa eneo liongezwe Kwa kuchukua maeneo ya wananchi. Sis tuliona ni kweli Kuna uhitaji wa kuongezwa eneo la shule kwani shule hii Inahitaji kuwa na mabweni ambapo Moja limeshajengwa kwenye eneo la mwanachi hata kabla hajafanyiwa tathmini ya eneo lake. Tunachosikitika ni Kwamba tulikubali kutoka maeneo YETU na tulizuiwa kuyaendeleza Toka mwaka 2020 na hivyo tukasubiri kuja kufanyiwa tathmini. Tathmini ilifanyika mwezi wa saba mwaka huu 2023. Tuliambiwa kuwa Kwa ardhi, mita Moja ya mraba itakuwa ni shilingi 5000/= miti ya matunda 100,000, Kila migomba mitano ilikuwa inahesabika kama shina Moja Kwa 35,000, na katani (mkonge) Kwa 4500 na MENGINEYO. Sasa kabla hatujapewa jumla YETU tulianza kutishiwa na mkuu wa shule hii Mwalimu Athanas na mtendaji wa kata ya Bugogwa kuwa iwe isiwe kuwa lazima maeneo YETU yachukuliwe na Kwa GHARAMA YOYOTE watakayoamua wao. Mwezi uliopita tuliitwa halmashauri ya Ilemela na Afisa ardhi na tukaambiwa kuwa serikali imebadili utaratibu wa kulipa fidia na hivyo ardhi italipwa Kwa 3,500 Kwa Kila mita Moja ya mraba na pia vitu vingine kama majengo, miti, na vingine vyote walikadilia tu bila kutupa mchanganuo. Sasa tunawaimba RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN na WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA mtusaidie Ili tupate stahiki zetu. Kwanikwa tathmini ya mwanzo tulivyokokotoa ni Kwamba tungepata pesa kubwa kidogo ila Sasa hivi pesa tuliyolazimishwa Kuisaini ni kidogo mno na wanatumia mabavu. Hivyo, tunaomba msikie kilio chetu.
fungueni kesi mahakamani.
 
Mkiqmbiwa na Mwabukusi tuandamane tupate katiba mpya hamtaki. Uliona wapi mwananchi (bosi wa rais na waziri mkuu) anamlilia rais amsaidie?

Katiba inatamka wazi kwamba mamlaka yote yako mikononi mwa wananchi, hivyo mwananchi ulipswa kuwa ndiyo mwenye sauti kuliko rais na waziri mkuu .

Ingieni bararabarani na Mwabukusi tuondokane na ujinga huu!
 
Nchi hii bado ina watu wajinga sana,yaani mkuu wa shule anawapiga mkwara Mbuzi mnaogopa kudai haki zenu,mpaka Honorable causa na Mzee wa kuzindua Gereza aje atoa msaada kwenu.
 
Umeeleza vizuri na waziri mkuu ni mtu wa watu atawasaidia shida zenu, ila huyo mkuu wenu wa mkoa ni shida sijawhi kumwamini hata siku moja.
 
Back
Top Bottom